Nini kinaendelea kati ya Makonda na Steve Nyerere

Tuwaseme

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
645
1,188
Kwa nn Steve Nyerere hakwenda kwenye Maandamano ya Wasanii wa Bongo Movie? Kwenye page ya Mange nimemuona Steve mapovu yanamtoka anapinga utaratibu huo uliotumiwa na Makonda na Wasanii wenzake wa kuwazuia machinga kuuza movie za nje.

Sasa nikajiuliza, Steve alivyokuwa na Uswahiba na Makonda kweli wa kushindwa kwenda kwenye maandamano? Steve anavyopendaga kujipendekeza kwa viongozi leo ameshindwa kwenda kweli?

Nikahisi wenda lile sakata lake na Mama Wema kuvujisha Yale mazungumzo yao ndo imewafikisha hapa, sidhani kama msimamo wa sasa wa Steve unatoka moyoni.. Nadhani ni vile tu hana mawasiliano mazuri na Makonda ndo mana ameshindwa kwenda.
 
Huyo anataka kubebwa, hajui kwamba Mh. Makonda yeye ni Kiongozi. Hapa kazi tu kwanza na anaweza kucheka na mtu story mbili tatu ila sio wa mchezo mchezo.

Moja ni alimuongelea uongo kwa yule Mama ili kutafuta misifa, na akajulikana ni nyoka mkubwa. Asingeweza kwenda kwa sababu ni muongo mkubwaaaaaaa.
 
Ila hili swala la kukataza machinga kuuza movie za nje ili kukuza Movie za bongo halijakaa vizuri ki vile..........
 
Ameshamshtukia jamaa kilaza na kweli amefoji vyeti, bashite aonyeshe vyeti, na asilete maigizo yake, hizo movi za nje watu wanaweza kuzidownload kwenye Mtandao.
Hao bongo movie nao wasimsikilize kilaza bashite anawaharibia, wafanye kazi nzuri waone kama hazitanunuliwa
 
Pamoja na kwamba yawezekana wana matatizo yao ila Steve kaongea mambo ya kiuhalisia kabisa,kuna wakati tumkubali mtu pale anapoonyesha hekima kwa kiwango fulani.
 
Matukio mengine yametengenezwa ili ku-keep watu busy wasahau yaliyopo hewani. Steve ameliona hili maana hakuona sababu. Hizi filamu za nje zimeanza leo? Hata zisipouzwa kariakoo haziwezi kutazamwa? Prison break hii ya sasa inauzwa kariakoo? Haihitaji kusoma sana ili kujua hili.
 
bashite kahangaika sana kurudisha urafiki na steve, steve kagoma na hata simu zake hapokei...simply steve ni timu membe, jk na wanawe akiwapo bwana nape nnauye, hivyo hawezi kuwasaliti na hatakufa njaa asipojipendekeza kwa bashite
 
Steve anaangalia maslahi kwanza, mjini pa gumu. Baada ya sakata la mama Wema mbona alikwenda Kolomije na Le Mutuz kuhonga wanakijiji wakatae kuwa mnaemjua nyinyi kama Paul siyo Daudi.
hawakwenda kolomije, waliishia mwanza mjini na siyo kwa ishu za bashite
 
wote wendawazimu mmoja kajibadili jina la ukoo kutoka Steven Mangele kwenda Steven Nyerere mwingine kajiita Paul Makonda badala ya Daudi Bashite.
 
Kwa nn Steve Nyerere hakwenda kwenye Maandamano ya Wasanii wa Bongo Movie? Kwenye page ya Mange nimemuona Steve mapovu yanamtoka anapinga utaratibu huo uliotumiwa na Makonda na Wasanii wenzake wa kuwazuia machinga kuuza movie za nje.

Sasa nikajiuliza, Steve alivyokuwa na Uswahiba na Makonda kweli wa kushindwa kwenda kwenye maandamano? Steve anavyopendaga kujipendekeza kwa viongozi leo ameshindwa kwenda kweli?

Nikahisi wenda lile sakata lake na Mama Wema kuvujisha Yale mazungumzo yao ndo imewafikisha hapa, sidhani kama msimamo wa sasa wa Steve unatoka moyoni.. Nadhani ni vile tu hana mawasiliano mazuri na Makonda ndo mana ameshindwa kwenda.
Ni sawa umechoma tire kwenye shimo yumo nyoka kinachofuata nyoka waatoka kama mshale, ndio kinatokea sasa wanaanza kutambua huyu bashite akili zake zimekaa kama mbuni
 
Kalee sikajamaa ka yulee jamaa wa mtama sasa bosi wake katemeshwa sababu ya fafafafaaa unategemea atamsapoti kweli?
 
Back
Top Bottom