Unajua jamaa yangu huwa kuna mahala napata taabu sana kujadili maada kama hizi.
Unaweza kuwakwepa IMF na World bank kama toka uhuru unakopa kwao na bado wanakudai na bado unahitaji misaada yao na misaada ya wanachama wao, ukipata maafa kama mafuriko, njaa, milipuko ya magonjwa nk unahitaji misaada toka kwao. Madeni yakikuzidi unaenda kuomba wakusamehe madeni, miradi kibao ya kijamii unahitaji waje wakusaidie, bajeti yako zaidi ya 40% inatoka kwao... Hao IMF na World bank ukumbuke ni moja ya organs za UN na watoa michango mikubwa huko na hela zao ndio tunawaita wadau wetu waendeleo..
Njia pekee ya kuwakwepa IMF na World bank ni kujitegemea kwa kila kitu na kutoomba msaada kwao na kwa wanachama wao au wanaombatana nao. Tukipata Maafa yoyote tujiokoe na kujisaidia wenyewe na resources zetu, madawa either tununue kwa hela zetu au tutengeneze wenyewe.. IMF na World bank sidhani kama watakufuata fuata kama wewe unajitegemea na huwafuati fuati..