Nini kinaendelea ndani ya Klabu ya Simba?

Nini kinaendelea ndani ya Klabu ya Simba?

umeongea point sana na hii kitu sio tu kwa simb ahata yanga ikianza kukosa matokeo muda wowote ule mashabiki wataanza mdomo...nadhani hawa matajiri watengeneze vilabu vyao maana uwezo huo wanao
Ni ngumu kufanya biashara na club mpya
Simba na Yanga kwenye biashara ni kitu kikubwa
Ni rahisi kujitangaza zaidi ukiwa Yang au Simba
Binafsi sioni tatizo pale Simba, kimsingi wakumbuke walianguka na wakubali process waunde team ya ushindani.
Ila Kwa hawa mashabiki makelele yanawanyima wawekezaji utulivu na hivyo hii itavuruga Simba kiuchumi na utawala
 
Kabla ya kuzungumzia matatizo ya sasa ya Simba tuanze na kuangalia chanzo chake.
Wa kwanza kulaumiwa ni aliyekuwa waziri wa michezo wakati mchakato unaanza Dk. Mwakyembe, huyu ndiye anapaswa kubeba lawama nyingi kwani wakati mchakato unaanza yeye ndiyo alitengeneza kanuni na kuamua vilabu vya wanachama viweze kuuza hisa zisizopungua 49% kwa wawekezaji wasiopungua watatu lakini Simba iliingia kwenye mabadiiko na kumpa mwekezaji mmoja hisa 49 na yeye na vyombo vilivyopo chini yake kukaa kimya.
Wa pili kulaumiwa ni kamati iliyoteuliwa kuandaa mchakato wa mageuzi ya mfumo Simba, badala ya kutengeneza mfumo ili Simba ipate wawekezaji wenye nguvu ilitengeneza mchakato kwa ajili ya kumpa timu Mo Dewji na wengi wao walipewa zawadi ya kuwa wajumbe wa bodi ya Simba upande wa mwekezaji.
Watatu wa kulaumiwa ni wanachama waliopitisha mchakato wa mabadiliko na mabadiliko ya Simba, wengi uelewa wao ulikuwa mdogo ndio maana wakampa madaraka makubwa mwekezaji wakati alikuwa anamiliki hisa chache pia walikaidi amri ya serikali ya kuwa na wawekezaji wasiopungua watatu na kumpa mwekezaji mmoja na hata pale walipojitokeza wanachama wengine kupinga mchakato wakiongozwa na mzee Kilomoni walionekana maadui na kutengwa na klabu.
Wanne wa kulaumiwa ni viongozi waliokuwepo kwa sababu hawakuweka mbele maslahi ya Simba na kumkumbatia mwekezaji mmoja Mo dewji pia walikuwa na makubaliano ya kisirisiri na Mo Dewji kabla mchakato haujaanza mfano pale Aveva na Kaburu waliposaini mkataba wa udhamini wa Sportpesa pamoja na kwamba mchakato ulikuwa haujaanza Mo Dewji alijitokeza na kulalamika hakushirikishwa.
Mtu wa tano kulaumiwa ni Mo Dewji kwani alitanguliza maslahi yake badala ya kutanguliza maslahi ya Simba. Kabla ya kupewa asilimia 49 Mo alikuwa akiongea kwenye vyombo vya habari na kusema anataka Simba iwe timu inayoshindana na Al ahly pamoja na TP Mazembe na kulaumu Simba kuuza wachezaji wake bora lakini tangia ameingia kwenye uwekezaji Simba imeuza wachezaji wengi zaidi huku gharama za mauzo zikifichwa, mapato ya matokeo ya uwanjani yamekuwa yakifichwa na hata mapato na matumizi yanayosomwa kwenye mkutano mkuu wanachama hawapati nakala zake. Wakati Azam inataka kuingia mkataba wa udhamini kwa Simba na Yanga wa bilioni 40 kwa miaka 10 Mo Dewji alipinga na kusema Simba ina thamani kubwa kuliko yanga na kama Simba watakuwa na shida ya pesa yeye atawapa ila leo tunasikia anaidai Simba mabilioni ya pesa.
Tatizo kubwa kwa wanachama wa Simba ni kutokuwa na elimu ya uwekezaji na maswala ya fedha kiujumla na hata wale waliokuwa na elimu hiyo kukaa kimya.
Hesabu za Simba zinapaswa kusomwa na mkaguzi na siyo Mhasibu wa Simba lakini si tu mhasibu amekuwa akisoma taarifa za pesa lakini hesabu hizo hazikaguliwi. Baadhi ya wanachama wameamua kupeleka malalamiko ya pesa kukaguliwa BMT badala ya kupeleka malalamiko yao NBAA ambao wanasimamia taaluma ya uhasibu. Pia wanachama wameshindwa kuhoji kwanini mkaguzi alijitoa badala yake wameridhika na taarifa ya klabu yao.
 
Simba inaviongozi wengi wanaotunishiana misuli (Mangungu, Magori, Salim Abdala try again, Mohamed Dewji n.k), huku yanga wana Hersi Said ambaye anashughulikia mambo bila kuingiliwa na yeyote jbo kinasababisha utulivu uwepo.

Hivi ndivyo nionavyo.

Red black.
 
Mo kutaka kuhodhi Simba wakati kanuni hazimruhusu, sasa hivi wanataka kusimamia hata jukumu la kusajili wanachama wakati sio la kwao na pia katiba bado haijarudi.
 
Back
Top Bottom