Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,872
- 28,156
Amani iwe kwenu wadau, natumai wote mu wazima wa afya tele.
Kama kawaida nimekuwa na mfululizo wa kuleta thread mbalimbali kwa ajili ya kuchangia mawazo yangu katika jukwaa hili nikiamini kuna siku wahusika watayaona na kuyafanyia kazi kwa kiwango kikubwa sana na mwisho tutapata matokeo chanya kama taifa.
Moja ya mambo ambayo nimaamini yameirudisha Tanzania nyuma kimaendeleo ni Sera za ujamaa zilizoingizwa nchini mwaka 1967 nchi ikiwa ni changa mno.
Kwa maono yangu niamini kuwa sera hizi ziliwafunga akiri jamii ya watanzania kiasi cha kuamini kila kitu ni Serikali tu kwa sababu moja ya nguzo kuu ya ujamaa ni Serikali kumiliki njia zote za kibiashara na kiuwekezaji.
Ujamaa pia unawafanya watu wasifikiri juu ya uwezo wao binafsi katika kujiondolea changamoto za kimaisha.
Kwa nini nasema ujamaa ndio umeiangusha Tanzania kiuchumi?
Kwa wale msiojua kabla ya sera za ujamaa Tanzania kulikuwa na wafanyabiashara na wawekezaji wengi sana, wazawa na wasio wazawa. Wawekezaji hawa waliwekeza kwenye Elimu, Kilimo, Ujenzi na Biashara.
Mfano ni mzungu Steyn aliyeleta kashikashi ya ndege zetu Africa Kusini. Pia kulikuwa na wakulima wakubwa Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Iringa na hata mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Kulikuwa pia na wawekezaji waliojenga mashule kama wakatoliki na taasisi za Dini na pia walikuwepo wawekezaji wa kiasi a waliowekeza kwenye majengo maeneo ya Mzizima (Dar es Salaam), Mwanza, Kagera, Dodoma, Mbeya, Iringa, Tanga, Kilimanjaro, Arusha n.k.
Sera ya ujamaa ilitaifisha sehemu kubwa ya mambo yote hapo juu na hapo ndipo tatizo lilipoanza.
Matokeo ya Sera za ujamaa kwa Watanzania:
1. Ni kuondoa uwezo wa wananchi kufikiria juu ya uwezo wao binafsi katika kutatua changamoto za kimaisha
2. Kuharibu njia zote nzuri za kiuchumi zilizowekwa na wakoloni ambazo zilikuwa thabiti. Viwanda vilikufa, mashamba na biashara zilikufa.
3. Ambalo ni kubwa zaidi ni kuwepo kwa Fikra mfu kuwa mtu kuwa na pesa ni dhambi, beberu na mnyanyasaji
4. Kuharibu fikra za watanzania mpaka wanaoajiliwa serikalini kutowaza kibiashara na kiuwekezaji. Waajiliwa wengi wa Serikali na taasisi zake hawaoni thamani ya Biashara, hawawazi kibiashara na kupelekea uwekezaji mzuri kukwama kutokea Tanzania na wawekezaji kuikimbia Tanzania.
Nini Kifanyike:
1. Mtaala wa Elimu kuanzia shule za msingi hadi chuo ubadirishwe. Wanafunzi wafundishwe kujiajili, maana ya kazi binafsi na pia wafundishwe skills zaidi kuwawezesha kuwaza na kutenda kibiashara na kuona changamoto za kidunia
2. Sera za nchi zinadirishwe, uwekezaji wa ndani na nje ndo iwe first priority kwa taifa. Watu wawaze biashara, watende biashara na wafanye kila kitu kibiashara
3. Serikali iondoe influence kwenye uwekezaji na biashara. Sera zisiwe zinabadirishwa kila uchao ili kutengeneza confidence kwa wawekezaji wa ndani na wa nje.
Nawatakia weekend njema.