BilliGates
Amekuja inawezekana tu kwakuwa pesa yake ndio inayomfanya aje.
Mtu akiwa na pesa hitaji lake la kwanza ni uhakika wa kupata chakula.
Pesa ikiongezeka linakuja hotaji la pili ambalo ni kujilinda na mazingira yake, hapo anatafuta pa kulala penye usalama,
nguo nzuri, nk.
Pesa ikiongezeka binadamu anaanza kufikia hatua ya hitaji la tatu la zoezi la kuanza kuweka akiba ili arahisishe maisha yake kama kujenga nyumba au kununua gari hapo baadae nk.
Pesa ikiongezeka binadamu anaingia hatua ya nne ya kutaka kujulikana na watu kuwa anazo, hapo wale wapenzi wa Ngwasuma utamwona mtu anajiita Papa Nyamihela kazi yake ni kumwaga pesa jukwaani na na kupenda kusifiwa.
Kwa watu wa dini mtu ananza kutoa sadaka kubwakubwa na kugharimia safari za mchungaji au Shehe ktk kuimarisha dini yake. Watu wengi wanaanza kuwekeza katika miradi ya biashara wakifika katika hatua hii.
Pesa ikiongezeka sasa mtu anaingia katika hatua ya tano ya kuzigawa pesa zake kwa jamii yote anayoona inafaa.
Huyu mtu sasa anaifikia hatua ya kutaka kutambuliwa kimataifa na analindwa na serikari.
Analindwa na kufuatiliwa na serikari kwasababu asije akarubuniwa na waharifu na akaamua kuwafadhiri na kusababisha usimbufu mkubwa.
Anaweza akaunda jeshi la uasi na akaipindua serikari hivyo kila nchi anayoenda anakuwa anafuatiliwa na kulindwa ma nchi husika.
Hitaji hili la tano ni la mwisho kwa mwanadamu, hapa kazi yake ni kuunda taasisi za kutoa misaada kwa jamii.
Bill and Merinda Gates na Roockfera foundations, ni moja ya taasisi za matajiri zinazojihusisha kusadia jamii duniani.
BillGates amekuja kutimiza hitaji hili la tano la mtu mwenye pesa nyingi sana.