Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,554
Naamini hamjambo waungwana
Mkoa wa kagera unategemea zao la kahawa kibiashara. Inashangaza kuona zao hilo linashuka bei wakati nchi jirani - Uganda bei iko juu. Mkoa una wawakilishi wa wananchi ambao wamekaa kimya wakati wapiga kura wao wananyanyasika kwa kuuza kilo moja ya kahawa kwa Tshs. 1,000/=
Kama ni mwana-Kagera na kama unaguswa na hii hali - tafadhali jitokeze ili tuweze kunusuru uchumi wa mkoa wetu - nashukuru Mkuu wa nchi ameishaliona hilo.
Nini kifanyike kunusuru bei ya zao la kahawa?
Nionavyo mimi: Badala ya kuuza kahawa kama ilivyo .. tuiongezee ubora kwa kuisindika huko huko ili tuuze kahawa inayoenda kutumika.
Kila kata iwe na kinu chake kwa ajili ya kukoboa kahawa ili yale maganda yaendelee kubaki kwenye kata husika na kuboresha ardhi (mbolea)
Nawasilisha!