Nini kitatokea endapo jua litazima/ litapotea?

Kwa hakika itakuwa giza muda wote na hapo ubinifu utaongezeka maradufu na mianga itagunduliwa.
 
..Wewe ndio hujaelewa naposema huu uzi ni wa ku-provoke critical thinking! Kufikiri, sky is the limit, kutenda kuna mipaka. Msingi wa hoja yako ni kwamba kuna mipaka ya kufikiri, mimi nimekupinga. Suala la kuona kilicho nyuma, iliposemekana haiwezekani kuona kama udaivyo, WALIFIKIRI na kuja na njia za kuweza kuona nyuma in real time.
 
Jua likizima sasa hivi paap.

Hutakuwa na uwezo wa kujua hilo mpaka takriban dakika 8 na sekunde 20 zipite.

Utaendelea kuliona jua linawaka kwa dakika 8 na sekunde kama20 bila kuona tofauti yoyote.

Kwa sababu, huo ndio muda unaouchukua mwanga kusafiri kutoka kwenye jua mpaka kwenye jicho lako.

Ukiliangalia jua sasa hivi, hulioni kama jua lilivyo sasa hivi, unaliona jua kama lilivyokuwa dakika 8 na sekunde 20 zilizopita.

Kwa hiyo, muda wowote, hatuna uhakika kama jua lipo na linawaka, au limezimika.

Tunaweza kuwa na uhakika jua lilikuwepo na liliwaka takriban dakika 8 na sekunde 20 zilizopita tu.
 
Mitandaoni kuna maarifa mengi sana....lakini bahati mbaya vijana wetu wanasoma ili kufaulu mitihani
Kila kinachoandikwa ktk hili jukwaa (intelligence) kipo mitandaoni, unafikiri kwa nini hili jukwaa bado limewekwa hapa licha ya kuwa watu wanaweza wakaenda jichotea maarifa kimya kimya?
 
Bwana Yesu asifiwe.
 
Hii artificial sun ikiwashwa inacover umbali gani?
 
Kaka bado hujaelewa mzee. Kupinga kwako kuwepo kwa mipaka ya kufikiri ni uchache wako wa elimu na maarifa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119] ikiwa great thinker wapo hivi ngoja mi niendelee ku think great
 
Kaka bado hujaelewa mzee. Kupinga kwako kuwepo kwa mipaka ya kufikiri ni uchache wako wa elimu na maarifa.
Nimeelewa, tatizo ni wewe kutaka nifikirie kama wewe KUWA KUNA MIPAKA YA KUFIKIRI. Hii haiwezekani, nitabaki na msimamo wangu kuwa hakuna mipaka. Cha msingi ni logics, ila nimekuelewa.
 
Kwangu jua likizima, kitacho tokea ni kiza na mwanga hafifu na baridi isiyo pungua
Tukumbuke kuna chakula, ni mmea ule. Na mmea unahitaji mwanga wa Jua ili kujitengenezea chakula chake. Jua likitoweka mimea itashindwa katika ukuaji na itakufa, ikifa Hamna chakula.

Satellite nazo zitashindwa kufanya kazi, nguvu kazi yake inatokana na mionzi ya Jua.

Baridi itakuwa ni kubwa sana fikiria nchi kama Urusi,Korea kaskazini, Canada, sijui wataishije. Na baridi kwa ujumla wake ikitanda mfumo wa upumuaji wa binadamu unashindwa kufanya kazi vizuri. Watu wengi sana tutakufa kwa baridi, fikiria kama Makambako hali itakuaje. Dunia yote itakuwa ni barafu.
 
there will be no photosynthesis anymore, kwahiyo kutakua na mlundikano wa carbon dioxide na kutozalishwa kwa oxygen, hence death of living organisms will occur very fast due to lack of oxygen.
 
Itachukua kama dk 8 kabla watu hawajagundua kua jua halipo na itategemea hilo jua litapotea Kwa njia ipi na kama likitoweka basi kunauwezekano wa mabadiriko makubwa katika mwendokasi wa Dunia pia nafasi yake katika mzunguko.Refer universal law of gravitation kipi kitatokeo kama force itakuwa sawa na zero!?Dunia itaangukia anga za mbali kama haitogongana na sayari au magimba mengine pia inawezekana tukaishia kuvutwa na black bodies au tukajikuta kwenye solar system nyingine maana jua ni nyota na nyota zipo nyingi na kuna zero chance ya kiumbe yeyote kusalia kama hilo litatokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…