Janvansina
Member
- Nov 5, 2025
- 50
- 60
Onyo: simulizi hii ni kazi ya ubunifu (fiction). Wahusika, matukio, majina ya kampuni (isipokuwa yale yanayojulikana sana, mfano 'Dar es Salaam)na taasisi za kisiasa zilizotajwa hapa ni za kutungwa. Kufanana kwa aina yoyote na watu halisi, wakiwa hai au wamefariki, au matukio halisi ni bahati mbaya tu na haina uhusiano wowote na nia ya mtunzi.
****************
Karibu katika ulimwengu wa fitina, usaliti, na siri hatari zinazoweza kuitikisa nchi. Kitabu hiki kimeandikwa kwa heshima kubwa kwa wasomaji wa hadithi za kusisimua. Jitayarishe kushudia Mambo mengi, mazito na ya yenye kushangaza, kwani safari hii ya Eliza ni imejaa hatari.
SEHEMU YA 1
Giza lilikuwa limeanza kutanda jijini Dar es Salaam. Taa za barabarani zilikuwa zikimulika kwa uvivu, baadhi zikiwaka na kuzima.
Eliza alikuwa anatembea haraka kuelekea nyumbani kwake, Mbezi. Alikuwa amechelewa kutoka kazini, na daladala alilopanda lilimwacha mbali kidogo na nyumbani kwake. Alipenda kutembea njia hii fupi ya mkato kupitia vichochoro tulivu.
Lakini leo, utulivu ulikuwa tofauti. Ulikuwa wa kipekee.
Alisikia tu sauti ya viatu vyake vya ofisini vikigonga lami: Tak... tak... tak...
Ghafla, akasikia sauti nyingine.
Tak... tak... tak...
Ilikuwa sauti ya hatua. Mtu mwingine alikuwa akitembea nyuma yake.
Eliza alisimama ghafla ili kujifanya anatafuta kitu kwenye mkoba wake.
Hatua nazo zilisimama.
Moyo wake ulianza kudunda kwa nguvu. Alijipa ujasiri na kuanza kutembea tena, safari hii kwa kasi zaidi.
Tak-tak-tak... (zake).
Tak-tak-tak... (zake yule).
Yule mtu naye aliongeza mwendo. Alikuwa akijaribu kumuwahi?
Eliza hakuthubutu kugeuka. Aliona geti la nyumba yake mbele. Alikimbia hatua chache za mwisho, akaingiza ufunguo kwa kutetemeka, na kufungua geti kwa kasi. Aliingia ndani haraka na kufunga geti kwa nguvu, akifunga na komeo la ndani.
Akapumua kwa nguvu, akiwa amejiegemeza kwenye geti. Alikuwa salama.
Alichungulia kwenye tundu dogo la geti. Hakukuwa na mtu. Barabara ilikuwa tupu.
"Ni mawazo yangu tu..." Alijisemea.
Aligeuka kuelekea mlangoni kwake. Alipofika mlangoni, akagundua kitu.
Karatasi ndogo nyeupe ilikuwa imewekwa chini, mbele ya mlango wake.
Aliiinama na kuichukua. Ilikuwa imekunjwa. Aliifungua.
Ilikuwa na maneno matatu tu, yaliyoandikwa kwa wino mwekundu mzito.
"MIMI NYUMA YAKO."
Je, nini KILICHO nyuma ya Eliza
Je Eliza ni nani
Usikose sehemu ya 2
simulizi hii kwa wiki angalau tutaburudika na vipande viwili. Fuatana nami. Karibu