Nini kitatokea endapo jua litazima/ litapotea?

Imagine miaka zaid ya milion nyuma kuna jiwe lilidondoka duniani kutoka outer space.lilitimka vumbi la hatari anga yote ya dunia ikakosa mwanga wa jua kwa miaka 20.hii ilipelekea dunia yote kuwa barafu.
 
Kuna muvi nyingi tu za beyond imagination zinazohusu space, hivyo point yako siikubali kwa asilimia kubwa. Suala la kuona kilicho nyuma yangu ni simpo sana, unageuka basi unakiona, na kama ni kisogo ndio maana watu wakaja na vioo au kamera! Vioo zaidi ya kimoja ktk angle tofauti naweza ona kilichopo nyuma yangu in real time. Unafikiri waliokuja na wazo la kwenda ktk space, mwezini na sasa wamarekani wanataka kufanya the impossible kupeleka kifaa karibu kabisa na jua, bila hizi imagination wangeweza?
Hata hivyo, hii thread ni kwa ajili ya ku-provoke ideas endapo itatokea sababu kazi ya jua tunaijua ingawa kiuhalisia inasemekana haiwezi tokea.
 
Jua likizima au likitoweka dunia na sayari zengine zitaganda na kuwa barafu iliongumu zaidi ya chuma cha reli..no life.
 
Kaka jaribu kuelewa nilichokiandika,naposema huwezi kuona kilicho nyuma yako,hakuhitaji shule hapo ni kwamba hapo hapo ulipo kaa na ulipo elekea huwezi kuona kilcho nyuma yako.

Pili unajengea hoja juu ya movie huku ni kufikiri kimakosa. Nini asili ya movie ni maigizo kama maigizo mengine hupunguza katika ukweli na huongeza katika ukweli,kwahiyo hii si hoja dhidi ya kile nilicho kiandika.

Tuandike ukweli na uhalisia
 
Kwanza likizima ghafla kutatokea baridi ambayo itaondoa uhai wa viumbe karibu vyote bali probability ni kubwa sana kubaki kwa bactreias (pia oxygen itapungua kwa kasi na kisababisha vifo kuwa 100%). hii ni kutokana na ukweli kuwa joto linalotokana na jua huzuiliwa kwenye anga la thermosphere ili kuweza kusawazisha hali ya hewa ambayo ni rafiki kwa viumbe hai pia si hapo tu pia mimea itakufa kwa kushindwa kujizalishia carbohydrates wakaati wa mchana kupitia mwanga wa jua (photsynthesis) pia dunia na sayari nyengine zitakosa usawa kutokana na kukosa sehemu ya kuzungukia hivyo zitafuata njia mnyooko hadi zitakapokutana na jua jengine au sayari yenye ukubwa ambao inaweza kuzufanya zizunguke.
 
Did You Know?

In the TOWN BARROW in Alaska the sunset on November 18 & rises January 23.
Between this period there is total darkness in BARROW Town for 67days.

Ndicho kitakachotokea mkuu..
 

Kuna Mahali nilisoma inachukua dk nane na nusu Mionzi ya jua kufikia Dunia....
Je ni dakika zile zile kufikia Mwezi?
 
Mkuu kasome tena...jua sio chanzo cha gravity.
Pia kulijibu swali lako angalia faida za jua baada ya hapo zitoe zoote uone tutakuwaje...
 
1. Wanasayansi watalikarabati au watatengeneza jua lingine.
Hii ni kwa mujibu wa watu wasiotambua uumbaji wa Mungu mwenyezi.
Kwamujibu wa tunaemwamini Mungu,
2. Jua haliwezi kufa wala kuharibika maana Mungua alilitrngeneza lituletee mwanga kuotesha mimea nk, hadi siku ya mwisho wa dunia ambapo Mungu atuondoa duniani na kwenda kuishi naye kwake mbinguni.
Chagua jibu moja hapo juu.
 
Watu wote wataanza kufa baada ya masaa 168, hawatakuwa na nguvu ya kufanya chochote maana dawa inayotolewa na jua kwa binadamu ni mhimu sana.
 
jua likizama cha kwanza
1.Miti yote itakauka kwa kukosa energy ya kutengeneza chakula
2.Baridi litaongezeka na barafu sehemu yote ya dunia
3.Nguvu ya mvutano ya sumaku dunia itapotea na kusababisha balance ya dunia kupotea
3.Usiku utakuwa daima akuna mwanga
4.Binadamu tutakuwa zaifu kwa kukosa energy itokanayo na jua ni hayo tu ingawaje yapo mengi zaid na zaid
 
Unaona kinachotokea North Pole kule ambapo miale ya jua haipafikii kwa sana basi iwapo jua litazima basi tegemea dunia nzima kuwa vile!. Kila kitu kitaganda na kwa kuwa Jua ndio chanzo cha uhai basi hakuna maisha yatakayo endelea kuwepo popote pale!.
Mwanga toka kwenye Jua kufika duniani unatumia dakika 8 na sekunde 19 ina maana kwa makadirio nayoona Jua likizimika ghafla ndani ya siku 3-5 Dunia itakua kimya yote!!..
Jua kuzima ghafla ni kitu kisichowezekana kabisa, Lakini labda likizimika tuwape moyo wachina watutengenezee copy ya Jua lao 😀🙂

Ingawa kwa maendeleo ya sayansi ya binadamu, wenzetu huko walishaweza kutengeneza kitu chenye mwanga (artificial sun) ingawa sio na nguvu kama Jua (ni kazi kulifikia joto lile ukasurvive lakini kina nguvu kuikaribia jua!).

Scientists just switched on the world's largest 'artificial sun'
 
According to scientific calculation mwishowe jua litapungua nguvu baada ya kumalizika energy yake na kuwa kitu wanachokiita RED DWARF .
Ikifika hali hiyo halitakuwa na joto kama la sasa na kupelekea hewa yote duniani kuganda na kuwa barafu na ndio itakuwa mwisho wa uhai duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…