Nini kifanyike kuzuia Mabinti wadogo kudanga.

Nini kifanyike kuzuia Mabinti wadogo kudanga.

Habari za wakati huu, ndugu zangu, wakubwa kwa wadogo nyote njooni hapa kutoa maoni yenu.

Kwa masikitiko makubwa kuna wimbi kubwa sana msimu huu wa shule zilipofungwa la mabinti wadogo kudanga na kuzurura sana mitaani. Wao ni mtaa kwa mtaa huku wakiwa na kila mwanaume bila kujali kwao ni mkubwa au mdogo au muhuni tu.

Nimejaribu kuwa hoji baadhi ya mabinti wengi, wao wanasema wanatafuta mabwana, inatisha sana mabinti wadogo sana wanazurura hovyo huku na huko, wanadanga na kila mwanaume ni huzuni kuu kwa kweli.

Nini kifanyike kuokoa hiki kizazi ndugu zangu, maana hawa mabinti wa sasa ndiyo wa mama wa kesho, shangazi na hata bibi za wajukuu zetu?


Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Tujiulize kwanza ... Kwanini wafanye hivyo?

1. Maisha magumu?
2. Tabia zao tu ni chafu ?
3. Kupupia ukwasi?
 
Walisema bodaboda ni ajira kwa vijana, cha ajabu vijana wa jinsia ya kike hawapo huko. Mabinti ni muhimu wakajifunza stadi za maisha zinazoendana na miiili yao, zaidi mitandao siku hizi imekuwa mabinti watafaute maarifa mitandaoni kuna fursa nyingi bado kuliko kutumia miili yao kama kitega uchumi..
 
Back
Top Bottom