Uchaguzi 2020 Nini kitangulie, haki au amani?

Inahitaji akili kubwa sana kueleza kwa ufasaha dhana ya haki na amani.

1. Kuna nyakati watu hupigana ili kutafuta amani.
2. Vurugu sio kinyume/ (opposite of) cha amani.

Dhana ya Haki na Amani huwa aimuliwi kwa kuangalia kipi kinatangulia.

Kumbuka :- Amani ikiwepo inatoa nafasi kwa haki kutendeka, Haki ikiwepo inatoa uhuru na hakikisho la watu kufurahia amani.

Justice and peace is a two headed snake.
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Kwanini walikushambulia
 
Mmh watu hupigana wakitafuta amani mbona sio kweli, kwani kupigana huja mnapokubaliana au kutofautiana?. Penye amani ndo Penye mafanikio, penye maisha. Amani huzaa haki, na haki huendana na wajibu.
 
Unaniangusha, yani hujui vurugu hutokea pale ambapo panakuwa na uonevu/upendeleo?

Haki ikiwepo, amani nayo itakuwepo automatically.

Tanzania kuna amani ya kinafiki ambayo haijajengwa kwenye misingi ya haki, ni amani inayolazimishwa kwa mabomu ya machozi na kuweka watu ndani bila makosa, hasa pale wanapodai haki zao.
 
Mmh watu hupigana wakitafuta amani mbona sio kweli, kwani kupigana huja mnapokubaliana au kutofautiana?. Penye amani ndo Penye mafanikio, penye maisha. Amani huzaa haki, na haki huendana na wajibu.
Unapiganaje kutafuta amani wakati kupigana kwenyewe huondoa amani?!

Na hata kama ingekuwa watu wanapigana kutafuta amani, bado pia ulitakiwa kutafuta kwanini walipigana!!

Watu wanapohangaika kutafuta amani kwanza ndipo haki ichukue nafasi ni katika mazingira ambayo tayari amani imeshavurugika, na katika mazingira kama hayo, of course, no peace no justice!!!

Lakini katika nchi kama yetu tunatakiwa kutafuta na kutoa haki kwanza ili tusifikie kupigana kutafuta haki na hatimae kulazimika kutafuta amani kwanza ndipo haki itawale!!

Mababu zetu walipigana Vita Vya Majimaji sio kwa ajili ya kutafuta amani bali kutafuta haki ambayo ilipokonywa na Wajerumani na kuwafanya babu zetu kama viumbe dhalili!!

Kule Nigeria kulitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe in the name of Biafra War! Watu wa Biafra hawakuanzisha vita ile kutafuta amani bali walianzisha kupigania kile walichoona kukiukwa kwa haki zao!!!

Enzi za ubaguzi wa rangi kule SA vurugu zilikuwa haziishi!!

Vurugu zile za SA hazikuwa za kutafuta amani bali za kutafuta hakl ambayo iliporwa na makabaru na kuwafanya watu weusi kuwa ni watu wa daraja la chini!!

USA nako kumekuwa zikitokea vurugu! Vurugu zile zinatokana na kile kinachodhaniwa mamlaka kutotenda haki kwa watu weusi na wala sio vurugu za kutafuta amani!!!

Watu wa CCM wamekuwa wakiwaita wale wale wanaowasaidia kwa majina mabaya kama vile Mabeberu! Hasira hizi za wana-CCM bila kujali kama zina mantiki au hapana hazitokani na wao kuamini kwamba Mabeberu wanavuruga amani nchini bali zinatokana na wao kuamini Mabeberu wanaingilia mambo ya ndani ya Tanzania wakati mambo ya ndani ya nchi ni haki ya kimsingi ya any sovereign state!!!

Itoshe tu kusema kwamba, more often than not, ukiona pahala amani imetoweka basi hapo kuna haki ama imeporwa au haitekelezwi!!!

Hata ndani ya nyumba, amani hutoweka pale haki baina ya wanandoa inaposigidwa... ama mwanamke kutotekeleza wajibu kama mwanamke na hivyo kumnyima mumewe haki yake kama mume, au mume kutotekeleza wajibu wake kama mume na hivyo kumnyima mkewe haki yake kama mke!!

HAKUNA AMANI PASIPO NA HAKI, na hata ikiwepo, inakuwa sio amani bai utulivu ulio chini ya mafuta ya petroli ukisubiri cheche ndogo tu ya moto petroli iripuke na utulivu na kuunguzia mbali utulivu!!
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Haki maana yake ni nini? ni kwa upinzani kushinda ndipo inakuwa haki?
 
Basi tuhitimishe kwamba kwasababu Tanzania kuna amani basi haki ipoooo, but hapa si mbinguni useme kutakua na haki asilimiab100 buuhh!!!,ukifanyiwa madhila ukienda kushtaki unasikilizwa unapewa haki yako, au haki gani mnataka?
 
HAKI
Kwa Kigiriki inaitwa dikaiosyne, kutokana na neno asili dike yaani anayeelekeza na kwa hiyo pia mwongozo, utaratibu. Tofauti na nomos, yaani sheria inayoongoza wanyama pia, dike inahitajiwa na binadamu ili kuishi kwa utaratibu. Ni kinyume cha bie, ukatili, nguvu inayoangamiza. Dikaios (mwenye kujali haki), ni mtu anayemtendea kila mmoja haki yake. Dikaia zoe ni maisha ya kiutu yanayopingana na hybris (kiburi) na ushenzi.

Kwa Kilatini kutokana na neno jus, haki, linapatikana neno justus, mwenye kujali haki, na hatimaye justitia, iliyo adili la msingi la utulinalotufanya tumpatie mwingine anachostahili.

Maana ya haki inatofautiana Kwa kila utamaduni. Katika maana ya kwanza kabisa ambayo ilitafsiriwa na mwanafalsafa wa Ugiriki, Plato kwenye kazi yake Jamhuri. Kutokana na historia dhana mbalimbali zimegunduliwa.
..........................................
Amani ni hali ya raha na salama bila ugomvi; ni kinyume cha fujo au vita.

Mara nyingi hali za amani ya nje na amani ya ndani hutofautishwa.

Amani ya nje au amani ya kisiasa na kijamiiEdit

Amani ya kisiasa ni hasa kutokuwa na vita na mapigano kati ya nchi mbalimbali au kati ya vikundi ndani ya jamii. Kama kuna mgongano kutokana na tofauti ya upendeleo juu ya jambo fulani amani inatunzwa kama pande zote zinafuata sheria au kanuni za jamii bila kutumia mabavu.

Mara nyingi maana kuu ya "amani" ni hali ya kutokuwa vita kati ya nchi kwa sababu vita huleta uharibifu mkubwa kushinda aina nyingine za ugomvi.

Amani inaweza kutaja pia tendo la kumaliza vita kwa njia ya mapatano kati ya washiriki wa vita au pia kati ya washindi na washindwa wakikubali kumaliza uadui. (linganisha Amani ya Westfalia).

Tangu vita kuu za dunia kulikuwa na majaribio mengi kuhakikisha amani kwa njia ya mapatano kati ya nchi zote za dunia. Shirikisho la Mataifa lilianzishwa mwaka 1919 likashindwa kuzuia vita kuu ya pili ya dunia ikafuatwa na Umoja wa Mataifa ulio na shabaha ya kupunguza na kuzuia vita kwa njia ya ushirikiano.

Tunatakiwa kulinda amani ili kusonga mbele hata kiuchumi.

Amani ya ndani au amani ya kirohoEdit

Tangu kale watu waliona ya kwamba amani ya nje inaenda sambamba na amani ndani ya kila mtu. Penye hasira nyingi moyoni mwa watu ni vigumu kutunza amani ya nje.

Kwa sababu hiyo amani imekuwa jambo muhimu katika dini na falsafa.

Dini mbalimbali zina ujumbe kuhusu amani:

ndani ya roho wa mtu mwenyewe

kati ya Mungu na mwanadamu

kati ya watu

Credit : Wikipedia
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Amani ndio cha kwanza kwanza kwanza
 
Mmh watu hupigana wakitafuta amani mbona sio kweli, kwani kupigana huja mnapokubaliana au kutofautiana?. Penye amani ndo Penye mafanikio, penye maisha. Amani huzaa haki, na haki huendana na wajibu.
Nadhani hupo sahihi. Huenda unamaanisha utulivu. Huwezi kuwa na amani kama hakuna haki.

Unahitaji utulivu ili haki iweze kutekelezeka. Kukisha kuwa na haki, ndipo amani huja.

Amani huanzia moyoni kwa mtu. Utulivu ni hali ambayo hakuna vurugu, hata kama hakuna amani wala haki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Watu mnaojinasabisha na Tanzania Kwanza, ama kwa makusudi au kwa kutojua huwa mnachanganya dhana ya taifa na serikali!!!

Na kutokana na kuchanganya kwenu huko, mara kwa mara mmekuwa mkitetea serikali huku mkidhani mnatetea taifa!!!

Na kutokana na kuchanganya kwenu huko, mmekuwa mkichukulia watu wanaoipinga serikali ni kama wapenda vurugu na wasio na nia njema kwa taifa huku mkidhani wale madhalimu wa CCM na vibaraka wao ndio wanasimamia dhana ya utaifa!

Watu aina yenu huwa mnashau kwamba hata marais huwa wanayasaliti mataifa yao, na hapo ndipo utakapokuja kuona taifa na serikali na vitu viwili tofauti!!!

Kwa mfano, licha ya Watanzania kulalamika mara kwa mara kuhusu matendo ya PK kwa Tanzania, Magufuli ile kuingia tu madarakani akataka kuunda Uswahibu na Kagame yule yule anayeaminika kuwa mtu mbaya kwa taifa la Tanzania!!!

Pale Magufuli alifanya usaliti kwa taifa, na mtetezi wa kweli wa Tanzania kama taifa, alitakiwa kuukemea usaliti ule wa Magufuli bila kujali itikadi yake kisiasa!!

Thanks God, inawezekana hatimae Magufuli ama kayaona yale waliyokuwa wanasema watu dhidi ya Kagame au wana-Usalama wamempa A-Z why PK shouldn't be trusted na ndo maana inaonesha wazi hivi sasa JPM kamtupa mkono PK!!!
 
Back
Top Bottom