Nini kinaendelea ndani ya Klabu ya Simba?

Nini kinaendelea ndani ya Klabu ya Simba?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Ni zaidi ya miaka minne sasa, mambo ndani ya klabu ya Simba yanaonekana kuwaendea kombo. Timu ambayo ilijenga heshima Afrika Mashariki na kutisha kwenye mashindano ya CAF, kila siku inaonekana kuzidi kupoteana.

1770365913746.png
Pamoja na changamoto za kiufundi na usajili, kuna jambo jingine linaloonekana wazi kwa macho ya mashabiki, migogoro kati ya mashabiki,na baadhi ya viongozi wa sasa, na viongozi wastaafu.

Uhalisia wa hali hiyo ulijidhihirisha baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Esperance Sportive de Tunis, iliyosababisha kuondolewa kwa Simba katika hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika. Baada ya mchezo huo, mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu, alishambuliwa na kunusurika kipigo kutoka kwa mashabiki wenye hasira kali.



1770364104878.png
Kila msimu mashabiki wanaambiwa, “tunaijenga timu.” Lakini ujenzi huu unaanza lini na unaisha lini? Wachezaji wanakuja na kuondoka bila mwendelezo, makocha wanabadilishwa kabla hata hawajatekeleza falsafa zao, na uongozi unaonekana kama unazima moto badala ya kujenga msingi imara.

1770364181237.png
Kinachokosekana kinaonekana si pesa, bali ni mwelekeo, utulivu, na dira ya wazi kwani tangu mambo ya transformation yazungumzwe hali bado iko kwenye mkwamo.

Ishu nyingine ni kuongezwa kwa mkataba wa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba SC, Zubeda Sakuru, ambapo baada ya mkataba wake wa awali wa miezi sita kumalizika, aliongezewa mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi, Mo Dewji, bila kuishirikisha Bodi ya Wakurugenzi kama inavyotakiwa kisheria, kwa kuwa uteuzi wa CEO hupaswa kupitishwa na Bodi.

Hali hiyo imeibua maswali miongoni mwa baadhi ya wajumbe wa Bodi kuhusu vigezo vilivyotumika katika kumuongezea mkataba huo kwa siri na iwapo aliyetia saini aliridhika kwa misingi gani kwamba anafaa kuendelea na nafasi hiyo, huku wengine wakieleza wazi kuwa hawaridhishwi na utendaji wa CEO wa sasa na wanaona hafai kuendelea kuwa Mtendaji Mkuu wa Simba SC.

1770364022100.png
Kuna taarifa pia Muwekezaji wa Simba SC, Mo Dewji, ametuma makubaliano ya kukopeshana (loan agreement) kwa CEO wa klabu hiyo, Bi Zubeda Sakuru, ili yasainiwe na kupelekwa kwa mkaguzi kisha kuthibitishwa na Bodi, hatua ambayo ingeifanya Simba Sports Club iwe na deni kwa mwekezaji wake, lakini hadi sasa makubaliano hayo bado hayajasainiwa baada ya kuchelewa kutokana na changamoto za kiafya za CEO na safari ya matibabu nje ya nchi, huku ikielezwa kuwa licha ya kurejea, bado hajasaini kwa sababu ya hofu kuwa kusaini kutaiingiza klabu kwenye madeni.

Nimesoma “TAARIFA KWA UMMA” zote 2 za Klabu ya Simba ambazo moja ilitoka kwa Uongozi wa Simba SC na nyingine kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi, Crescentius Magori, lakini hakuna hata moja iliyojaribu kujibu hoja zilizowasilishwa na wanachama wao.

Yametamkwa mambo mazito kumhusu Rais wa heshima na mwekezaji wa klabu, ndugu Mohammed Gulam-Abbas Dewji, ambayo binafsi nadhani yalifaa kujibiwa kwa hoja na si kwa vitisho. Badala ya kuona majibu ya kina yanayofafanua ukweli wa tuhuma hizo, kilichoonekana ni msisitizo wa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wanaotoa maoni yao.


Kusema watu watapelekwa Polisi kwa kutoa maoni yao ni kujaribu kuzuia uhuru wa kutoa maoni ambao upo kikatiba. Kama kweli watu hawa hawasemi ukweli wowote, kwa nini Bodi haijajibu kwa kukanusha uongo na kuleta ukweli wazi? Kwa nini wanaoshambuliwa ni watoa hoja badala ya hoja zenyewe? Maswali kuhusu kuzimwa kwa simu wakati wa usajili wa dirisha dogo, changamoto za mishahara, na madai ya kukopa fedha kwa ajili ya safari za timu ni mambo mazito yanayohitaji majibu ya wazi, si vitisho.

 
Tatizo mmeendekeza siasa kwenye mpira, huyo CEO anachaguliwa na CCM ulitarajia nini!!

Alikua chadema ila alipohamia CCM tu akapewa CEO Simba, meaning maamuzi ya nani anakaa hapo hufanywa na CCM wenyewe. Then mlitegemea alete mabadiliko wakati yeye yuko hapo kujaza pochi lake tu na ku assert control ya CCM waliomuweka.

Siku mkiacha kuchanganya siasa na mpira ndio tutaona mafanikio.
 
“TAARIFA KWA UMMA” zote 2 za Klabu ya Simba ambazo moja ilitoka kwa Uongozi wa Simba SC na nyingine kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi, Crescentius Magori, lakini hakuna hata moja iliyojaribu kujibu hoja zilizowasilishwa na wanachama wao.

Yametamkwa mambo mazito kumhusu Rais wa heshima na mwekezaji wa klabu, ndugu Mohammed Gulam-Abbas Dewji, ambayo binafsi nadhani yalifaa kujibiwa kwa hoja na si kwa vitisho. Badala ya kuona majibu ya kina yanayofafanua ukweli wa tuhuma hizo, kilichoonekana ni msisitizo wa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wanaotoa maoni yao
Ni sahihi, corporate communication ndio inataka hivyo kuanza kujibu tuhumu kwenye official communication kunaweza ingiza taasisi kwenye litigations.

Wapo sahihi kujibu hivyo maana malalamiko yana proper channels sio press conference wakati kuna mikutano rasmi, barua pepe, vikao vya matawini n.k

Uelewa wa mashabiki wa mpira bongo ni mdogo sana ndio maana timu ikifeli lawama kwa rais wa timu as if anahusika na mechi za kila siku.
 
Sasa hivi kuna Simba Mo , Simba Ngungu na Simba ya Ahmed Ali ( hii Simba ya AI)
 
Mahala timu yetu ilipo fikia ni pagumu sana tunahitaji hekima, busara, kuvumiliana, na kukubaliana kwa kila upande hasa kwenye uongozi tuweze kuinusuru timu, tukifanya mchezo tutapotea zaidi ya sasa tulivyo. Naamini kabisa hata wachezaji hiki kitu kinawatafuna sana maana nao hawawi na raha pindi wanapoona washabiki wana wasusa na kubakia wenyewe uwanjani bila washabiki. Tuungane na kukaa chini tuone wapi tulipo pakosea tuweze kujirekebisha na viongozi wakubali hali haiko sawa marekebisho yafanyike kwa hekima na busara bila ubabe wala utemi. Simba Nguvu Moja.
 
Ubora wa simba huwa unaimarisha ubora wa yanga , sasa yanga imebaki kama mtoto yatima , hii inaua ile nguvu ya kupambana , hizi timu mbili huwa zinasaidiana sana kufanya vizuri .
Huwezi kufananisha Yanga na timu aliyoinusuru kushuka daraja mara mbili
 
Mahala timu yetu ilipo fikia ni pagumu sana tunahitaji hekima, busara, kuvumiliana, na kukubaliana kwa kila upande hasa kwenye uongozi tuweze kuinusuru timu, tukifanya mchezo tutapotea zaidi ya sasa tulivyo. Naamini kabisa hata wachezaji hiki kitu kinawatafuna sana maana nao hawawi na raha pindi wanapoona washabiki wana wasusa na kubakia wenyewe uwanjani bila washabiki. Tuungane na kukaa chini tuone wapi tulipo pakosea tuweze kujirekebisha na viongozi wakubali hali haiko sawa marekebisho yafanyike kwa hekima na busara bila ubabe wala utemi. Simba Nguvu Moja.
Wachezaji wanachoangalia ni kibunda, mshahara, posho na Bonasi, vitu muhimu vya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu soka,
 
Binafsi naonà tatizo la Simba ni mashabiki
Hawa mashabiki huwà wanàpeleka shinikizo kwenye uongozi bila kuheshimu taaluma
Mashabiki walivyo wapumbavu wanasababisha wachezaji wazuri wanaondoka
Mfano mchezaji potential kama Onana, Ateba, Mukwala, wameondoka
Mashabiki hawaamini process wao wanataka matokeo
 
Binafsi naonà tatizo la Simba ni mashabiki
Hawa mashabiki huwà wanàpeleka shinikizo kwenye uongozi bila kuheshimu taaluma
Mashabiki walivyo wapumbavu wanasababisha wachezaji wazuri wanaondoka
Mfano mchezaji potential kama Onana, Ateba, Mukwala, wameondoka
Mashabiki hawaamini process wao wanataka matokeo
umeongea point sana na hii kitu sio tu kwa simb ahata yanga ikianza kukosa matokeo muda wowote ule mashabiki wataanza mdomo...nadhani hawa matajiri watengeneze vilabu vyao maana uwezo huo wanao
 
Back
Top Bottom