Nini Kinachoendelea IMF na World Bank?

Hii article ya wakati wa Clinton ndiyo unatuletea hapa leo?!😵
 
Toeni kwanza Ripoti za uchumi mwruhusu watamu wenu wachapishe takwimu sahihi tuzione.
 
Anaehujumu uchumi siyo IMF bali anaekataa kutoa takwimu za uchumi ili kila mtu ajue kinachoendelea!!Usifikiri sisi ni mazuzu kama wewe!!
 
Ni wivu tu
 
Serikali bana eti pesa zako zinanuka na huku unazipenda
 
World banck na imf ni walewale. Sasa ili kuweka urari wA takwimu tuwe na sheria za uhuru wa takwimu na sio mfumo wa sAsa wa tAkwimu toka chanzo kimoja. Imf wala world banck hAzinA hata mwafrika aliye wahi kua mkuu wA taAsis hizo.

..Raisi wa World Bank ni mteule wa Raisi wa Marekani kwasababu nchi hiyo ndiyo yenye hisa nyingi ktk benki hiyo.

..Mkurugenzi mkuu wa Imf naye hutokea nchi za Ulaya. Bado natafuta sababu zake. Lakini huenda ni kwasababu nchi za ulaya ndiyo waanzilishi wa taasisi hiyo.

..pamoja na hayo kuna nafasi ya Vice President for Africa ktk WB na nafasi hiyo imekuwa ikishikwa na Waafrika siku zote.

..pia kwa sasa hivi kuna vice president anayeshughulikia masuala ya infrastructure anatokea Africa.

..zipo nafasi nyingi ndani ya WB zimeshikwa na Waafrika. Kwa mfano kuna kipindi Chief of Staff wa Raisi wa WB alikuwa Mtanzania. Pia yupo Mtanzania alikuwa muwakilishi wa WB South Korea. Hata Dr.Mpango, na Dr.Benno Ndulu waliwahi kufanya kazi WB.

..Kwa maoni yangu fursa zipo WB tunachopaswa kufanya waTz ni kuzichangamkia.

..Kwa upande wa Imf kuna deputy managing director wa Africa, na kwa kumbukumbu zangu nadhani anatokea Ethiopia.

NB.

..kama haturudhiki na muenendo wa taasisi hizo kwa nchi yetu, tunayo haki ya kusitisha uanachama wetu.
 
WB wamewapa mkopo kwa sababu uchumi wenu ni MBOVU otherwise msingeomba!! Na hiyo ndio sababu imf wametoa taarifa mbaya maana liuchumi lenu ni libaya pia.
 
Kwa hiyo IMF in mabeberu sana kuliko world Bank, washahili husema "ukipenda chongo huita kengeza" eti Leo mnawapenda world bank,

Word bank na IMF in mapacha
 
Bowie,

..Tz ni mwanachama wa Imf na Wb.

..tulijiunga na mashirika hayo wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

..kama Imf haina msaada kwetu, au inatuhujumu, tunayo haki ya kusitisha uanachama wetu ktk taasisi hiyo.
Hatuwezi kujitoa wb na imf hata siku moja ,kama unafahamu vizuri kitu kina choitwa SAP ,ndio ilikuja na hizi condition
 

Inabidi uweke ushahidi wa vielelezo kuhusu hizo hujuma zao. Huwezi kufanya mambo kienyeji enyeji halafu ukataka tukuamini.
 
Huwezi hata siku moja juitenganisha na WB na IMF hawa ni mapacha kama vile samaki na maji, ila pia kulingana na kasi ya jpm kuiletea Tanzania maendeleo sion haja ya kutoa hayo makimu , ss tunachotak ni maendeo bas
Kwa hiyo IMF in mabeberu sana kuliko world Bank, washahili husema "ukipenda chongo huita kengeza" eti Leo mnawapenda world bank,

Word bank na IMF in mapacha
 

Huwezi ukawatenganisha IMF na WB.
Kumbuka masharti waliyotoa WB baada ya yule Vice President wao kuja hapa na kuzungumza kinyume na alivyozungumza mwenye nchi.

Hiyo mikataba iliyosainiwa na Dr Mpango maana yake ni kwamba tuliyakubali masharti waliyoyatoa, na kama hayatatekelezwa hela haitoki. Unaposaini sio kwamba hela unapewa hapo hapo ukatumie.

Kama masharti tuliyopewa, k.m., wasichana kutobaguliwa, sheria ya takwimu kutorekebishwa na mengine ya kupigia kelele ushoga, tukiyakomalia kama vilevile tulivyosikika tukiyatangaza, usitegemee hiyo hela ya WB kuja hapa.

Unapofanya ubabe hakikisha hutikisiki hata hao unaowafanyia ubabe wanapokusonya.
 
Hatuwezi kujitoa wb na imf hata siku moja ,kama unafahamu vizuri kitu kina choitwa SAP ,ndio ilikuja na hizi condition

..siyo kweli.

..sap ilikuja miaka kadhaa baada ya kuwa tumejiunga imf na wb

..kwa msingi huo tunaweza kuondoka huko kama tulivyojiunga, na hakuna wa kutuzuia.

..tatizo letu ni UOGA.

..kama utakumbuka Raisi aliwahi kutoa amri kwamba hakuna kusomesha wasichana waliozaa. Alipokuja Makama wa Raisi wa WB tukasalimu amri na msimamo wetu kuhusu kusomesha waliopata mimba ukabadilika.

..Again, TZ ni nchi HURU hivyo uamuzi wa kuwa mwanachama au kujitoa imf na wb ni wetu.
 
Kama IMF ni vichaa Kama ulivyo waita kwanini umejiunga huko, kichaa na Vichaa wenzake, sasa Kama umejiunga si na wewe kichaa?

Chapisheni taarifa za ukuwaji wa Uchumi ulitoka huko unakowaita Vichaa tuone, kwanini mnaficha ukweli, ndani unaficha, huko nje wanataka ukweli, hapa Tanzania mnaficha ukweli, mnataka kuficha ukweli na huko? Wale wanataka kujua mnatumia vipi wanacho wasaidia, sio wanawapa PESA mnakuja kuhonga wabunge wa upinzani kujiunga na CCM, chapisheni taarifa zao msiwaite vichaaa,

Hao hao Mabeberu mnawasema, haohao mnakwenda kuwaomba mko sawasawa kweli nyie, msiombe Kama hamtaki wajue mnatumiaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…