Nini kifanyike kuing'oa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kifanyike kuing'oa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Inkoskazi, Apr 15, 2010.

 1. I

  Inkoskazi Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ama kwa hakika wakati tulio nao ni rahisi zaidi kuingo'a CCM na serikali yake kuliko wakati wowote mwingine uliopita.Kuna kila sababu na uwezo wa kufanya hivyo kipindi hiki ambacho tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu.
  Binafsi huwa sipendelei kuviita vyama vingine vya siasa (mbali ya CCM) kama ni vya upinzani bali ni vyama vya USHINDANI. Vyama vyote vya siasa vinashindana kupata ridhaa ya wananchi ili viweze kuongoza nchi sio kupingana. Na hili la kuviita vyama vingine kuwa ni vya upinzani, ni moja ya sumu mbaya ambayo CCM huwa inaimwaga kwa wananchi wengi ambao wako vijijini na kujenga taswira kwao kwamba ni vyama vya kihaini, kigomvi, kidini na vinavyoweza kuleta madhara katika nchi - hivyo basi waviogope na wavikatae.
  Kwa hili hiyo basi tuviite vyama vya USHINDANI, tofauti yake na CCM ni kwamba CCM kilishinda uchaguzi (kama hila au laa sote tunajua jibu lake) - period.
  Nini kifanyike:
  Kwa vile CCM imeshindwa ku-deliver na wala haielekei kubadilika, vyama vya USHINDANI vina nafasi kubwa ya kuutumia mwanya huu pamoja na madudu mengine anuai ambayo yametokana na CCM na serikali yake. Ni wakati muafaka vyama hivi vya USHINDANI sio tu kutangaza sera za chama chao, waende mbele zaidi wakati wanajinadi wawaambie wananchi watazilindaje sera zao baada ya kupewa ridhaa ya kuongoza (sio kutawala). Hata wanaotaka kupindua nchi huwa tayari wameshapanga rais pamoja baraza la mawaziri. Kama wanavyokuwa na inayoitwa "Bajeti ya Upinzani" basi wakati wanatangaza sera ni vizuri pia wasema bila kuficha kwamba baraza lao litafanya nini:
  1. Tuanze na katiba ambayo inaonekana ina mapungufu na viraka vingi, waseme kwamba tutasimamia mabadiliko ya katiba ili yaweze kukidhi haja za watanzania kwa kizazi kilichopo na kijacho bila kujali ni kwa manufaa ya chama gani cha siasa.
  2. Tutabana matumizi ya serikali ili mapato yanayowanufaisha wateule wachache yaweze kwenda kwenye maeneo yanayonufaisha wengi - how?
  - tutapunguza baraza la mawaziri
  - tutaondoa vyeo vilivyojazana na kufanya "duplication" of duties. Hakuna sababu kwenye mkoa kuwa na msururu wa viongozi, mkuu wa mkoa, RAS, meya wa mkoa (jiji), mkuu wa wilaya, DAS, mameya wa wilaya,nk wakati huo huo kukiwa na halmashauri za jiji na wilaya na madiwani kibao -WHY? Halmashauri ya miji na wilaya zikiongozwa na madiwani na mameya ambao wamechaguliwa na wananchi wanatosha kabisa kuleta maendeleo katika maeneo yao husika wakishirikiana na wabunge wao waliowachagua.
  - tutapunguza mishahara na marupurupu makubwa (kama alivyosema ndugu Slaa) ya wabunge na mawaziri ili iweze kuendana na hali halisi ya mtanzania ( kwahili nandani wengi hawatagombea ubunge, kwani sasa ni dili inayolipa kuliko zote).Ikibidi tutapunguza viti vya ubunge kwani pia ni vingi bila ya uwiano wa uchumi.
  - Magari yote ya anasa (VX, GS, BMW) tutayapiga mnada na kununua magari yananoendana na uchumi wetu, km Suzuki.
  3. Viporo vyote ambavyo hajafanyiwa kazi sisi tutavinyia - VIPI?
  - Madudu yote ya EPA, Meremeta,Kagoda, Richmond, rada,nyumba za serikali zilizouzwa,nk tutafufua upya bila kuacha jiwe moja kiligeuza na kila aliyehusika atachukuliwa hatua stahiki hata kama alikwisha staafu au kujiuzulu, hii ni pamoja na wale wote ambao kesi zao za kisanii ziko mahakamani.
  4. Kwavile watakuwa wameshapanga baraza lao la mawaziri ni vizuri wakawaambia wananchi kila wizara itafanya nini, km:
  -Wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga taifa( kama watakuwa nayo), wawaambie wananchi kuwa kwa hali halisi ya dunia ilivyo hivi sasa, hatuhitaji jeshi kubwa ambalo ni mzigo kwa taifa. Majirani wetu wote sasa hivi wanajitawala na wala hatuna mpango wa kupigana nao hivyo basi tunahitaji jeshi dogo lenye vifaa vya kisasa na sanasana ni jeshi ambalo litakuwa linatusaidia wakati wa vipindi vya maafa kama kule Kilosa au Same (tender za hovyo hovyo zitapungua kama sio kwisha kabisa).
  - wataalam ambao wako jeshini kama wahandisi, mabwana shamba, madakitari,nk, watashirikishwa kwenye wizara zingine kama miundo mbinu, kilimo, afya,nk ili waweze kuongeza tija kwenye taifa.
  5. Wizara ya madini na nishati:
  - wawaambie wananchi kuwa wataipitia upya mikataba yote kati ya serikali na makampuni yote yanayochimba madini yetu na kwa kushirikiana na wataalam na wadau wote kuhakikisha kwamba tunanufaika nayo na sio tutaachiwa mashimo.
  - wawaambie wananchi wataipitia upya mikataba ya IPTL, SONGAS, DOWANS na mjomba wake Richmond na kuirekebisha ili imsaidie mwananchi na pale ambapo kuna uchafu ulifanywa, mhusika atachukuliwa hatua stahiki.
  - wawaambie wananchi kwamba warudisha mazungumzo ya kufua umeme kutoka Stieglers Gorge ili kukamiliana tatizo sugu la umeme nchini.
  6. Wizara ya elimu:
  - wawaambie wananchi kwavile tumepunguza gharama nyingi serikalini niwazi kwamba sasa tutakuwa na uwezo wa kuwa na shule bora zenye kutoa elimu bora na sio bora elimu. Vitabu, madawati, maabara, walimu wanaolipwa vizuri na kufanya kazi katika mazingira mazuri vitapatikana.
  - wawaambie wananchi ni jinsi gani wataitunza na kuilinda mitihani ili isiibwe na kwa namna gani itawashughulikia wale wote watakaobainika kuiiba au kujipatia vyeti bandia kwa mustakabala wa heshima ya elimu yetu.
  Wana jamvi nimejaribu kuweka angalau wizara chache na dondoo chache lakini nia ni kwamba kila wizara sasa hivi ina madudu, kwahiyo hivi vyama vya USHINDANI viseme kwa kila wizara itafanya nini - hii ndio serikali (pamoja na sera zao).
  Tusaidiane kuainisha nini kifanyike kwa kila wizara kwa nia ya kuing'oa CCM.
  Naomba kuwasilisha.
  Moringe wote ni wamasai lakini sio kila mmasai ni Moringe
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Broda HONGERA,...UKO KWENYE POST YA 4, lakini umekuja na hamasa na jazba sana, na inaonyesha una hasira sana na utawala dhalimu tulio nao sasa...Tunahitaji sana watu wa aina yako ili tufanye nabadiliko ya ukweli!
  Lakini swali kwako...ULISHAJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA?..maana hakuna njia zaidi ya hiyo ambapo unaweza kuondoa hata nukta moja ya kauli ya fisadi, kwa katiba yetu ya sasa!
  Vigezo ulivyoviorodhesha ni hatua moja nzuri sana kuanza navyo, na kama vingepata au kupewa uzito muafaka, basi angalau tungejihakikishia kupata watu mujarabu katika serikali, na mali asili za taifaletu zingekuwa at least secured!!

  Shida inakuja palepale...kuung'oa huu MBUYU!
   
 3. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 668
  Trophy Points: 280
  Mchango mzuri huo. Lakini kuna taabu kubwa mbili. Kwanza, sidhani kama Watanzania wengi wana uwezo wa kuunganisha yote hayo uliyoainisha na mustakabali wao kiasi cha kuiona CCM kama tatizo na, hivyo, kuwa na mdadi wa kutaka kuing'oa madarakani. Na wenye uwezo huo ama ni wachache au wanaangalia maslahi yao ya wakati huu - ambayo yameshikiliwa kikamilifu na CCM. Pili, wananchi wengi kinachowahangaisha ni ridhiki ya leo na, katika hilo, wako katika mashindano ya panya kukanyagana bila kujali na/au kujua kama wote ni dhiki tupu. Mbaya zaidi ukiwazungumzia ufisadi, wengi wanaona ni vita ya wanasiasa kuzidiana kete na kuzibiana ulaji.

  Usishangae basi kuja kugundua kwamba "kete zote zikiwekwa chini" kuna wengi sana wana wanawaheshimu akina RA, BWM, EL, Chenge, n.k. kwa "mafanikio" waliyopata katika mbio hizi za panya. Tena wanaamini hata wao watakujafika huko siku moja (one day). Na kwa hapo, wako wengi pia wanaoamini kwamba harakati za watu kama akina Slaa, Kabwe, Mwakyembe, n.k. ni mkakati mwingine wa kutaka kushinda mbio mbio hizo hizo - janja ya wanasiasa. Nadhani akina RA, EL & co. wanaijua vizuri sana hali hii ndio maana wametulia kabisa wakiamini nafasi yao ya kushika madaraka na kuendelea kuila jamii iliyopumbazika kiasi hicho ni kubwa tu na wanaopiga kelele hawajui kitu. HIVYO, changamoto kubwa zaidi ni jinsi ya kuipindua SAIKOLOJIA iliyopinda ya Taifa hili - Wananchi waweze kuunganisha mambo na kuachana na ujinga wa kukubaliana na uozo uliotamalaki kwenye safu za siasa na uongozi wa nchi.
   
 4. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,494
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Sijui inakuwaje! lakini naamni kama asilimia hata 30 tu ya wanahabari wetu na wamiliki wa vyombo hivyo wangeamua kuacha unafiki na kuamua kuwaeleza wananchi kinagaubaga upuuzi wa CCM, yaani waandike sana sana wawaelimishe wananchi n.k nadhani wananchi wangeamka na tungewamwaga wezi wakubwa hawa (ccm).
  Vinginevyo.......labda tuombee yale ya POLAND yatokee hapa TZ.
   
 5. I

  Inkoskazi Member

  #5
  Apr 15, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kujiandikisha kupiga kura ni swala muhimu ili mtu uweze kutumia haki yako ya kikatiba kuchagua kiongozi unayemtaka. Lakini sio wote ambao wako nyumbani ukiondoa wanaoishi nje ya nchi watakuwa wajiandikisha. Hususan ukichukulia jinsi uandikishaji ulivyoendeshwa na NEC (ref: Dar es salaam) kuna wengi wamekosa hiyo nafasi ya kujiandikisha.
  Kwahali hiyo basi kwa hao wachache tulio/waliojiandikisha ni muhimu sana hivi vyama vya USHINDANI watakapokuja kwenye kampeni zao wasiishie tu kunadi sera zao kwetu na kutueleza kwamba CCM ni mafisadi, waende mbali zaidi kutueleza wataunda serikali ya namna gani. Kama tunavyolalamika kwamba mfumo uliopo ni mbaya basi waje watueleze wao wataufumua vipi ili kuusuka upya au wataufuata jinsi ulivyo?
   
 6. Kiwalani

  Kiwalani Senior Member

  #6
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo lingine kuhusu chaguzi zetu ni kwamba hatuna Tume Huru ya Uchaguzi ... ile ni Tume ya CCM!
   
 7. m

  magee Senior Member

  #7
  Apr 15, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tunachohitaji ni ukombozi wa kifikra,tunahitaji kujua nn tunataka kama taifa,mnaweza king'oa ccm na mkabaki palepale.........tunachohitaji ni mabadiliko katika nyanja zote na mabadiliko hayo yanaletwa kwa kuacha kuitupia mzigo serikali wa wao kufanya kila kitu na kufikiria badala yetu kazi yetu iwe kuhakikisha na kuishinikiza serikali kufanya maamuzi na kutengeneza sera zitakazofanya fikra zetu bora kustawi........
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mimi sioni kama tatizo ni ccm,
  tatizo ni WANA-CCM WA SASA!
  ccm kama chama kina hadhi kubwa dunia nzima

  thread ingeuliza ''NINI KIFANYIKE KUWANG'OA WANA CCM WALIOKOSA MAADILI
   
 9. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Yale yaleeeee!! Dua za kuku.......!! Wakati wana CCM wanafungua matawi ughaibuni na vijijini, sisi tuko bize kufungua threads in JF kana kwamba kila mpiga kura anatusoma hapa JF. We need to live in reality!!
   
 10. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ni kila mmoja wetu ajitambue kama ana ufahamu kichwani mwake na

  ana umri gani? na kama ana umri wa miaka labda 37 je amefaidika

  nini na CCM?
   
 11. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mawazo ni ya kukatisha tamaa, inonekana kweli ukimwi umekula sana mishipa yako

  ya ufahamu wewe... una sensa gani inayokwambia jf ina wapiga kura kiasi gani

  tambua kuwa taarifa yoyote huanza na mmoja kwanza, mbona una mawazo mafu kiasi hicho
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Umeanza vizuri mkuu, bila shaka tutapata mchango wa maana sana kutoka kwako hapa jamvini!
   
 13. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Sawa Mkuu, naona busara imekushinda na sasa unakwenda "personal", but nitarudia kusema kwamba CCM haitang'olewa kwa kutumia internet. CCM wanafungua matawi vijijini wanakoishi wapiga kura wengi wasio na internet wala umeme, sisi JF tunakesha kumaliza finger prints kwenye keyboards za computer tukizani ndio jukwaa la siasa zitakazoing'oa CCM....we lie to ourselves.
   
 14. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Piga kura chagua chama ukipendacho period!
   
Loading...