Kibunago
JF-Expert Member
- Jan 11, 2008
- 300
- 122
Umuhimu wa idara hii nchini unajulikana. Malalamiko dhidi ya idara hii nchini yameoneshwa na kutajwa katika magazeti, blogu, tovuti, vijiweni na hata kidogo Bugeni.
Mapungufu yameelezwa kwa namna tofauti tofauti na makundi mbalimbali mbali ya kijamii nje na ayumkini kutoka ndani ya idara, kwa Waastaafu na Watumishi waliopo katika idara yenyewe, alimuradi hawavunji kiapo chao cha pili cha Usalama kinachohusu kutotoa taarifa walizonazo bila idhini ya mamlaka husika kwa mujibu wa seria husika iliyopitishwa Oct.1996.
Mapungufu yanaweza kuorodheshwa katika makundi mbali mbali kufuatana na eneo husika. Pengine ni katika sheria na sera husika au muundo wa idara au ni mgawanyo wa kazi au ni mnyororo wa uwajibikaji au ni katika mamlaka na madaraka au uwezesho wa vitendea kazi na teknolojia au katika ujuzi na utekelezaji wa majukumu.
Haitoshi sisi wananchi kulalamika tu. Kupitia JF penye wachambuzi nakaribisha maoni ya nini ungependa kibadilishwe au kuboreshwa kivipi ili Idara iweze kuwa ya ufanisi zaidi kama inavyopaswa.
Mimi naanza na hapo penye ukolezo wa wino na kupigiwa msitari (bold & underlined).
Ujuzi na utekelezaji wa majukumu hutegemea sana aina ya rasilimali Watu ulionao.
Ni bayana kuwa duniani kote mambo kadhaa katika idara hii yanafanyika kwa usiri. Lakini si kweli kuwa yote yanafanyika wa usiri.
Katika karne hii, naona kuwa mwanzo wa mfumo wa kuajiri (recruitment process) au kushikiza mawakala katika idara hii unaweza kuwa wa wazi na wenye ufanisi zaidi kuliko ilivyo sasa.
Napendekeza kuwa, idara iwe na Tovuti (Website) na waeleze waziwazi madhumuni ya kazi ya idara hii, sifa za wanaotafutwa kufanya kazi katika idara hii na kutangaza nafasi (positions) wazi (a position doesnt equal assignment!) katika idara au vitengo vyake.
Na hata mahala ambapo idara inaweza kuweka matangazo au maelekezo yake yale yasiyo ya siri na pia hata wananchi wanaweza kuwasiliana na idara kupitia tovuti juu ya mambo mbalimbali yanayowahusu ingawa tunajua kuna namna nyingi ya kupata taarifa hizo.
Mfumo uwape nafasi watu waliojipima wenyewe katika vigezo vitakavyowekwa kwa Waomba nafasi za kazi, Mawakala n.k. Hii haimaanishi kuwa utaratibu makini wa vetting ufutwe la hasha; huo utakuwepo tu lakini idara iweke wazi matangazo kwa wote chini ya sera ya fursa sawa katika ajira kwa umma.
Kwa kufanya hivi Idara itakuwa inapanua wigo wa kutafuta rasilimali Watu wenye ujuzi , uzoefu mbalimbali kupambana na mazingira ya karne hii ya 21 na wenye maadili yanayopaswa. Aidha Idara itakuwa inajisogezea uhalali wake na ushiriano mwema toka kwa Wananchi kuliko ambavyo mtu anavyoweza kufikiri tu kuwa hawa jamaa ni jamii fulani ya siri tusiotakiwa kuijua au inayojitosheleza bila ushiriano tokwa kwa raia.