Nini kilikufanya ukimbie au upende masomo ya sayansi?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Katika maisha ya elimu, kuna maajabu mengi. Yaani katika mazingira sawa. mepesi au magumu lakini utakuta zaidi ya 70% ya wnafunzi wanakimbilia masomo ya Sanaa na biashara na kuachana na sayansi.

chanzo huwa ni propaganda za ugumu wa sayansi au tunapenda vitu visivyoshughulisha sana.
Kuna masomo yameshapitishwa kuwa ni magumu kama Physics na Hesabu. Kuna kijiji kimoja nilipita mwalimu mwenye heshima kuliko wote kijijini ni mwalimu wa Hesabu. tena siku alipoiwezesha shule ya kata kupata A moja ya Hesabu form four. popte anapopita wanamsalimia kwa heshima na wengine wakionyeshana kwa ishara.


Tatizo hili lilianza lini, Nini Chanzo wakuu. Je ni tatizo la taifa au Dunia?
 
Nliacha kusoma science baada ya mwl wangu Wa chemistry kua tooo harsh...alikua mkali na alipenda wale walokua wana catch up easily..she used to say "im moving with the people who are moving".. Ila sijutiii kuachana na science.
 
Nliacha kusoma science baada ya mwl wangu Wa chemistry kua tooo harsh...alikua mkali na alipenda wale walokua wana catch up easily..she used to say "im moving with the people who are moving".. Ila sijutiii kuachana na science.
waalimu wengi sana wanasababisha tatizo hilo. Kuna mwalimu mmoja form one physics aliingia anatamba na kudharau kama watu wataiweza.
Kuna mwingine wa chemistry yeye kuandika maandishi ubaoni huku amekunja ndita alafu anaandika mcharango usiosomeka yeye anaona hiyo ndio sayansi. Watu wakakimbia na kubaki wavumilivu wachache
 
mob psychology
Masomo ya sayansi ni magumu. Kuliko mchepuo wowote.
Ingawa kuna watu au kikundi cha watu huwa hawataki kukubaliana na huo ukweli.

Hilo suala la Mob Psychology huongelewa ili kutomeza hali ya kukatisha tamaa wanafunzi, ili wasiogope kuthubutu, ingawa wao wenyewe ndio wanaoisoma namba na wao ndio wanaokiri kwa vinywa vyao wenyewe kisha wanaachana nayo na kutafuta kwenye uhafadhali.

Na ukweli mwingine ni kwamba, wanafunzi wengi waliokuwa bright uliosoma nao, ndio waliendelea na mchepuo wa science, wenye uelewa wa kati waliachana nayo (ingawa darasani miaka ya nyuma kila mtu alipenda kuwa doctor,engineer, sijui pilot n.k).

SISEMI KUWA NADHARAU MICHEPUO MINGINE HAPANA, KILA MCHEPUO NA UGUMU WAKE ILA LAZIMA TUKUBALIANE UGUMU HUO HAULINGANI.
KINA MAMBO MENGINE NI MAGUMU ZAIDI.
DUNIA NZIMA INATAMBULIKA HIVYO.
 
nilipogundua kuwa eti kuna mtu aligundua oksjeni nikaacha kusoma sayansi
nikaona tunadanganywa mengi ila hili hapana
yaani hadi mwaka wakataja
Wanacho gundua wanascience although Oxygen ipo wanataka waiandae maabara na ikiwezekana wanakua wameigundua......... nikama unavyoona sayari ya Mars although ipo ila wanascience ndo wanaichunguza kuona kama inafaa kwa binadamu so wakicomfirm wanakua wamegundu na ndo maana wanasema wameigundua since inaweza andaliwa maabara ya kemia kwa kutumia raw materials nyingine

Na oxygen inasaidia sana hasa kwa wagonjwa mahospitalin wanaohitaji oxygen inaandaliwa maabara inatunzwa kwasababu ukitegemea oxygen kwenye hewa ni just 21% na nitrogen 78% so kwa mgonjwa anaweza kufa so thats why walibinu mbinu ya kugundua oxygen so that kusave watu
 
Nadhani changamoto kubwa ni style ya ufundishaji,kwamba sayansi ni observation kwamba iwe practically taught other than theoretically,then ukiangalia katika shule zetu au kwa mfumo wetu tunafundishwa theories tu.
Kingine,ni uhaba wa walimu pia tatizo jingine ni aina ya walimu waliopo the way wanafundisha hawavutii wanafunzi kuendlea kusoma hayo masomo,yani hawawaencourage zaidi wanawatia hofu na wogu wanafunzi wanaosoma au kupenda hayo masomo.
My best science subject is chemistry.
 
Mimi nilipenda na kufaulu zaidi sayansi (PHY - "A", CHEM - "A", MATH - "A", BIO - "B") kuliko sanaa ila ngoma ipo adv level ni mwendo wa tripple "D". Inachangiw na kukosekana kwa walimu mashuleni na wanafunzi weng kuw masikini hawanunui vitini, vitabu (eg. Thom duncan, roger muncaster, nelcon etc) na kusoma tuition
 
Back
Top Bottom