Nini iwe hatma ya Wapiganaji walio CCM, Warudishe kadi au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini iwe hatma ya Wapiganaji walio CCM, Warudishe kadi au?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Field Marshall ES, Aug 22, 2009.

 1. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Wakuu wote JF yaani Great Thinkers,

  - Ninaamini kwamba kilichotokea majuzi Dodoma ni only a big set back lakini sio mwisho wa vita na mafisadi, sio siri kwamba wapiganaji wetu kwa sasa spirit ziko chini, sasa huu ni wakati wa Great Thinkers, kuwapa ushauri of what to do next.

  - Ninaomba kutoa shukrani kwa wakuu wote wa JF waliotoa maoni yao mazito kule kwenye thread ya Kusila, yamesaidia sana kuwapa moyo baadhi ya wapiganaji, ambao nimewasukumia tayari.

  - Ninaomba mawazo hapa ili niwafikishie kama yalivyo, binafsi ninaanza kuwaza kwamba huenda huu ni wakati muafaka kwa wapiganaji kurudisha kadi zao za CCM, kwa sababu sasa hawawezi tena kupiga kelele za kuikosoa serikali, wala CCM mbele ya public, wanatakiwa kuyafanya haya ndani tu ya vikao vya chama chao CCM, hapa nia na madhumuni pamoja mengine mengi ni ili sisi wananchi tusijue wala kusikia ya huko ndani ya vikao vyao, na vile vile kuwakimbia mafisadi kunaweza kuwapa mwanya wa kutumaliza kabisa sisi wananchi!

  - Sasa hawa wapiganaji wafanye nini as we move forward na hii vita na haya manyang'au?, wabaki CCM au warudishe kadi, au what else? Tujadili wakuu ili tuwafikishie mawazo yetu wananchi!

  Respect.


  Field Marshall Es! - ni Sauti ya Umeme!
   
 2. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kurudisha kadi naamini itakuwa kujimaliza wenyewe hususan kama bado wanania ya kuendeleza mpambano mjengoni.

  Makombora dhidi ya ufisadi hayatakiwi kurushwa kutokea upande mmoja tu, yaani kutokea upinzani peke yake. Naamini mafisadi wanahitajiwa wapingwe toka pande zote yaani kutoka vyama vya upinzani, ndani ya ccm na kutoka civil societies kwa namna hii vita hii inaweza kuchukua muda mfupi zaidi.

  Njia muhimu ni kukaidi uamuzi wa kuwafunga mdomo na kuwaachia jukumu la kuwafukuza kwenye chama nec. kwa namna hiyo ccm
  itadhiirika moja kwa moja na wananchi kama chama kinachotetea mafisadi. Aidha kwa kuzingatia kwamba uchanguzi upo karibu
  naamini ccm itakuwa na wakati mgumu sana kufikia maamuzi ya kuwafukuza wapiganaji kwani hawajui wananchi wata-react namna gani.

  Pamoja na ukweli huu upo pia uwezekano wa ccm kujaribu maji kwa kumfukuza mpiganaji mmoja/wawili ili kuona wananchi wata-react vipi na kupiga mkwala kwa wapiganaji wengine.
   
 3. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,110
  Trophy Points: 280
  my opinion warudishe kadi za CCM wajiunge na wapiganaji wenzao akina Slaa, Minyaa. Otherwiae kama wanaubavu kama ule wa Shibuda basi wabaki na waendeleze moto ili wakimalizie kabiasa hicho chama. As i known for now, is almost impossible to revive CCM kwasababu sauti za wapiganaji haziwezi kubadili kitu ndani ya CC, NEC etc.

  Tuzingatie kwamba, mabadiliko yeyote makubwa ndani ya chama huwa yanaongozwa na viongozi wa juu. Tofauti iliyopo CCM viongozi wa juu (Kikwete, Makamba, Msekwa, Karume na Chiligati) either wapo upande wa mafisadi au wanawaogopa mafisadi hivyo they are defeated so can't do anything contrary to fisadis motion.

  Lazima tuzingatie kwamba, CCM kwasasa ni dhaifu sana kiitikadi, kimsingi haina idikadi inayoeleweka. Hivyo, haina mwongozi imara wa kisera na kiitikadi. CCM haina imani tena, ile imani ya chama iliyopo kwenye kila kadi ya mwanachama ni maandishi tu, wala haipo akilini (achilia moyoni) mwa viongozi wa juu. So, katika hali kama hii wapiganaji hawawezi kutimiza malengo yao kama kweli wameamua kuirudisha nchi ktk heshma, taadhima na ustawi wa jamii, siasa na maendeleo kwa ujumla.
   
 4. m

  masawila Member

  #4
  Aug 22, 2009
  Joined: Dec 25, 2007
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mzee FMES,
  -Kwanza heshima mbele, hongera, pole na Akshante kwa kutuletea habari moto moto kutoka jikoni ndani ya NEC.
  -Kwanza kabisa, Nadhani its a good idea kwa wapiganaji ndani ya CCM kuanza kufikiria exit strategy na jinsi watakavyoendeleza kupigania haki za wanyonge post CCM. At the same time mimi ningewashauri kuwa na exit plan kuliko kuondoka kwa hasira bila ya kuwa na effective plan B. Unajua kwa kumbukumbu zangu za hivi karibuni, hakuna mwanasiasa aleyetoka CCM akaenda upinzani na kuwa successful, ie: Mrema et al. Naamini kabisa the only way CCM wanaweza kutetereshwa from the insiders, na kwa hao insiders waka unite, wakatengeneza exit strategy(kutoka kwa pamoja), wakaunda chama chao au waende kwenye chama chenye infrastructure nzuri and most importantly, wafanye yote hayo pasipo high hierarchy ya chama kuwa na idea of what's about to happen.
  -The element of suprise will paralyze the leadership na wasijue jinsi ya ku respond haraka and swiftly.
  -At the moment, watu wote wanajua kwamba watu wa usalama wanawafuatilia nyendo zao zote hao wapiganaji, kwa hiyo timing si nzuri kwa sasa.
  - Lakini, huu ni muda mzuri na muhimu kabisa kwa wapiganaji ndani ya chama kuanza kufikiria maisha yao post CCM if they truly want to make a change.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa maoni yangu wasitoke, waendelee kupambana humo humo ndani kwa sababu wakisema kutokea nje, wataonekana wanasema kwa sababu nin wapinzani. Kama wakitoka wenyewe, itakuwa ni dalili ya kushindwa. dawa ni kuendelea kupambana na ikibidi wafukuzwe na hilo litawajengea heshima na kukishua hadhi CCM kwa sababu wanawafukuza watu wanapigana dhidi ya ufisadi. hapo, wanaweza kuwa na nguvu ya kuendeleza mapambano hata wakiwa nje.
  Na kama wakiwa na strategy nzuri, wanaweza kutimiza 'unabii' wa mwalimu kwua upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM
   
 6. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Kama lengo lao ni kukisaidia Chama ni bora waendelee kupambana na huo Ufisadi wakiwa ndani ya Chama,kujitoa katika Chama/kurudisha kadi sidhani kama itakuwa ni hatua muafaka.Waendeleze mapambano humohumo ndani ya Chama mpaka mafisadi waondoke/wakimbie ndani ya chama...Kurdisha kadi/kuondoka katika Chama itakuwa ni sawa na kunyoosha mikono/kuwapa ushindi Mafisadi..Wasikate tamaa waendelee na mapambano mpaka kieleweke.......
   
 7. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kwa upande wangu huko nyuma nimekuwa very skeptical kuhusu hawa wapiganaji ndani ya CCM na naamini nilikuwa na sababu za msingi kabisa kuwa na msimamo huo. Hata hivyo baada ya kutafakari (na bado naendelea) yote yaliyojiri kwenye huu mkutano wa siri wa NEC-CCM, nalazimika kuwapa benefit of doubt japo si kwa asilimia mia moja.

  Kama kweli wako tayari kusimamia na kutetea kile wanachokiamini huu sio wakati mwafaka wa kurudisha kadi. Kwa vile naamini, kwa sababu nyingi tu, kuwa wananchi wengi wako upande wao, huu ni wakati mzuri wa kutulia na kupanga jinsi watakavyoweza kuwakabili wasaliti hao kwenye eneo lao la kujidai, ndani ya Bunge wakilindwa na sheria mama, Katiba.

  Msimamo wao usioyumba ndani ya Bunge utawalazimsha wapinzani wao kuchukua hatua ama ya kuwafukuza au kusalimu amri na kujiondoa chamani. Uzuri wa njia hii ni kuwa kwa namna yoyote utafunga mlango kwa mbinu zozote za upatanisho wa kilaghai. CCM, kama ilivyo, imefikia hali ambayo haina manufaa yoyote kwa mwananchi wa kawaida.

  Kwa kuwa yaliyojiri kwenye kikao cha NEC-CCM, hayakuijitokeza kwenye vikao vya kamati ya wabunge wa CCM, nina hakika hawa wapiganaji wataungwa mkono na wabunge wenzao wengi ndani ya Bunge. Hapa si swala tena la itikadi, ni swala la kulinusuru taifa kutoka mikononi mwa wezi, mafisadi na wahujumu wa taifa letu - taifa linateketea ndugu zangu.

  Muda mwafaka utafika ambapo kadi ya CCM itaogopwa kama ukoma na muda huo naamini hauko mbali. CCM kwa kubaka katiba ni kama, kwa maneno ya Mwalimu, mtu kula nyama ya binadamu - huyo haitwi mtu tena, anapoteza sifa hiyo. Waliokuwa wakifoka Dodoma mpaka mapovu yanawatoka wakitaka nyama ya Spika Sitta si watu, ni manyang'au -
  A luta continua - mapambano yanaendelea.
   
 8. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kuwepo ndani ya CCM au kuwa nje ya CCM inategemea na malengo yao binafsi au ya pamoja.


  Moja kati ya ahadi walizozitoa wakati wanajiunga na Chama Cha Mapinduzi waliahidi kuwa:
  "Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika."

  Vilevile walikubaliana na masharti ya kuwa miongoni mwa wanachama wa Chama Cha

  Mapinduzi kwa kukubalia moja wapo ya masharti:
  "Kuwa mtu anayeheshimu watu. Kuwa mtu anyefanya juhudi ya kuielewa, kuieleza, kuitetea, na kuitekeleza itikadi na siasa ya CCM. Kuwa mtu mwenye kuamini kuwa kazi ni kipimo cha utu, na kuitekeleza imani hiyo kwa vitendo."

  Kwa mantiki hiyo basi, kama hao 'wapiganaji' wanaona kuwa hawako tayari kutii ahadi zao na kukubaliana na masharti ya Chama Chama Mapinduzi, nadhani ni wakati mwafaka kwa wao kurudisha kadi na kuondoka na kwenda kule ambako watatimiza malengo na ndoto zao.
  CCM ni chama kilichojengwa katika misingi madhubuti na maamuzi yake si ya mtu mmoja ni yale yatakayotokana na vikao vya kidemokrasia. Dhamana kubwa waliyokuwa nayo viongozi wote wa Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha kuwa wanakijenga Chama kiendelee kuwa imara wakati wote kwa faida ya na manufaa ya wanachama wake.
  Maamuzi halali ya vikao vya Chama hayana budi kuheshimiwa na kiongozi yeyote mwenye wazo mbadala na maamuzi hayo basi ana haki ya kuyasilisha kwenye ngazi za vikao vya Chama kwa kufuata utaratibu ulioweka.
  Washauri hao 'wapiganaji' wako kuwa kama hawaridhiki na maamuzi ya NEC basi wafuatate taratibu zilizopo ndani ya chama za kulalamika au la basi warudishe kadi, watafute pa kwenda.
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Eti wafanye nini?
  Warudishe kadi?
  Nani kati yao aliye na ujasiri huo? Nitajie mmoja tu!
  Hawa kila siku wanapiga kelele "patachimbika hapa", wakiwa bungeni tu lakini wakitoka kimyaaaaaaaaaaa.
  Usanii tu.Aliye na ujasiri awe wa kwanza kurudisha kadi yake maana si upepo wameuona?
   
 10. Z

  Zurich Member

  #10
  Aug 22, 2009
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika."

   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tatizo hata hao tunao waita "wapiganaji" kuna wengi tu kati yao ni wanafiki and they are just paying lip service. Kama wapiganaji wapo very serious waunganishe nguvu na kuunda chama kipya from the ground up. Ila hii ita hitaji kuji tolea kwa hali ya juu na kutambua kwamba wao wanaweza wasi faidi hayo matunda binafsi(kwa maana wasianzishe chama kipya kwa kila mmoja wao kuwa na dhana ya kupata cheo fulani). Tanzania ina hitaji chama walau kimoja cha upinzani chenye nguvu na hiyo inaweza kuwa ndoto ya wapiganaji hao.
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0


  - Wakuu wote hapo juu ahsanteni sana kwa majibu yenu ya kistaarabu na yenye kuonyesha Great Thinking indeed, naona wengi so far tunakubaliana kwamba wakibaki watatusaidia wananchi zaidi, ingawa swali bado kwamba sasa watafanya nini?

  - Maana mafisadi wameweka mtego mzito sana, wakiendelea wataishia kuwang'oa kwenye chama, that they mafisadi watafanya wala sio siri, sasa wakibaki watafanya nini humo ndani ya CCM?

  Respect.


  Field Marshall Es!
   
 13. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Kamanda...Kwa hali ilivyo ni kwamba tayari Mafisadi wameelemewa na mapambano haya,ndo maana unaona wanatapatapa na kuja na kila aina ya mbinu kuwamaliza wapiganaji hawa shupavu.Sasa ni bora hawa jamaa(wapiganaji) wazidishe juhudi katika kupambana na hao mafisadi hasa katika kipindi hiki kigumu cha kuelekea uchaguzi mkuu,kusema waondoke CCM itakuwa ni kuwapa ushindi mafisadi na kuwafanya wapete katika uchaguzi mkuu wa mwakani...Cha msingi wabaki na waendelee na mapambano maana waTanzania tunaona na kusikia kila kitu kinachoendelea.........
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu wangu vipi unaita Ufisadi kwamba ni lengo la kuimarisha chama? Halafu bado hujaelewa the ishu ni kwamba Spika anatakiwa apindishe sheria za bunge ili kukumbatia sera za ufisadi, wabunge wapiganaji hawakuapa kiapo cha kutetea ufisadi bungeni,

  - Wamelaaniwa kwa sababu wanawashambulia mafisadi bungeni so kwenye chama, jaribu kuelewa tofauti, Spika sio mkuu wa chama ni Spika wa bunge, wapiganaji walioshambuliwa hawakushambuliwa kwa sababu wameshambulia chama, ila kwa sababu wameshambulia serikali bungeni, kitu ambacho ni wajibu wao kwa mujibu wa katiba!

  - Ninaheshimu sana mawazo yako na ningeshangaa kama hii thread ingefika mpaka mwisho hujajitokeza kwa njia moja au nyingine, lakini bado huelewi mkuu the real ishu hapa, Spika ametimiza kazi yake bungeni, kama amekosea basi atakuwa amekosea kisheria, yaani amevunja katiba, sasa kwa nini CCM isimfikishe kwenye sheria, badala yake inamuita kwenye vikao visivyohusu katiba ya Jamhuri na kumtishia kwa kazi yake bungeni that is a crime byitself, sisi wananchi tungekua makini na wenye uwezo sasa hivi tulitakiwa kuwafungulia mashitaka NEC ya CCM, kwa kuvuruga katiba ya jamhuri , that is what they did Dodoma juzi ni kuichafua katiba ya Jamhuri, ndio maana Karume akagoma kwenda kushiriki kwenye kuvuruga katiba ya Jamhuri ya Muungano.

  - Hebu nenda mkuu usome tena, kama ilani na itikadi ya CCM kama inasema CCM inafuata ufisadi, kwa hiyo hoja zako hapo mkuu nafikiri ni clear kwamba ni batili, wapiganaji wameapa kiapo cha kusimamia taifa na Jamhuri sio sera na itikadi za kifisadi.

  Respect.

  Field Marshall Es!
   
 15. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0

  - Strong na right on the money, mkuu ninakusikia sana.

  Respect.


  Field Marshall Es!
   
 16. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Pa1 Kamanda
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0

  - Mkuu ahsante sana for your Great Thinking, nimekusikia maana hii ni demokrasia makini tunaheshimu mawazo ya kila mtu hata haya yako!

  Respect.


  FMEs!
   
 18. Z

  Zurich Member

  #18
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  "Nitakuwa mwanachama mwaminifu kwa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika."


  Uzito mkubwa uko katika haya maneno ya katikati ambayo mafisadi hawawezi kuyaona, "Nitakuwa raia mwema wa Tanzania'' Wapiganaji, wanataka kutunza hii ahadi, ila mafisadi wanaangalia tu kuwa mwaminifu kwa CCM, tena sio ile CCM ya mzee wetu Nyerere, eti kuwa mwaminifu kwa CCM ya sasa hivi, yaani kama wewe ni mwana dini, halafu uko katika hicho chama, tena kwa bahati mbaya ukawa ni mjumbe wa NEC, hapa kila ukiingia MISA, au msikitini ni kutubu tu, maana umeshindwa ''kuwa raia mwema wa Tanzania'', yaani kwa maana rahisi, ili uwe mwanifu kwa CCM ya sasa hivi, inabidi uwe nyang'au kwa wananchi(fisadi), na kila unapopiga magoti kusali, kanisani au msikitini unajikuta kila wakati ni kutubu tu maana hiyo dhambi haitoki, na haiishi, . mwana JF mmoja kaiweka vizuri, ni sawa na kula nyama ya mtu, mpaka pale utakapoamua kuwa raia mwema wa Tanzania. Kwa ushauri wangu, hawa wapiganaji wakubali tu kutoa maisha yao kwa ajili ya watanzania nzuri walio wengi zaidi ya milioni 40, mafisadi wako wachache hawafiki 5,000 . Wako wengi waliopoteza maisha yao kwa ajili ya Tanzania ya kesho wakiwemo akina Sokoine, siku moja ndugu zao wataipata Tanzania iliyojariwa maziwa na asali, utajiri wake ni vizazi na vizazi. Tanzania yenye amani ya kweli, ambapo kila raia ana uhakika wa kula chakula bora, kunywa maji safi, na kupata elimu bora, na kupata malazi safi kutokana na baraka nyingi na utajiri wa nchi yetu.

  Sisi raia tutazidi tu kuwaombea hawa wapiganaji wasipatwe na ugonjwa wa moyo, maana kujitahidi kuwa mtiifu kwa CCM ya sasa, da! Inahitaji uwe na moyo wa SOKWE na sio wa binadamu.
   
 19. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mimi nimesema wabaki lakini uzi uwe ule ule - kutetea maslahi ya taifa, kutetea uhuru wa Bunge na kuisimamia na kuilinda Katiba. Sioni mtego hapa kwa sababu kama watasimamia wanachoamini ni sawa bila kutetereka na CCM ikaamua kuwatosa, watakuwa wameshinda awamu ya kwanza kwenye hii vita - watapokewa na wananchi kama mashujaa. Kinachonisumbua ni haya maneno yafuatayo ya Mzee John Samwel Malecela kabla ya huo mkutano,
  Kwenye mkutano wa NEC-CCM JM hakuwepo, je ni kwa sababu alijua matazamio yake hayangefikiwa au ndio mbinu mpya anazosema CCM haijawahi kuzitumia kupambana na Upinzani.
  I am trying hard to believe that somebody, somewhere, somehow is not trying to pool the wool over our eyes !
   
 20. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Hii ndio tunaita Great thinking!, ubarikiwe tu mkuu!

  Respect.


  Field Marshall Es!
   
Loading...