Nini kifanyike kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi Tanzania

1.Badili katiba ili kuwepo na usalama kisiasa na kichumi,
Tuwe na decentralized gorvenance, selikali za majimbo,

2.Empower sector binafsi,

3.badili mitaala ka kikoloni ya kukariri kama yule mwenye digrii 4 zisizo na faida

4. Punguza kodi ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje.

5.Badili sheria za umiliki wa raslimali aridhi/madini kutoka kuwa 100% selikalini kuwa na miliki za ubia kama 30%/70%
 
Bahati mbaya zaidi awamu ya tano ina fufua kwa kasi sera za kijamaa ambazo zilianza kupotea taratibu.

Kama JPM angeachana na sera za ujamaa, akasimamia mazingira bora ya biashara na kukusanya kodi angefika mbali sana. Lakini ndo hivyo tena. Ni wale waliokulia na kuaminishwa ujamaa.
 
Mawazo mazuri sana ndugu
 
Tunaweza pata mapato maKubwa kuliko ilivyo sasa kwenye madini ikiwa tutabadili sheria ya umiliki, ili madini yamilikiwe na wazawa na selikali kwa uwiano utakaokubalika, alafu wazawa ndo waingie ubia na makampuni ya utafiti na uchimbaji, hii itaiobdoa serikali kwenye mikataba ya rushwa,
Pia nafasi ya umiliki wa wazawa itahakikisha makubaliano leseni za uchimbaji yanakuwa ya kibiashara zaidi,

Wataalamu wa haya mambo ya uwekezaji wa sekta ya madini wanaweza weka sawa mawazo haya
 
Ni kweli kabisa. Magufuli ana nafasi kubwa ya kuifanya hii nchi kuwa na maendeleo makubwa na mageuzi makubwa sana.

Kati ya sehemu ambazo ningeweza kuonana nae ningemshauli aachane nazo ni Sera za kijamaa na kujenga trust kwa wawekezaji wa ndani na wa nje
 
Jiwe atolewe tu Madarakani. Katiba ya Warioba ianze kuwa Implemented, hakika tunaweza aanza hata Kuwaza Kuifikia Kenya na hata Kuipiku kabisa.
Falsafa ya Mwl Nyerere kuhusu maendeleo ni mambo makuu: ARDHI, WATU, SIASA SAFI na UONGOZI BORA.

Katika hayo mambo manne, Rais Magufuli amejitokeza kiongozi bora kwa sababu zifutazo:
1) Ardhi, kama maliasili muhimu kwa uchumi, uthibiti wa matumizi ya hovyo wa ardhi ikiwa ni pamoja na maliasili yake (km madini).
2) Watu: usimamizi na uimarishaji wa hudumu za kijamii (elimu, afya, maji, nk), kupiga uzembe, urasimu, rushwa na maovu mengine ya watumishi wa ummahasa watumishi wa umma wanawajibika ipasavyo.
3) Siasa Safi: Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, 2015 ambayo imerafsiri Sera na Mikakati ya Maendeleo ya Taifa kwa vitendo.

Kwa sababu hizo siamini kama Katiba mpya italeta maendeleo zaidi ya kuwapatia nafasi wanasiasa wenye uchu wa madaraka.

WaTz, HAWADANGANYWI tena na wanasiasa.
 
Bahati mbaya zaidi awamu ya tano ina fufua kwa kasi sera za kijamaa ambazo zilianza kupotea taratibu.

Kama JPM angeachana na sera za ujamaa, akasimamia mazingira bora ya biashara na kukusanya kodi angefika mbali sana. Lakini ndo hivyo tena. Ni wale waliokulia na kuaminishwa ujamaa.
Ushamba na ujinga wakuwachukia waliofaniwa, umetuathiri wabongo
 
Falsafa ya Mwl Nyerere kuhusu maendeleo ni mambo makuu: ARDHI, WATU, SIASA SAFI na UONGOZI BORA.

Katika hayo mambo manne, Rais Magufuli amejitokeza kiongozi bora kwa sababu zifutazo:
1) Ardhi, kama maliasili muhimu kwa uchumi, uthibiti wa matumizi ya hovyo wa ardhi ikiwa ni pamoja na maliasili yake (km madini).
2) Watu: usimamizi na uimarishaji wa hudumu za kijamii (elimu, afya, maji, nk), kupiga uzembe, urasimu, rushwa na maovu mengine ya watumishi wa ummahasa watumishi wa umma wanawajibika ipasavyo.
3) Siasa Safi: Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, 2015 ambayo imerafsiri Sera na Mikakati ya Maendeleo ya Taifa kwa vitendo.

Kwa sababu hizo siamini kama Katiba mpya italeta maendeleo zaidi ya kuwapatia nafasi wanasiasa wenye uchu wa madaraka.

WaTz, HAWADANGANYWI tena na wanasiasa.
Umejitahidi kuandika lakini bado sana, mawazo yako bado ni mwendelzo wa kuabudu watu siyo mawazo huru, not practical
 
Tunaweza pata mapato maKubwa kuliko ilivyo sasa kwenye madini ikiwa tutabadili sheria ya umiliki, ili madini yamilikiwe na wazawa na selikali kwa uwiano utakaokubalika, alafu wazawa ndo waingie ubia na makampuni ya utafiti na uchimbaji, hii itaiobdoa serikali kwenye mikataba ya rushwa,
Pia nafasi ya umiliki wa wazawa itahakikisha makubaliano leseni za uchimbaji yanakuwa ya kibiashara zaidi,

Wataalamu wa haya mambo ya uwekezaji wa sekta ya madini wanaweza weka sawa mawazo haya
Nakubaliana na wewe ndugu- kuondoa mentality ya Kijamaa kuwa Serikali ndo iwe kwenye kila kitu ni jambo ambalo limelirudisha nyuma sana taifa letu
 
Ushamba na ujinga wakuwachukia waliofaniwa, umetuathiri wabongo
Kweli kabisa, tunatakiwa tuachane na mentality za kijamaa za kuwaona waliofanikiwa binafsi na wenye hela zao binafsi ni wezi na watu wasiofaa.

Tuwe na akili na kupenda watu kufanikiwa kwa sababu wanaofanikiwa ndo wanafungua biashara na viwanda, kuajili watu na kulipa kodi nyingi zaidi ambazo zinainufaisha jamii yote kwa ujumla.
 
China walipata kiongozi mwaka 1976 baada ya kifo cha Mao. Anaitwa Deng Xiaoping , huyu ndo wachina wanamfahamu kama The Father of Reforms. Aliweza kuwabadiri wachina kutoka mentality za kikomunist na kuwapa mentality za kibiashara na kiuwekezaji jambo ambalo hadi leo linamfanya mchina kuwa mtu anaengalia fursa duniani.

Tunaitaji sana kubadili fikra zetu juu ya uwekezaji na biashara na kuachana na mentality za kijamaa ili kupata maendeleo ya kweli hapa Tanzania
 
Umejitahidi kuandika lakini bado sana, mawazo yako bado ni mwendelzo wa kuabudu watu siyo mawazo huru, not practical
Mimi si mmoja wanaobudu ila hutafakari jambo, kulifanyia utafiti kabla ya kulitolea uamuzi. Pia naheshimu mawazo ya wengine na kuyafanyia kazi.

Wanazuoni huamini, na ndio uhalisia, anachojua mwengine wewe hukijui. Hivyo kuheshimu mawazo ya binadamu mwingine ni ustaarabu, na kungeza busara na hekima.
 
Eti tajiri mkubwa anatekwa wiki mbili,

matajiri wengine wanafungwa ili kuwakomoa, wanabambikiwa kodi kubwa, ili kuua biashara,

wanaharibu mashamba ya mfanyabiashara, ambaye ana amini mlengo wa upinzani, au wapi tayari kuharibu biashara za wasiowaunga mkono

Au zile Sera mbaya za kijamaa za kutaifisha Mali za wafanyabiashsra

wafanyabiashara wanatekwa wanaporwa hela na Mali ili Waachiwe

Sidhani kama tutafanikiwa kiuchumi Bila usalama wa bishara na uwekezaji
 
Ni kweli kabisa, Kati ya mambo yanayotutia doa ni jinsi tunavyo watreat wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa katika awamu hii. Ni vizuri kujenga trust kwao ili wawekeze zaidi kwa manufaa ya taifa
 
Amani iwe kwenu wadau,
Natumai wote mu wazima wa afya tele. Kama kawaida nimekuwa na mfululizo wa kuleta thread mbalimbali kwa ajili ya kuchangia mawazo yangu katika jukwaa hili nikiamimi kuna siku wahusika watayaona na kuyafanyia kazi kwa kiwango kikubwa sana na mwisho tutapata matokeo chanya kama taifa.

Moja ya mambo ambayo nimaamini yameirudisha Tanzania nyuma kimaendeleo ni Sera za ujamaa zilizoingizwa nchini mwaka 1967 nchi ikiwa ni changa mno.

Kwa maono yangu niamini kuwa sera hizi ziliwafunga akiri jamii ya watanzania kiasi cha kuamini kila kitu ni Serikali tu kwa sababu Moja ya nguzo kuu ya ujamaa ni Serikali kumiliki njia zote za kibiashara na kiuwekezaji.
Ujamaa pia unawafanya watu wasifikiri juu ya uwezo wao binafsi katika kujiondolea changamoto za kimaisha.

Kwa nini nasema ujamaa ndo umeiangusha Tanzania kiuchumi
.
Kwa wale msiojua kabla ya sera za ujamaa Tanzania kulikuwa na wafanyabiashara na wawekezaji wengi sana, wazawa na wasio wazawa. Wawekezaji hawa waliwekeza kwenye Elimu, Kilimo, Ujenzi na Biashara.
Mfano ni mzungu Steyn aliyeleta kashikashi ya ndege zetu Africa KUSINI. Pia kulikuwa na wakulima wakubwa Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Iringa na hata mikoa ya kanda ya ziwa. Kulikuwa pia na wawekezaji waliojenga mashule kama wakatoliki na taasisi za Dini na pia walikuwepo wawekezaji wa kiasi a waliowekeza kwenye majengo maeneo ya Mzizima(Dar es Salaam), Mwanza, Kagera, Dodoma, Mbeya, Iringa, Tanga , Kilimanjaro, Arusha n.k. Sera ya ujamaa ilitaifisha sehemu kubwa ya mambo yote hapo juu na hapo ndipo tatizo lilipoanza.

Matokeo ya Sera za ujamaa kwa Watanzania
1. Ni kuondoa uwezo wa wananchi kufikiria juu ya uwezo wao binafsi katika kutatua changamoto za kimaisha

2. Kuharibu njia zote nzuri za kiuchumi zilizowekwa na wakoloni ambazo zilikuwa thabiti. Viwanda vilikufa, mashamba na biashara zilikufa.

3. Ambalo ni kubwa zaidi ni kuwepo kwa Fikra mfu kuwa mtu kuwa na pesa ni dhambi, beberu na mnyanyasaji

4. Kuharibu fikra za watanzania mpaka wanaoajiliwa serikalini kutowaza kibiashara na kiuwekezaji- Waajiliwa wengi wa Serikali na taasisi zake hawaoni thamani ya Biashara, hawawazi kibiashara na kupelekea uwekezaji mzuri kukwama kutokea Tanzania na wawekezaji kuikimbia Tanzania.

Nini Kifanyike.
1. Mtaala wa Elimu kuanzia shule za msingi hadi chuo ubadirishwe. Wanafunzi wafundishwe kujiajili, maana ya kazi binafsi na pia wafundishwe skills zaidi kuwawezesha kuwaza na kutenda kibiashara na kuona changamoto za kidunia

2. Sera za nchi zinadirishwe, uwekezaji wa ndani na nje ndo iwe first priority kwa taifa. Watu wawaze biashara, watende biashara na wafanye kila kitu kibiashara

3. Serikali iondoe influence kwenye uwekezaji na biashara. Sera zisiwe zinabadirishwa kila uchao ili kutengeneza confidence kwa wawekezaji wa ndani na wa nje.

Nawatakia weekend njema.
Kwangu mimi tungeanza naumwagiliaji nchi nzima sehemu yapili umeme kwamaana ukiwa naumeme viwanda vingekuja bila shida unapokuwa namaji na umeme vyauhakika uwezi kosa viwanda vingejileta tu Nalatatu kwamimi reli tatizo haikuwa usasa bali usimamizi mbovu nakuboresha ile kama walivyofanya kwenye shule kongwe ndege zingesubiri matokeo hayo yaukezaji sikama tulivyo yanunua hayo mandege kwasasa tusingekuwa namadeni makubwa kama sasa nahali ingekuwa nzuri mtaani
 
Kwangu mimi tungeanza naumwagiliaji nchi nzima sehemu yapili umeme kwamaana ukiwa naumeme viwanda vingekuja bila shida unapokuwa namaji na umeme vyauhakika uwezi kosa viwanda vingejileta tu tatu kwamimi reli tatizo haikuwa usasa bali usimamizi mbovu nakuboresha ile kama walivyofanya kwenye shule kongwe ndege zingesubiri matokeo hayo yaukezaji sikama tulivyo yanunua hayo mandege kwasasa tusingekuwa namadeni makubwa kama sasa nahali ingekuwa nzuri mtaani
Uko sahihi pia ndugu. Ila ni vizuri kwanza kuacha mentality za kijamaa ili tuweze kufanikisha haya yote.
Pia tuna Tatizo kubwa sana la utunzaji wa mazingira kupelekea hatari kubwa sana huko mbeleni ya kukosa Maji ya uhakika kwa shughuli za kilimo (hapa nimegusia juu ya suala la kilimo cha umwagiliaji) . Ila hili nitalitafutia muda niandike mapendekezo yangu humu.
 
Majibu mbona yanajulikana siku nyingi? Suluhisho la kuondosha umaskini Tanzania ni kuiondoa CCM madarakani haraka iwezekanavyo.
 
Katika mambo yaliyokosewa nchi hii ni siasa. Siasa za CCM za kimaskini, kijamaa, na kishamba awamu hii zinairudisha nyuma sana nchi hii.
 
Back
Top Bottom