ligendayika
JF-Expert Member
- Aug 31, 2012
- 1,183
- 198
Huu nao ukweli CCM ndo waumini wa muungano hili huitaji kwenda shule kujua. Mkinga kavaa nguo ya CCM akimaanisha lile aliloliamini kuhusu muungano. Mkinga mtu wa misimamo na hapa anasimamia muungano ila ukimwambia richmondi. meremeta, deep green utajua huyo ni nani.Huo ndio ukweli wenyewe!. CCM ndicho chama pekee kitakacho ulinda muungano!. Asili ya CCM ni kama asili ya Muungano, muungano wa TANU na ASP. Wale CCM wanaopinga muungano kule Zanzibar, sio CCM kweli, wale ni CCM kadi na sare tuu ila ndani yao bado ni ASP!. Wale wengine wote ambao ni CUF, wale ni ZPP, ZNP na Hizbu, wao ni wahanga wa mapinduzi, kwa vile muungano ndio umeyalinda mapinduzi daima, hawawezi kupenda aslan!.
Tuna tatizo kubwa humu jukwaani, mtu akiwa CCM, kila kitu asemacho mnakiona kama sicho!, alichosema Mkinga ndio ukweli wenyewe!. Kwa vile mpaka sasa hatujajua katiba mpya itasemaje kuhusu asilimia ya kura za Zanzibar, ili chama chochote kiweze kushinda urais wa JMT!
CCM na CUF wana uhakika wa kura za Zanzibar, Chadema haina uhakika wowote wa kura za Zanzibar, katiba mpya itatamka wazi kuwa ili chama chochote kitangazwe mshindi wa urais wa Muungano, lazima kishinde kwa theluthi moja ya kura za pande zote za muungano!
Wengine wanakalia maandamano huku siku zinakwenda!, wakiambiwa hawajipanga wanakuwa mbogo!, sasa wewe unaambiwa CCM ndicho chama pekee kinachotetea muungano, unashangaa nini?!, mkiambiwa 2015 ni CCM tena!, mapovu yanawatoka!.
P.