Nini kimefanya Reggae ipotee kwenye ramani Tanzania?

blogmaster

Senior Member
Aug 15, 2015
167
74
jhiko-poster-1.jpg


WAWEZA ELEZA SABABU ZAKO KUPITIA KWENYE PAGE YETU, KWA KUBONYEZA HAPA NA COMMENT YAKO ITASOMWA LIVEE
 
Kwa sababu radio stations zinawaaminisha watu kuwa genre zengine za miziki ni bora kuliko reggae. Lau mziki huo ungekuwa unapata airtme ya kutosha, watu wangeukubali pia. Umepotea kwa sabab sio common maskioni mwa watu wengi Tanzania. Kenya na Uganda bado ni mziki unaokubalika na kuheshimika.
 
Tatizo lingine wasanii wa reggae wa kibongo hawakutaka kubadilika, tofauti na wenzetu waganda.Wasanii wa kibongo tangu enzi za kina Kalikawe na Galinoma mpaka leo bado wanacopy riddim za kijamaica.Ubunifu hakuna.
 
Ungefafanua umepotea katika ramani ipi. Kama ulimaanisha reggae kwa ujumla basi hauko sahihi, kwani reggae is still very strong. Kama ulimaanisha reggae ya Tanzania basi naweza kubaliana na wewe kuwa reggae ya Tanzania imerudi nyuma sana, lakini sio kupotea kwenye ramani. Reggae si mziki wa msimu au wa kustarehesha. Kizazi kikubwa cha sasa kinapenda zaidi mziki wa mapito, ambao reggae haipo huko kabisa. Kutokuwa muziki wa mapito kinafanya watu wasifuatilie maendeleo ya muziki huu. Lakimi nadhani wasanii wanaofanya muziki wa reggae bado wanafanya vizuri sana tu. Inawezekana wakawa hawasikiki kwenye radio na televisheni zetu, hapo napo kuna sababu zake. Mfano ni hilo la kutokuwa muziki wa mapito, reggae aio muziki wa kufurahisha na kustarehesha, reggae ina ujumbe mzito zaidi ya hapo. Kizazi tulichonacho kinataka muziki wa kustarehesha usio na muelekeo wala ujumbe wala unaoongelea jamii. Ndio maana utona "wasanii" wa muziki wetu wanatoa wimbo haukai sokoni hata wiki mbili unakuwa umefuja, sababu hauandaliwi inavyopaswa. Kuna sababu nyingi lakini kwa kifupi sana naishia hapa..
 
LUGHA NI TATANISHI.
Na unajua kwamba kikundi cha Morgan Heritage kinapania kuamia Kenya?
Pia kuna fununu kwamba Alaine huenda akafuatia!
 
Watangazaji wengi kwa kipindi kirefu sasa wanaigana aina za vipindi kwenye radio na television. Sio watu wa kusumbua vichwa vyao.
Alafu huu muziki lugha yao; Jamaican Patois ni ngumu kwa watu wengi hapa Tanzania. Promoters, event organisers waoga kufanya show za reggae na kama ni mdau/mpenzi wa kwenda kwenye matamasha ya Reggae utakuwa unafahamu hili jambo.
Pia wengi bado wanaamini reggae ni muzik wa harakati tu bila ya kujua kwamba una maswala ya mapenzi hivyo kuuchukulia sio muziki wa kustarehe.
 
Back
Top Bottom