Nini kimemsibu RENATUS MKINGA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kimemsibu RENATUS MKINGA?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakende, Oct 4, 2012.

 1. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Katika hali isiyo ya kawaida mchambuzi mashuhuri wa siasa bwana RENATUS MKINGA amekuja kwenye kipindi cha marumbano ya hoja kinachoendeshwa na kituo cha TV cha ITV akiwa amevalia nguo ya CCM. Kitendo cha kuvaa nguo hiyo wakati yeye anafahamu kwa undani madhambi yaliyotendwa na chama hicho kama alivyokuwa akiainisha kipindi cha nyuma kimeniogopesha mimi binafsi. Moja kati ya dhambi kubwa ni kuunga mkono jambo fulani wakati ukijua kuwa ni jambo la hatari.

  Eti anasema chama pekee kinachounga mkono muungano ni CCM wakati kwa sasa Wazanzibari wanataka kujitenga wakiwa chini ya utawala wa CCM tangu muungano. Mkinga anafikiri kuunga mkono muungano ni maneno tu, kwanini CCM hawajatatua kero za muungano wakati wao muda wote ndiyo watawala, na wana uwezo wa kufanya hivyo?.

  Mkinga ambaye jamii masikini ilimuheshimu sasa anaanza kupotea, kitendo cha kuvaa nguo ya CCM ni dalili za kufa kiakiri. Shujaa ufa akisema ukweli, mkinga umeanza kupotea na ndiyo maana mwendesha mada bwana DEOGRATIUS RWEYUNGA alikuponda hapohapo kuwa jadili maswala ya kauli ya nyerere kuhusu muungano na siyo jezi ya CCM
   
 2. t

  tenende JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mtu aliyevuta bangi akiwa kijana maamuzi ya bangi unaweza kuyaona akiwa mtu mzima. Leo mmeona madogo, Subiri atakapoingia mtaani kavaa tri-angle!
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,583
  Trophy Points: 280
  Huo ndio ukweli wenyewe!. CCM ndicho chama pekee kitakacho ulinda muungano!. Asili ya CCM ni kama asili ya Muungano, muungano wa TANU na ASP. Wale CCM wanaopinga muungano kule Zanzibar, sio CCM kweli, wale ni CCM kadi na sare tuu ila ndani yao bado ni ASP!. Wale wengine wote ambao ni CUF, wale ni ZPP, ZNP na Hizbu, wao ni wahanga wa mapinduzi, kwa vile muungano ndio umeyalinda mapinduzi daima, hawawezi kupenda aslan!.

  Tuna tatizo kubwa humu jukwaani, mtu akiwa CCM, kila kitu asemacho mnakiona kama sicho!, alichosema Mkinga ndio ukweli wenyewe!. Kwa vile mpaka sasa hatujajua katiba mpya itasemaje kuhusu asilimia ya kura za Zanzibar, ili chama chochote kiweze kushinda urais wa JMT!

  CCM na CUF wana uhakika wa kura za Zanzibar, Chadema haina uhakika wowote wa kura za Zanzibar, katiba mpya itatamka wazi kuwa ili chama chochote kitangazwe mshindi wa urais wa Muungano, lazima kishinde kwa theluthi moja ya kura za pande zote za muungano!

  Wengine wanakalia maandamano huku siku zinakwenda!, wakiambiwa hawajipanga wanakuwa mbogo!, sasa wewe unaambiwa CCM ndicho chama pekee kinachotetea muungano, unashangaa nini?!, mkiambiwa 2015 ni CCM tena!, mapovu yanawatoka!.
  P.
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Yaani mtu akiwa na mawazo mengine ndani ya ccm basi sio mwana ccm wa ukweli inashangaza sana mtu kama wewe mwaka 2012 unahubiri siasa za zidumu fikra za m-kiti.

  Kuhusu katiba ingawa hujui kama ulivyokiri hapo juu kuwa katiba mpya itakuwaje lakini wakati huo huo unaconclude kwa kutumia mawazo ya katiba ya zamani kuwa watu hawajiandaa kwa ajili ya kumeet matakwa ya katiba ya zamani ni ngumu kukuelewa au sijui mtu akishakunywa maji ya bendera labda uchanganyikiwa??

  Unawalaumu hawajajiandaa wakati huo huo unawalaumu kwa kufanya maandamano ambayo ni sehemu ya maandalizi ya kujiandaa sasa sijui anayetokwa na mapovu ni nani anayeongea na pande zake mbili za mdomo au yupi?
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Huenda kisukari kipo juu tusimlaumu bure
   
 6. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Kama kutakuwa na kipengele kama hiki, basi katiba hiyo itakuwa imetengeneza mazingira ushindi kwa CCM
   
 7. aye

  aye JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,989
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  njaa ndo ilikuwa inamsumbua baada ya kupata mamilioni ya voda kaamua kutulia
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,583
  Trophy Points: 280
  Kuna watu wanaamini katiba mpya imekuja tuu kama "manna"!. CCM ndio waliokuwa hawataki kabisa kuisikia katiba mpya!, mara all over a sudden change of heart sasa serikali ya CCM imekubali katiba mpya kwa moyo mkunjufu!

  Ndio maana natumia msemo huu "I fear the Greeks, especially when they bring gifts", kipengele gani kitaingizwa kwenye katiba mpya na kipi hakitaingizwa, watatumia principle of "concensus" ya wengi wape!. Composition ya constituent assembly itasukwa kwa utaalamu wa hali ya juu kuhakikisha katiba hiyo inalinda "status quo" ya waliopo!

  Kura ya maoni ni kuikubali tuu au kuikataa in its totality!, yaani itakuwa na swali moja tuu la "Jee Unaikubali Katiba Mpya?. Jibu ni "YES" or "NO". Yes zikishinda, katiba mpya imepita, no zikishinda, katiba ya zamani inaendelea!.
  P.
   
 9. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  CCM kitaulinda Muungano kama Seif anavyolinda Muafaka. Vyote viwili ni siri za watu fulani kwa manufaa yao binafsi. Hakuna muungano wa serikali mbili ukabakia na serikali mbili, either moja or Tatu. Kama kosa hili la muundo lisipofanyiwa kazi, Muungano hautadumu tena
   
 10. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Hoja ya Pasco ina mashiko..
   
 11. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,136
  Likes Received: 7,384
  Trophy Points: 280
  Hoja ya Pasco haina mashiko
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Pasco,
  Hicho kifungu kuwa lazima ushinde theluthi moja ya kura za Zanzibar kwanza si democratic na mimi nitaungana na ndugu zetu wa Zanzibar kukipinga. Theluthi moja ya kura za Zanzibar ni kura laki tatu wakati ambapo theluthi moja ya kura za mainland ni kura zaidi ya milioni nne.

  Uwiano hapo uko wapi? Halafu majority ya Wazanzibari wanataka muungano wa mkataba. Hujasikia? Huwezi kukinyima chama nafasi ya uongozi ambacho kimeshinda majority votes katika mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Iringa, Arusha, Moshi na Dar-es-salaam, to say the least, simply because hawana kura laki tatu za Wazanzibari. It does not make sense.

  Hapa Marekani Republicans wanajua kwamba hawawezi kushinda California na New York ndio maana wamekazania majimbo mengineyo kama vile Florida, Virginia na Pennsylvania, lakini hawana katiba kuwa lazima ushinde theluthi fulani ya kura za jimbo fulani. Ni ujinga huo.
   
 13. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu Pasco,

  Tatizo la hili chama lako ni kwamba "they are always trying to swim against the tide". Waliambiwa tunataka katiba mpya wakagoma, maji yalivyozidi wakaamua kwenda nayo. Binafsi bado naamini kwa dhati kabisa kwamba CCM hawana nia njema na hii "katiba mpya", swali la kuwauliza wana CCM ni kwamba "wanategemea kucheza na akili za watanzania mpaka lini?"

  Wanajijengea chuki mbaya sana mbele ya wananchi, na kama wanaamini wataendelea kutumia mbinu chafu kutawala hii nchi, wanapaswa kujitazama upya. Siku watayokufa hawataweza kufufuka kamwe. Watoto wakichoka udikteka wa baba, matokeo yake huwa mabaya sana.
   
 14. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Ndio maana hata wakati wa uchaguzi mnabeba dhana ya kuibiwa kura,si kila mwenye kukipinga CCM huwa hana mapenzi na chama chake.CCM ni chama ambacho mwanachama ana uhuru wa kuhoji,kupinga na kukosoa.
   
 15. Mkali Tozz

  Mkali Tozz JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  That is the power of money! It is easy to turn HERO to BLUFF,
   
 16. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Nilishasema na labda kurudia tu mtu awaye yeyote ukisikia anasema ni ccm huyo na ufisadi ni kama masaburi na chupi.mkinga hamjui kuwa ni kibaraka wa membe,na kelele zote zile ni kukosa tu bakhshishi? ameshagombea mara kadhaa akapigwa chini magamba humo,mmmfyoooo
   
 17. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Hata mimi nilimuona na kumsikia, kuhusu mavazi ya CCM,unajua njaa inasumbua sana watu na ukiiendekeza unaweza hata kuinamishwa,hapo uenda anauota U-DC.Hoja aliyoitoa ni dhaifu kwani kwa upande wa Tanzania Zanzibar kauli mbalimbali za kuupinga muungano zimekuwa pia zikitolewa na viongozi waandamizi wa CCM,labda angesema kuwa CCM bara ndio watetezi wa muungano angeeleweka zaidi.
   
 18. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Chezea njaa wewe?
   
 19. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hahahahaaaa yaani kweli tumefikia hatua hii siamini kabisa. Je kama angeingia amevaa gwanda za Chama chako mtoa mada ndiyo siyo dhambi? Nadhani kuna umuhimu wa kujua maana ya dhambi kabla ya kuitaja pia vua boriti kwenye jicho la chama chako kabla ya kuangalia chama kingine. Nimekuwa nikiosoa sana mambo fulanifulani yanayofanywa na baadhi ya wana ccm ambayo ni kinyume na katiba ya chama vilevile Mkinga ana haki ya kufanya hivyo na kuwa mwanachama na ndiyo uzalendo siyo kuwa na ndimi mbili. Na sijawahi kusikia Mkinga akitaja chama chake wala kuikana ccm.
   
 20. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  CCM ni lazima iulinde Muungano kwa nguvu zote kwa sababu kuu moja tu.Nje ya Muungano kuna TANU na ASP.Hivyo ukisema Muungano uvunjike ni sawa na kusema CCM ivunjike ,hapo utabashiri kuwa Automatically CCM itakuwa imeondoka madarakani.Sasa nani atakubali hiyo.Hivyo tunapojadili Muungano yapaswa tujue kuwa tunajadili kitu hiki:

  Muungano( TANU+ ASP) = CCM (TANU +ASP)
   
Loading...