Bwaga ya moyoni
Senior Member
- Aug 21, 2012
- 147
- 76
Niliposoma kuwa kuna waandishi wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya tresspass kwa kutaka kuripoti mazungumzo ya mpaka kati ya nchi yetu na Malawi nikapata picha kuwa kunaseriousness katika hili suala.
Hawa Wamarekani na Waingereza wanaenda kwenye viongozi dhaifu.Tony blair ndiye aliyeshawishi tuuziwe rada ili kulinda ajira za watu mia mbili ambapo alipingwa hata na mawaziri toka chama chake,ndiye aliyelazimishwa uk kuingia kwenye vita vya irak wenzake walikataa akapata sapoti ya conservative.siyo mtu mzuri siku zote chama cha labour kimekuwa na mahusiano mazuri na nchi za kiafrika lakini chini ya uongozi wake imekuwa kinyume na hata mgogoro wa zimbabwe ulipamba moto wakati wake baada ya kukataa kutambua makubaliano yaliyofikiwa na serikali zilizopita juu ya mgogoro wa ardhi.anapenda kuwashirikisha marais vibaraka kwenye foundation yake kwa hiyo lazima tuiangalie ziara yake kwa jicho la tatu.
Original Poster,
Kama wakubwa wa dunia hii wanatembelea Malawi wewe ndiyo labda ufafanue inakuhusu nini hadi ulete thread kama hii.
Kwani Malawi imeanza kutebelewa leo?
OK, kama inaleta alert, wewe tatizo lako ni nini hata kama dunia nzima inawatembelea na hawakutembelei wewe?
Au una kinyongo cha Rais wako kukata mbuga dunia nzima na ukadhani relfection kwako ukadhani lazima state visiting nazo ziwe nyingi kuliko Malawi? Fafanua na jipange vizuri.
Wewe ndiye utuambie ni nini attention uliyoweka kuhusiana na Malawi wakati sisi wengine tunaona ni jambo la kawaida.
tony ndiye aliyetuuzia 'rada' kimtindo, au sio mbwana eeh! sasa anaenda kumwambia 'sister' akubaliane na maamuzi ambayo mpaka sasa "WAMALAWI WAMESHAUMIA" kuwa wakifanya makosa kwenye maamuzi, TZ inaweza kuikolonize malawi, ninamaana malawi itachapwa, kiongozi wa nchi atafurushwa blatrye, na TZ itachimba mafuta na gesi ziwani kufidia vita, by the time wanyasa watapokea oder toka dodoma, kimsingi wanaenda kupewa plan "B" ya budget yao.
Blair ana ujumbe mzito toka kwa muwekezaji wa symbion power.
Nikupateje, maamuzi yakitoka unitafute ikiwa yatakuwa tofauti na mtizamo huo hapo juu.
Litaandaliwa dawati la mazungumzo kana kwamba tuyachimbe mafuta na gesi kwa pamoko kwa faida ya prince harry.
OVER.
Kama utatoka uamuzi wa kuchimba mafuta kwa pamoja kwenye Lake Malawi basi Tanzania ndiyo itakuwa imepata aibu. Kwa sababu aliyepiga marufuku yasichimbwe kwa sasa ni Tanzania wala si Malawi.
Wanachoeleza Malawi ni kwamba ziwa lote liko kwao, lakini hawajawahi kukataza shughuli ya uchumi isifanywe na Tanzania humo tangu enzi za Kamuzu Banda.
Kama utatoka uamuzi wa kuchimba mafuta kwa pamoja kwenye Lake Malawi basi tanzania ndiyo itakuwa imepata aibu. Kwa sababu aliyepiga marufuku yasichimbwe kwa sasa ni Tanzania wala si Malawi.
Wanachoeleza Malawi ni kwamba ziwa lote liko lakini hawajawahi kukataza shughuli ya uchumi isifanywe na Tanzania humo tangu enzi za Kamuzu Banda.
ushahidi uliuweka mwenyewe humu kuwa kuna visiwa viwili ambavyo kijiografia vipo karibu zaidi na tz kwa maana ya kati ya ziwa, kuliko ilivyo nyasa/malawi, nasi hatukuwahi kudai hivyo visiwa kwa msingi wa "mpaka upo kati ya ziwa"
Kwa kuwa "sister" aliitangazia dunia kuwa ziwa lote ni la wamalawi, itakuwa imempata aibu ya kutosha, mkuu Nikupateje, hilo dawati la stori litakuwa ni jaribio ambalo nalo tutalipiga chini, wakipata mafuta kwenye kipande chao cha maji iwe heri kwao, nasi tunawapa chevron texco watutolee crude oil (first class) kwenye eneo letu. Wera weraaaa!
kwa kuweka kumbukumbu sawa ni kuwa hatukuwahi kukataza eneo la nchi ya watu lisitumiwe na wenyewe!
Rekebisha kauli yako. Unaposema Joyce Banda aliitangazia dunia kwamba ziwa lot eliko kwao hii siyo habari kwani hakuna asiyejua tamko la Malawi kabla hata haijapata uhuru. Hawajawahi kubadilibadili kauli kama wenzao.
Kila kisiwa kilichomo kwenye ziwa lile ni cha Malawi bila kujali kiko karibu na Malawi, Tanzania au Mozambique.
Sasa kama mafuta yapo kwenye hivyo visiwa ungezuiaje wakati unakubali kuwa ni vyao. Hoja yangu ya visiwa ilikuwa ni kwamba wewe mwenyewe hujawahi kuvidai na shughuli za mle visiwani hazijawahi kuwa zako.
Leo unakataza mtu asifanye shughuli yake kwa vigezo gani?
Sasa, kikao kinakiwsiha leo kule Mzuzu, wala usiwe na papara. Kufikia kesho jioni au Jumatatu asubuhi tutajua kilichojiri. Na wale wenzako ambao huwa hawapendi kujisumbua ndipo post zao zitakapofurika wakiwaita wajume wa Tanzania kuwa ni wasaliti.
Wewe unachekesha!Kama utatoka uamuzi wa kuchimba mafuta kwa pamoja kwenye Lake Malawi basi Tanzania ndiyo itakuwa imepata aibu. Kwa sababu aliyepiga marufuku yasichimbwe kwa sasa ni Tanzania wala si Malawi.
Wanachoeleza Malawi ni kwamba ziwa lote liko kwao, lakini hawajawahi kukataza shughuli ya uchumi isifanywe na Tanzania humo tangu enzi za Kamuzu Banda.
SERIOUSNESS: Malawi kwenye mkutano huo ina wawakilishi 40 miongoni mwa hao kuna makamanda wa jeshi, polisi na usalama wa taifa
Kwa upande wetu sisi Watanzania tuna 24. Hatujapeleka hata mtu mmoja wa usalama. Na kiongozi wa juu kabisa kiserikali wa wawakilishi wetu ni balozi wetu nchini Malawi.
MAJADILIANO ILIPANGWA YAISHIE JUMATANO. HATA HIVYO HAWAKUPATA MUAFAKA. Ndo wakaendelea hadi Alhamisi. Inasemekana Alhamisi pande hizo mbili zilitumia mwenendo tofauti na wa awali, hapakuwa na mapumziko ya chai, Wamalawi walikusanyika kivyao na Watanzania kivyao
Pia baada hii taarifa ya kinachojiri hapo mkutanoni kuvuja, waandishi habari wawili walikamatwa na polisi
My take: Tuombe Mungu shetani rushwa ashindwe ukizingatia kila siku tunasikia madudu mapya ya viongozi wetu vinginevyo mpaka Alhamisi matumaini yalikuwepo
tony ndiye aliyetuuzia 'rada' kimtindo, au sio bwana eeh! sasa anaenda kumwambia 'sister' akubaliane na maamuzi ambayo mpaka sasa "WAMALAWI WAMESHAUMIA" kuwa wakifanya makosa kwenye maamuzi, TZ inaweza kuikolonize malawi, ninamaana malawi itachapwa, kiongozi wa nchi atafurushwa blatrye, na TZ itachimba mafuta na gesi ziwani kufidia vita, by the time wanyasa watapokea oder toka dodoma, kimsingi wanaenda kupewa plan "B" ya budget yao.
Blair ana ujumbe mzito toka kwa muwekezaji wa symbion power.
Nikupateje, maamuzi yakitoka unitafute ikiwa yatakuwa tofauti na mtizamo huo hapo juu.
Litaamdaliwa dawati la mazungumzo kanakwamba tuyachimbe mafuta na gesi kwa pamoko kwa faida ya prince harry.
OVER.
kiongozi, una hakika hatujapeleka mtu wa usalama? bongo hata mkutano wa kitongoji usalama wanatinga ndio itakuwa mkutano mkubwa kama huo. katika hao 24 usalama hawakosekani (manake ni zaidi ya mmoja) ila wamevaa kofia nyingine tu.
"Imezuiliwa Juu na Chini..........Kutokusoma ni Makosa"