Nini kifanyike kuwawezesha Wanasayansi wazawa?

game over

JF-Expert Member
Jan 1, 2016
10,593
24,272
Habari Za Wakati.
Kumekuwa na mijadala ya Namna tofauti kuhusu hatima ya Taifa letu,
Katika mada hii tugusie suala hili la wasomi wetu hususani Wanasayansi wazawa,

Ni dhahiri kuwa hakuna nchi inayoendelea duniani bila kujijenga kwenye sayansi na teknolojia, narudia tena, Hakuna!
Na pamoja na kuwepo kwa uwiano mdogo sana wa wanasayansi kwenye jamii yetu lakini tumekuwa hatuoni matunda ya taaluma zao hawa wachache katika kuendeleleza sayansi hususani kwenye suala la uvumbuzi,

Kwa wakati huu ambapo serikali ya awamu ya tano imejikita kwenye mageuzi ya Viwanda na Miundombinu, ambapo utekelezwaji wa adhma hii utaipa China na nchi nyingine manufaa makubwa kwa uwekezaji wa teknolojia yao nchini.,

Je, ni mambo gani hasa serikali inatakiwa kuyafanya?
Vyuo vikuu na taasisi za sayansi zifanye nini?
Na wasomi wenyewe wanatakiwa wafanye nini?

Karibuni....!!
 
Kuwe na school science day ambayo wanafunzi waliogundua kitu wakutanishwe mkoa mmoja, na mshindi apewe zawadi. Kuanzia mashuleni watoto wawe motivated. Mashirika makubwa yasaidie kudhamini science day kama ilivyo Bongo Star Search.

Mkuu umesema vizuri ila hiyo sidhani kama ni "applicable" kwa mtu mweusi attitude zetu za ajabu kuliko kawaida

Nahisi hata kuwe na hizo school science day kila week kama sisi wenyewe hatutasukumana kuaminiana sisi kwa sisi na kuacha utumwa wa kuamini mataifa ya magharibi bhasi....nahisi tubadilishe mitizamo kwanza na hapa tuna safari ndefu zaidi
 
Kitu kimoja kifanyike, kama science day ni mapema sana basi wanaopata alama za juu katika masomo ya science watunzwe vizuri, ikiwezekana serikali na wizara ya elimu ianze mpango wa miaka mitano wa kupeleka wanafunzi wa wawili au watatu wanaofanya vizuri masomo ya science O'level wasome A'level nje ya nchi kuwapa exposure na kutoa changamoto kwa wengine. Shule nzuri zitafutwe either South Africa au Egypt ambako wanamaendeleo mazuri katika science.
 
Proper question should perhaps be; Does the government believe in science. Put it differently, do our politicians and decision-makers believe in evidence-based decisions? If the answer is negative then presence of scientists adds nothing to human development!
 
Proper question should perhaps be; Does the government believe in science. Put it differently, do our politicians and decision-makers believe in evidence-based decisions? If the answer is negative then scientists community may be irrelevant.
Word.
 
Habari Za Wakati.
Kumekuwa na mijadala ya Namna tofauti kuhusu hatima ya Taifa letu,
Katika mada hii tugusie suala hili la wasomi wetu hususani Wanasayansi wazawa,

Ni dhahiri kuwa hakuna nchi inayoendelea duniani bila kujijenga kwenye sayansi na teknolojia, narudia tena, Hakuna!
Na pamoja na kuwepo kwa uwiano mdogo sana wa wanasayansi kwenye jamii yetu lakini tumekuwa hatuoni matunda ya taaluma zao hawa wachache katika kuendeleleza sayansi hususani kwenye suala la uvumbuzi,

Kwa wakati huu ambapo serikali ya awamu ya tano imejikita kwenye mageuzi ya Viwanda na Miundombinu, ambapo utekelezwaji wa adhma hii utaipa China na nchi nyingine manufaa makubwa kwa uwekezaji wa teknolojia yao nchini.,

Je, ni mambo gani hasa serikali inatakiwa kuyafanya?
Vyuo vikuu na taasisi za sayansi zifanye nini?
Na wasomi wenyewe wanatakiwa wafanye nini?

Karibuni....!!

Ukitaka kujadili jambo liwe na manufaa ondoa siasa ndani yake. Ili niweze kwenda sawa na wewe nitaanza na kuomba viashiria vya KUJIKITA KWA SERIKALI KWENYE MAGEUZI YA VIWANDA na hapo tutajikuta tunatoka nje ya mada.

Zipo shida nyingi vyuo vikuu vyetu na taasisi ya kuendeleza teknolojia kuanzia sera hadi uongozi lakini tutajadili vipi na wewe umetumbukiza siasa humo?
 
Kuwe na school science day ambayo wanafunzi waliogundua kitu wakutanishwe mkoa mmoja, na mshindi apewe zawadi. Kuanzia mashuleni watoto wawe motivated. Mashirika makubwa yasaidie kudhamini science day kama ilivyo Bongo Star Search.
Pia wanafunzi vipaji waendelezwe.Serikali ihakikishe mishahara inakidhi japo wastani wa mshahara wa mwanasayansi huyo katika nchi za kiafirika.Hii itasaidia kuziba pengo sehemu tusizojitosheleza bila kuwepo kinyongo kutoka kwa wanasayansi wazawa. Pili udahili ufuate sera ya "Hapa Pasi Tuu"
Tatu Board za discipline na upandishaji vyeo zisiingiliwe na wanasiasa.iwe" Hapa ni policy tuu".Viongozi wa board wawe wenye Taaluma,wazoefu na ikiwezekana wachaguliwe na wanataaluma wenzao kwa kura.
Nne tuangalie pia jinsi ya kumotivate taaluma zisizo za kisayansi ili tusije tukajenga huku tukabomoa kule.Nadhani African countries market value for the trade being considered ingefaa kuwa moja ya factors za kuangalia.
 
I can't agree more with you, vijana hawaoni faida ya kusoma science kama haitaleta tija kwenye maisha yao. Kwasababu ya fursa kwenye IT industry vijana wanajikita huko sana.
 
Kuwe na school science day ambayo wanafunzi waliogundua kitu wakutanishwe mkoa mmoja, na mshindi apewe zawadi. Kuanzia mashuleni watoto wawe motivated. Mashirika makubwa yasaidie kudhamini science day kama ilivyo Bongo Star Search.
Nadhani wahusika wanapita humu,
kuna ile taasisi ya sayansi pale makumbusho sijajua kazi zao hasa ni nini but naamini they can plan and do something.
 
Ukitaka kujadili jambo liwe na manufaa ondoa siasa ndani yake. Ili niweze kwenda sawa na wewe nitaanza na kuomba viashiria vya KUJIKITA KWA SERIKALI KWENYE MAGEUZI YA VIWANDA na hapo tutajikuta tunatoka nje ya mada.

Zipo shida nyingi vyuo vikuu vyetu na taasisi ya kuendeleza teknolojia kuanzia sera hadi uongozi lakini tutajadili vipi na wewe umetumbukiza siasa humo?
Nadhani nimekuelewa mkuu,
Bila shaka hatutafika huko.
Maana yangu ilikuwa ni kugusia uhusika wa Wanasayansi wetu katika utelelezwaji wa miradi ya maendeleo yetu.
 
Proper question should perhaps be; Does the government believe in science
Not really.

Put it differently, do our politicians and decision-makers believe in evidence-based decisions?

Quite the opposite. Juzi juzi hapa kulikuwa na sakata la Tabibu Mwaka. Ule ndio mfano halisi wa muingiliano wa siasa na taaluma. Ingekuwa mimi ndio naamua nini kifanyike, kwangu mimi Bw. Juma Mwaka angetafsirika kama 'scientific resource' mpaka ambapo ningethibitisha kuwa dawa zake hazitibu.

Na kama ingethibitika kuwa dawa zake zinatibu, saa hizi Bw. Juma Mwaka angekuwa Chuo Kikuu kitengo cha Utafiti na Tiba akizungukwa na maprofesa wa fani hiyo ili kuona kama sayansi na mavumbuzi yake vinaweza kuboreshwa. Huu ndio msingi wa sayansi na mavumbuzi kwenye dunia iliyoendelea. Lakini kilichotokea wote tuliona na kusikia, ila mimi sijafahamu mpaka leo kilifanyika kwa faida ya nani. Politics zinawafanya watu wahoji vyeti na madarasa badala ya ukweli uletao manufaa.

If the answer is negative then presence of scientists adds nothing to human development!
Hii ni kwa kesi yetu kama Taifa. Hakuna elimu inayotuongoza kuelekea kujitegemea au kuwa na cha kwetu. Wakati kwa wenzetu sayansi ndio msingi wa maendeleo, sisi tunafikiria kuisoma vitabuni kwa mtindo wa kukariri kama tunajifunza historia.

Nikiangalia kwa jicho la pembeni, nataraji VETA iwe na impact kubwa kuliko our political universities.
 
Kwanza nadhani serikali au chombo chochote kinachohusika kudhamini tafiti na miradi mbali mbali ya kisomi kiongeze bajeti zake katika tafiti hizo. Na pia wanataaluma husika wabanwe na sheria kuhusu matumizi sahihi ya fedha za miradi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha tafiti zao zinawezekana kutumika kiuhalisia na zisiwe kinadharia zaidi.
 
Pia kuwe na special allowance kwa walimu wa science, na mtoto atakaefaulu vizuri mwalimu wake awe recognized pia. Tunahitaji pia kuwa na maktaba (library) zenye vitabu kila wilaya na watoto wawe encouraged kupenda kujisomea. Huko tunakokwenda maktaba za wilaya zinaweza kutoa masomo ya bure basic IT knowledge.
 
Proper question should perhaps be; Does the government believe in science. Put it differently, do our politicians and decision-makers believe in evidence-based decisions? If the answer is negative then presence of scientists adds nothing to human development!
Kweli kabisa
 
Nadhani nimekuelewa mkuu,
Bila shaka hatutafika huko.
Maana yangu ilikuwa ni kugusia uhusika wa Wanasayansi wetu katika utelelezwaji wa miradi ya maendeleo yetu.

Shida ya Tanzania si kukosekana kwa wanasayansi, shida ni wanatambulika kwa ID ipi? Nani ni mwanasayansi hapa kwetu? Kuna mamlaka/idara yeyote inahitaji mwanasayansi?
 
Not really.

Quite the opposite. Juzi juzi hapa kulikuwa na sakata la Tabibu Mwaka. Ule ndio mfano halisi wa muingiliano wa siasa na taaluma. Ingekuwa mimi ndio naamua nini kifanyike, kwangu mimi Bw. Juma Mwaka angetafsirika kama 'scientific resource' mpaka ambapo ningethibitisha kuwa dawa zake hazitibu.

Na kama ingethibitika kuwa dawa zake zinatibu, saa hizi Bw. Juma Mwaka angekuwa Chuo Kikuu kitengo cha Utafiti na Tiba akizungukwa na maprofesa wa fani hiyo ili kuona kama sayansi na mavumbuzi yake vinaweza kuboreshwa. Huu ndio msingi wa sayansi na mavumbuzi kwenye dunia iliyoendelea. Lakini kilichotokea wote tuliona na kusikia, ila mimi sijafahamu mpaka leo kilifanyika kwa faida ya nani. Politics zinawafanya watu wahoji vyeti na madarasa badala ya ukweli uletao manufaa.

Hii ni kwa kesi yetu kama Taifa. Hakuna elimu inayotuongoza kuelekea kujitegemea au kuwa na cha kwetu. Wakati kwa wenzetu sayansi ndio msingi wa maendeleo, sisi tunafikiria kuisoma vitabuni kwa mtindo wa kukariri kama tunajifunza historia.

Nikiangalia kwa jicho la pembeni, nataraji VETA iwe na impact kubwa kuliko our political universities.
Na katika kipindi hiki cha uhaba wa walimu, serikali ingeweza kuleta walimu kutoka nchi kama India kufundisha VETA, masomo ya A'level + ufundi na wakimaliza waende engineering.
 
Kwa wale wenye ujuzk tayari wanahitaji kulatiwa mitaji mikubwa ili waweze kuwekeza ktk utengenezaji wa vitu wanavyovivumbua.
Hapa tunaona wengi wao wanapopata shahada zao hukimbilia kutafuta kazi ktk makampuni ya mitandao ya simu na kampuni zingine.

Wale walioko mitaani ambao wana vipaji ila hawana elimu pana wanapaswa kudhaminiwa na serikali au watu binafsi ili wapate elimh itakayosaidia kuboresha ijuzi wao na kisha wajiunge na hilo kundi la kwanza.

Mfano kuna shirika la TTCL linajikongoja miaka nenda miaka rudi halikuwa kila mwaka tunazalisha mainjinia. Tunashindwa hata na halotel inayomilikiwa na jeshi la Vietinam.
 
Back
Top Bottom