donniebrasco
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 887
- 774
Habari ndugu zangu.
Kuna jambo moja kubwa sana hususani hapa Tanzania naomba tusaidiane kuelewishana. Nini kipimo cha elimu ya mtu? Elimu ya mtu huwezi kupima tu kwa kiwango cha mfumo tuliowekewa na uliozoeleka. Ni kwa namna ipi tunaweza kupima elimu ya mtu?
Maana kuna baadhi ya watu ambao mimi binafsi nawajua, wanakuwa kweli wana elimu ambayo inawatosheleza; ila ni elimu inayo wasaidia wao kuweza kufanya kazi zao tu (yani 'professions).
Tukifuata mfumo huu huu mfumo wa elimu yani sekondari na vyuoni; kwa upande mwingine kuna watu ambao wamesoma kidogo tu yani basic kama ni "O" level au "A" level tu na hawakwenda elimu za juu (Vyuoni) - lakini wana upeo mkubwa sana wa kuelewa vitu na kuchanganua mambo binafsi. Hao pia nimekutana nao. Nafikiri ndugu zangu mmenielewa ninachomaanisha.
Sasa je tutumie kigezo gani kujua uwezo wa kielimu wa mtu alionao? Tuangalie level aliyofikia au tuangalie kila siku ya maisha yake anaweza vipi kuishi katika jamii na kufanya kazi zake? Au kuna kigezo ambacho nyie wenzangu mnaona kinaweza kutumika kuelewa zaidi kiwango cha elimu?
Narudia mimi binafsi nimekutana na vijana ambao wameishia tu "O" level lakini wako very smart kiasi unaweza kufikiri ana masters na pia makazini wanakuwa wako very sharp hata katika mambo mengine mbali mbali na pia nimeona wengine ambao wamepata masters lakini kuna mambo mengi wanashindwa kukabiliana nayo au hata kuchanganua vitu.
Naomba mawazo na michango yenu.
CC: gfsonwin, Maganga Mkweli, Kiranga, Nicas Mtei, Mentor, Mtambuzi, Smile, lara 1, MziziMkavu (Karibuni wakuu)

Last edited by a moderator: