Nini kilimng’oa Abubakar Kunenge Ukuu wa Mkoa Dar es Salaam?

wajibisha

Member
May 16, 2021
90
215
Nawasalimu Kwa Jina La JMT.

Katika teuzi mpya zilizofanywa na Mheshimiwa Raisi Mama Samia Suluhu Hassan ni kupangua safu za baadhi ya wakuu wa mikoa.

Mabadiliko yaliyonistua ni kuondolewa kwa RC Abubakar Kunenge katika jiji hili la MaRaha. Jiji letu la Dar es Salaam.

Hakuna ubishi RC wa Dar anabeba taswira ya nchi kwa maana ya idadi ya wakazi, uchumi na shughuli nyingi za Maendeleo.

Kwahiyo mabadiliko yaliyofanywa ni kushushwa ngazi (demotion) kwa RC Kunenge. Bahati mbaya hatuna investigative journalists nchini ambao wakichimba kujua sababu ya demotion.

Sasa nini kilisababisha ghafla bin vuu RC Kunenge atolewe Dar mara moja na nafasi yake kuchukuliwa na RC Amosi Makala.

Je kuna mahusiano yoyote kuondolewa kwa RC Kunenge na ukaribu wake wa hivi karibuni na mfanyabiashara mmoja maarufu hapa nchini ambaye makampuni yake yamekua yakituhumiwa kwa kashfa za rushwa na kukwepa kodi kwa miaka mingi.


Kuna uwezekano wazee wa kijitonyama walinusa hatari na kumpa taarifa Mama?

Mama hataki kashfa kwenye utawala wake.
 
Kwa mtazamo wangu ni kubadilishiwa majukumu tu kwani katika mtu ambaye pengine wakazi wengi wa Dar hawajapata kumfahamu, kwa kutokana na pilikapilika za kiuongozi na huyu. Hivyo naamini kupata fursa ya kubadilishiwa majukumu, ni ishara kuwa ni mwenyesifa stahiki.
 
Sema na yeye alipooza kama mkojo wa paka hapo kazi alikuwa anafanya....wapi aliyejiona rais wa Dar eti nikiwaona hao wabunge wanazurura ntawafukuza kwenye mji wangu mji wako my futi to hell na tambo zake...tujifunze kuna kesho kupitia Daudi.
 
Kunenge ni RAS sio mwanasiasa wa majukwaani bla nla bla yete back officena utawala ndani mkoa .....anferudishwa RAS kumpa RC unamporeza kwenye career pathyake

Yes huku kwenye siasa kama hayuko Sana ninge pata nafasi ya kushauri kwa Kazi aliyo ifanya Dar kama RC ambaye alikuwa RAS wange mpa unaibu katibu mkuu wa Wizara.
 
Ila jamaa alizidisha kunyenyekea mbele ya mama mstarini wakimlaki na kumpokea. Anakunja mikono na kuinamisha kichwa kupita kiasi ukilinganisha na wengine
Screenshot_20210520_211132.jpg
Screenshot_20210520_211114.jpg
Screenshot_20210520_211054.jpg
 
Kwa mtazamo wangu ni kubadilishiwa majukumu tu kwani katika mtu ambaye pengine wakazi wengi wa Dar hawajapata kumfahamu, kwa kutokana na pilikapilika za kiuongozi na huyu. Hivyo naamini kupata fursa ya kubadilishiwa majukumu, ni ishara kuwa ni mwenyesifa stahiki.
Kumbuka marehemu JPM alipokuwa anazindua stendi mpya ya mabasi yaendayo mikoa,aliweza kumsema Kunenge mbele ya hadhara kwamba amezubaa,mimi naiona power vacuum alioiacha Makonda ikiwa dhahiri.
 
Back
Top Bottom