Pundamilia,
Yote tisa, ila hata kama tutabadilisha jina, kama hili la wapiganaji linakuudhi, basi labda wan JF watafute jina lingine lakini, labda tuwaiite ''Raia wema wa Tanzania'' kwa kipindi kifupi, SITTA amewafurahisha watanzania walio wengi ndani na nje ya nchi, amewafanya watanzania kufurahia siasa zaidi, naami 2010, watu wengi watajitokeza kwenda kupiga kura maana wengi sasa wanajua cha kufanya, tofauti kabisa ni kile jamaa yetu alichotufanyia, eti maisha bora ka kila mtanzania, aibu tupu.
Yaani nikwambie, sasa hivi Sitta ana heshima kuliko Msanii. Just by comparison. Wewe endelea tu kutetea chama, ila tukirudi Dodoma, tunaibuka na jipya, si umeona mwenyewe jinsi ambavyo serikali ilivyotolewa baru, mbiombio kupitia mawaziri wake katika bunge lililopita,wanatulteate ripoti za kifisadi bungeni tena mbele ya Sitta, halafu usifikiri ni Sitta tu, pia watanzania wanamuomba na Mungu pia asaidiê, hivyo vita ni kali mno, utashangaa tu jamaa wanapeta, kwa mfano, angalia Dr. Slaa, akiwa chumbani akagundua kuwa ametegeshewa kinasa sauti, utasema uchawi, kumbe sio, angalia Dr. Mwakyembe, watu walijua sasa basi, tumemshau, kumbe licha ya kuwa ajari ilikuwa mbaya, lakini anapeta, hivi kwa hii mifano michache, naomba ujue kuwa sidhani kama JK atapita 2010, alikosea sana kutudanganya.