Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,480
- 5,506
Kuna watu wenye maoni tofauti kuhusu hali ya kiuchumi ya Tanzania. Kuna wanaofikiri kwamba uchumi wetu kama taifa unayumba na kuna ambao wanasema kwamba uchumi unakua. Katika hali ya kawaida kabisa ni lazima kila anayetoa hoja awe na sababu za msingi na ambazo zitahakikisha kwamba hoja inaeleweka na hatua stahiki zinachukuliwa.
Katika moja ya mapitia yangu nilikutana na hoja ndogo ya usimamizi wa uchumi ambayo inalenga zaidi kuleta fursa za kiuchumi (Unlocking the economy) Kwa kawaida kabisa katika usimamizi wa uchumi kila kauli,maamuzi na matukio yanayotokea katika mfumo wa kisiasa, kijamii na kiuchumi huwa yanaathiri hali ya uchumi katika njia ya faida(gain) au hasara (loss)Kwa hivyo basi tunapoutazama uchumi wa Tanzania ni lazima tuungalie katika namna mbili. Namna ya kwanza ni Macro economic Indicators na Pili ni Micro economic indicators.
Mimi binafsi nikiangalia katika hivyo vyote naona kwamba hali ya uchumi ni nzuri na kama taifa tunaelekea sehemu nzuri.Kufungwa kwa biashara, watu kupoteza au kukosa ajira na biashara kuwa ngumu ni kawaida katika uchumi wa soko ambapo kuna ushindani mkali. Kama biashara imashindwa ushindani basi huwezi kusema ni matatizo ya serikali hapana ila iwapo maamuzi ya serikali ama kisheria au kisera ndo yamefanya biashara hio kuanguka basi unaweza kulaumu serikali na ni lazima kuwa makini katika kutoa lawama hizo kwani kuna uwezkano kabisa kutoa lawana hizo kukawa na madhara zaidi ya kiuchumi.
Pamoja na ukweli huu hapo juu serikali haiwezi kujitoa lawamani kwa yanayotokea katika uchumi kaika kipindi hiki.Tanzania sasa limekuwa taifa la Wamachinga na Wachuuzi. Uchumi wetu umekuwa ni wa madalali, wachuuzi na wauza sura. Hakuna mfumo wa kiuchumi na kisera unaoongoza uelekeo wa taifa. Hii ni hatari.Serikali inapswa kutambua kwamba inapoendelea kuruhusu uchumi wetu kuelekea unakoelekea kuna siku SERIKALI ITAKOSA KODI HALALI YA KUKUSANYA na itaanza kukusanya kodi HARAMU au kodi ya DHULUMA. Kuna siku itafika serikali itshindwa kujiendesha kwa sababu ya ujinga na uzembe wa watendaji katika kushughulikia maswala ya kisera mapema.
Nasema hivi kama mtu ambaye nimeona kabisa hali ilivyo na nikagundua kwamb hali ikiacha kama ilivyo kama taifa tuna hatari kubwa mbele yetu. Swali la kujiuliza ni Je, nini kifanyike?
Kwanza kabisa ni lazimi serikali irekebisha mfumo wa ukusanyaji kodi na maduhuli ili iwe rahisi kulipa.Kisha iondoa ukiritimba katikka kuanzisha na kusimamia biashara.Sioni sababu ya Zoezi la kuanzisha biashara kuwa GUMU. Ukitaka kuanzisha biashara Tanzania unajikuta unatumia muda mwingi na gharama nyingi katika maswala ambayo hayaongezi thamani yoyote katika biashara yako.
Eneo lingine amblo linalohitaji kutazamwa ni eneo la uwekezaji hasa katika miradi ya miundo mbinu.Nasema hivi kwa sababu naona kabisa kama taifa tumewekeza biala mpangoa katika miradi ya miundo mbinu. Ujenzi wa MJi mkuu mpya. Ujenzi wa Miundo mbinu kule Dar es Salaam na katika miko mingine. Swali la kujiuliza je Rasilimali Pesa tulizonazo zinatiosha kuwezesha ujenzi wa miundo mbinu yote hii katika kipindi kifupi? Kama hapana basi ni bora tukaenda hatua kwa hatu huku tukitafuta namba ya kuingiza PESA kwa kuwekeza katika watu wetu na uzalishaji ili tuweze kujenga uchumi shirikishi.
Najua kuna mengi ambayo yanaweza kufanywa na serikali, watu binafsi na wananchi kwa ujumla. Tujadili hapa kwa pamoja kila kinachoendelea katika uchumi wa nchi yetu katika misingi ya uZalendo na Maendelea.
Karibuni.