Nini kinakuumiza kichwa katika biashara yako/zako?

Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
766
1,000
kweli wewe ndio boss mtu anakuja kuomba kazi anakwambia anaomba "Ajishkize" na kweli ukiangalia unahitaji mfanyakazi kama yeye,vipi utamuajiri au utamtakia safari njema huko aendako?
Mkuu siwezi kuajiri mtu anakuja kwangu kujishikiza. Mtu mwenye mentality ya kujishikiza hawezi kuwa na uchungu na kazi.
 

Mc cane

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,978
2,000
Kuna bosi mzuri sana somewhere ana shida ya mfanyakazi mzuri na mwaminifu sana

Kuna kijana/binti (mfanyakazi) mwaminifu na mzuri sana somewhere ana bosi kimeo balaa

Hii ni changamoto kubwa sana
 

financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,299
2,000
Hapana sikuwa mimi, ila ni kweli kwamba kuna vyakula/matunda hayafai kula kwa pamoja/wakati mmoja. kwasababu huchanganyika tumboni na kutengeneza SUMU.

Vitu kama hivi either unashauriwa usivile kwa pamoja au uengeze kitu chengine cha ziada ili kuvunja hiyo complex (sumu ambayo imejitengeneza)
Yeuwii natamani kufahamu kuhusu hayo matunda mkuu, huenda tunayatumia na hatujui kama yana madhara 😪
 

Cumudia

Senior Member
Sep 21, 2018
139
250
Tukiacha mambo ya kuajiri, tuje katika maisha mengine kabisa

Rayvanny enzi anaitwa Raymond unajua alikaa WCB kwa muda gani mpaka anatambulishwa rasmi kama member? Zuchu je?! Unajua alikaa WCB kwa muda gani mpk anakuja tambulishwa rasmi kama member official? Achana na hao

Tuje kwa MBOSSO unajua alisugua benchi kwa muda gani? Mbosso tena alikua WCB wenzake wanaenda show wao wapo tu hata sh 100 ya maji hana, alikua WCB lakini msoto aliokua anaupitia sio wa kawaida na sio kwamba huyo DIAMOND au kina tale walikua hawamuoni, walikua wanamuona daily. Kwanini sasa walikua hawamsaidii kum sign aanze pata pesa zake kupitia muziki wake/kipaji chake?!

Kwani Mbosso/Zuchu, Raymond na wengine wameanza kuonyesha vipaji baada ya kutambulishwa jamvini? Walikua na vipaji vyao tangu hukoo kabla hata ya lebo WCB haijulikani.

Unaweza nisaidia niambia kwanini walikua wanasita kuingiza wasanii wapya kwenye lebo mpaka wajiridhishe nae? Unazijua sheria na taratbu za mpaka kukubaliwa kuwa member wa WCB?? Kama ni msoto basi waulize wasanii wa WCB nini maana ya msoto watakueleza maana yake..

Huo ni mfano HAI ambao ni rahisi sana kueleweka, iko hivi mkuu mtu hawezi kukukabidhi ofisi yake usimamie kama hata huwezi simamia na tatua matatizo madogo madogo tu ambayo unakutana nayo ukiwa katika biashara yake.

Mtu unamkabidhi pikipiki/gari imsaidie katika kufatilia biashara zako, ila chombo cha usafiri anachokitumia yeye kwa zaidi ya asilimia 81 kinapata hitilafu "harekebishi" ana paki hapo, anakwambia kitu flani kimeharibika. Maana yake anataka mimi ndio nitengeneze.

Mtu unamuacha ofisini unasafiri, huku nyuma wanakuja TRA/TFDA wanakuta kasoro ofisini badala a solve tatizo halafu boss akirudi amueleze A B C D, yeye anaacha OFISI inapigwa kufuli wakati alikua ana uwezo wakuchukua hata 50,000 akawapa wale raia wakasepa boss akirudi unamuelezea ilikua hv hv hv, ila anakubali ofisi ifungwe halafu anarudi kulala nyumbani kwasababu anajua boss haupo na ofisi imefungwa.

Mkuu hamna mwajiri yuko tayari ajiri au muachia mwajiriwa ofisi aisimamie kama huyo muajiriwa hajielewi, kujielewa si tu katika utendaji kazi bora, ila kuna mambo mengi sana yanayoweza kukuonyesha huyu mtu anajielewa.

Mwajiri bora si yule anaetoa mshahara mkubwa, ingekua hivyo basi wahindi wasingekua wanalalamikiwa kila siku kuna vitu extra ambavyo mwajiri anataka avione kwa mwajiriwa wake lakini waajiriwa wengi wame-focus kwenye mishahara, ukitaka mfanyakazi afanye kazi sanaaa, atumie akili yake 99% kazini mlipe mshahara mkubwa jambo ambalo si sawa mfanyakazi anaekuwa bora kwasababu ya mshahara anaopokea huyo si mfanyakazi.

Biashara zina ups n down, vipi siku kampuni ikifilisiwa kabisa boss ukashindwa lipa hata wafanyakazi mishahara unafkiri kuna mfanyakazi ataebaki na wewe hapo? Mimi kuna wakati nachelewesha mishahara makusudi kabisa, sio kwamba nakuwa sina hela ya kulipa raia ila nachelewesha makusudi nione hali zao wangapi watamudu.

Kwahiyo mkuu hamna mwajiri anapenda kutesa wafanyakazi wake, HAKUNA ila kuna vitu waajiri wenye future wanatamani kupata wafanyakazi CREAM, unajua kuna wafanyakazi halafu kuna ile CREAM ya wafanyakazi ambao mpaka unampata mfanyakazi cream unaweza kaa kwenye biashara katika miaka mi 5 ukampata m 1.

Kuna vitu vingi mkuu ila mimi nataka tu ufahamu hamna boss anapenda tesa wafanyakazi wake labda huyo boss awe na mapepo tu.
You're right chief.
 

Cumudia

Senior Member
Sep 21, 2018
139
250
Unazungumza mambo mengi sana mkuu. Unashika hili unaacha.

1. Uvumilivu wa mfanyakazi biashara ikipitia downs: sasa biashara ikiwa njema unawapa peanuts then ukiharibikiwa unataka wastick na wewe? For what? Ugekuwa unawalipa vizuri wangeiona hali halisi na kuchagua wawe wavumilivu au wasepe. Its their right. Nothing you can do to force them.

2. Mwajiriwa akae benchi kwanza for a limited amount of time kabla ya kuanza kula raha mfano wcb singers. Understandable, Probation like. Ila at the end of the day walipwe according to the value that they offer. Sijaona ukigusia hili. Unataka probation iendelee forever? By the way, raymond, zuchu hawakuwa wakiingiza fedha wcb kabla ya kutambulishwa tofauti na staff wako ambaye ataanza kudeliver value from day 1 or else una matatizo kwenye hiring process yako.

3. Unatest loyalty ya wafanyakazi kwa kuwacheleweshea mishahara (stupid, childish, usiongee hili mbele ya watu wazima TENA). Dakika mbili mbele unasema hakuna mwajiri anayependa kutesa wafanyakazi wake makusudi. Can you see how silly it sounds? Limekaa kinafiki sana. Hao sio wake zako. Hamna mkataba wa shida na raha. Mna mkataba wa kudeliver value kwa malipo ya kiasi kadhaa kila baada ya siku zilizoainishwa.

4. Matatizo ya wafanyakazi. Kama hajielewi unaye wa nini? Sioni linaingiaje hapa. Kama hajielewi hata ukimpa mamilioni haitamfanya ajielewe.

5. Mfanyakazi anayefanya kazi vizuri kwasababu ya mshahara mkubwa sio mfanyakazi bora. Ni sawa na Unaniambia mfanyabiashara anayepambana kuimprove biashara yake ili apate faida sio mfanyabiashara bora.

Maoni yangu naona kuna tatizo la power play. Unajaribu kuexert your power over wafanyakazi wako kama mwajiri wao, ili uweze kupata as much as you can from them at minimum cost, instead of having clear roles and responsibilities and rewarding them according to their performance. Ndio hizo psychological manipulation za uvumilivu na loyalty zinapotokea.
Chief mtu anapozungumza haimaanishi yote ni ya msingi la muhimu ni kuchukua yaliyo ya muhimu tu, naona umemshukia kama Mwewe aliyeona kuku!?

Ila twende mbele turudi nyuma kupata mfanyakazi sahihi ni changamoto sometimes ukiwa unabiashara jitahidi kuwa mstari wa mbele kwa kila jambo.
Wasomi wanaita "balance/business score card",
yaani kama vile ukiwa una drive magari haya ya kisasa pakiwa na tatizo kwenye gari basi kwenye dashboard pale panaonyesha tatizo lilipo iwe kwenye tairi,engine au popote. sasa kwenye aspect ya kibiashara ishu za fedha, ununuzi, kodi, wafanyakazi, masoko, uzalishaji na usambazaji vyote yapaswa uvijue na uvisimamie vizuri, otherwise unahitaji watu sahihi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom