Nini hupelekea Wasomi wa Tanzania kukimbilia siasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini hupelekea Wasomi wa Tanzania kukimbilia siasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Mar 3, 2012.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Taifa letu liko kwenye kipindi kizito sana kuvuka kwenye nyanja ya siasa na uchumi.Lakini tumefika hapa kivipi?Jibu langu kwa kujiuliza huko swali hilo na kujifunza kupitia kuona na kusoma tatizo la msingi na kubwa walilonalo watanzania ni la wasomi wengi wa Taifa hili kuwa ni majisifu, ufithuli, kujigamba, wenye kujitwalia bila haki ,jipachika hasa bila haki, jitwaza,jipachika utukufu wa Taifa kwa mgongo wa siasa kufaidi matunda ya uchumi.[Allogance and Arrogate]

  Someone who is arrogant behaves in a proud, unpleasant way towards other people because they believe that they are more important than others.

  If someone arrogates to themselves something such as a responsibility or privilege, they claim or take it even though they have no right to do so.

  Leo hii Mtanzania aliyesomeshwa kwa mamilioni yapesa kwenye taaluma husika wamekimbilia kwenye siasa kwa kujua watakaa kwenye maamuzi na kuwa na kofia ya kujitwalia keki ya Taifa kimya kimya.Ni kwa wao kuingia kwenye kofia ya maamuzi leo Taifa halina watu wa kulishape [Think Tank],Wataalamu wa kilimo,maengineer,maprofesa, madaktari wa vyeo na madaktari wa Taaluma,walimuna wanasheria wote wamelundikana Bungeni na hatimae kuwa wana itikadi baada ya kuwa wanawataifa.

  Kwa wenzetu taaluma pia umpelekea mtu kuwa ni aina gani ya mwanasiasa katika ulingo wa siasa,wasomi wa masomo ya political economy,mausiano ya kimataifa, wanasheria,watu wa masoko na wachumi ndio ambao kwa namna fulani wamejikuta kuwa wanasiasa.Leo hii kwa Tanzania sivyo.

  Tumezalisha lundo la wasomi kila mwaka hawakai ofsini kuwa engineers wa kujenga Nchi kwa Taaluma zao bali wanatayarisha michakato ya kugombea ubunge ili atimae achaguliwe kuwa waziri hatimae kupata upofu wa si hasa.

  Tuangalie vyanzo vya matatizo yetu,ebu pitieni CV za wabunge wa Taifa letu kila mmoja wekeni hapa,pimeni wahusika wangetumika sehemu husika pengine leo tusingekuwa na wanataaluma kwenye foleni queue ya kukusanya pesa ya umma kupitia miradi ya serikali ili kuwania ubunge na presidential appointment huku Taifa likiwa limesimama kwa kukosa watu wa kuengineer mambo ya kusogeza Taifa mbele kwa kuanda mikakati.

  Je na wewe ni Mwanataaluma msomi?
   
 2. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  wanajifanyaga arrogate

  reality:we got bunch of arrogant
   
 3. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Argument zako ni very flimsy. Umeandika thread hii bila kufanya utafiti wa kutosha. I can't do it for you for sure.Please go back to the drawing board.

  Hint:
  Wasomi wa kweli hawako kwenye siasa, kwasababu hawawezi siasa. Wao ni watu wa facts. Walioko kwenye siasa huku wakidai ni wasomi ni matapeli wa elimu, sio wasomi.
   
 4. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,140
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Wasomi wakithaminiwa na wao wataheshimu taalum zao...,
  Ila kama wanasiasa wataendelea kuivuruga nchi hii , wasomi watakimbia taaluma zao
  au wataikimbia nchi .
  Hivi tunajua ni kuna madaktari bingwa wameshaondoka nchini
  kutokana na mizengwe ya mgomo wa majuzi tu .
   
 5. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wewe ndio unconvincing kwa udogo fanya tafiti kwa CV za wabunge wengi ni watu wenye elimu kubwa sana kwenye taaluma zao husika,uenda una conlude kwa kuangalia wabunge walio mawaziri ujui ndani ya bunge la wabunge walio kwenye Bunge letu wakiwakilisha majimbo ya mikoani,wengi ni maengineer, madaktari, wanasheria, wachumi na wenye uzoefu mkubwa sana kwenye sekta husika.Wametoka kwenye vitengo vyao kwenda kugombe ubunge eti wameombwa na wazee wao huko vijijini mwao.Vipi nawe ni mmoja wao nini?
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tanzania nayo kuna wasomi? waliifanyia nini zaidi Tanzania hao wasomi?

  Nilicheka sana nilipokuwa natazama kipindi kimoja Mlimani TV, wakati watu duniani wanatumia teknolojia ya Waste to Energy kwa miaka sasa na kila siku zinavyokwenda inaboreshwa, msomi wetu wa chuo kikuu anatamba na teknolojia yake open sewer disposal ambayo haina zaidi ya kuzidisha mnuko, nzi, na usumbufu, anasema eti inasaidia kusave kuja kuzolewa maji taka na magari. Na anasifiwa mpaka kwenye TV.

  Juzi nikaona anasifiwa nani sijui Mwanza eti kavumbuwa barabara za kutumia mawe, wakati barabara za mawe zipo kabla ya ujio wa Yesu kwa miaka 2000. Wakati wenzetu wana "chemical" unaimwaga kwenye barabara ya udongo na udongo unageuka jiwe. Sisi tunabomoa mawe ambayo ni natural stabilizers za mazingira, ngoja wayang'oe kwa wingi mje kusikia kasheshe za maporomoko ya udongo wakati wa mvua huko Mwanza.

  Hao ndio "wasomi" wa Tanzania.
   
 7. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ndio maana nikasema wasomi waliogeuka kuwa wansiasa sasa wamekuwa arrogant na arrogate hivyo kinachozalishwa watu wanapodai haki wanaanza kutengeneza mazingira ya pofu kwa kuwa wanajua na wanaufahamu na ndio maana hata kikwete alipowaludishia mswaada wa posho kuwa wakatafakari kwa umakini kuhusu posho wakamgeuka kuataka kumpiga chini,walipoona imeshindikana leo wabunge karibia sabini wanataka kuacha ubunge kama sio arrogance na arroagate ni nini?
   
 8. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,140
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Mkuu DSN
  wasomi wana haki kama alivyo mtanzania yeyote mwenye sifa stahiki kuingia kwenye ulingo wa siasa na kuiongoza nchi
  hii ,kuwa katisha tamaa wasomi hakutasaidia kitu, zaidi zaidi tutapata vipofu ambao watatupeleka pabaya zaidi,
  tujenga vijana wazalendo , tujenge taifa lenye wasomi wazalendo , haya matatizo mengi yatapungua ,

  BTW ,Mkuu kwenye RED , hiyo ni tishia nyau tu, 2015 watu kukatana mapanga kwenye kura za maoni tu CCM halitakua suala la ajabu kabisa
   
 9. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160


  Let them show their true colour

  1. Hivi kwenye population ya nchi na wasomi waliopo unataka tuanze kujadili approximately watu mia tatu ambao kwa utashi wao wamechagua siasa over professionalism???

  2. Tangu wamejiunga na siasa effect ya taaluma walizoziacha ni significant enough to cause a delay or static sectorial developmemt

  3. Katika taaluma yako una mmiss nani ambaye kwa sasa ni mbunge na pengo aliloacha haliwezi kuzibika????

  4. Tunakosa umoja na kusimamia taaluma (ethics) ndo tatizo letu na wala si hao waloamua kutoka wazi mchana kweupe.......seen doctors???? Tulobaki ni wengi kuliko waliotoka ila tunalia sana kuliko kujua nini cha kufanya
   
 10. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Criticism bila alternative ?????? So ulitaka wafanyaje kwa mfano au bado unaamini maendeleo ni "Rostowian" ???????
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Maendeleo na usomi ni pale alipopaacha mwenzako wewe kupaendeleza, sio wewe urudi nyuma miaka 2,000 kwa kupanga mawe ukasema umevumbuwa barabara za mawe na kusahau kuwa hizo ni stabilizers.

  Talking about alternatives? what is so hard about making a stone paved road mpaka iwe ni kiroja cha kutangazwa kuwa ni ubunifu? what is so hard about making open sewer and giving it another name halafu utuambie amegunduwa njia mbadala ya maji taka?

  Halafu TV inakutangaza kwa kukusifu badala ya kukuponda kwa kuturudisha nyuma na kuonesha wenzako sasa hivi wako wapi. Hapo unaendeleza au unadumaza?

  Gas tunayo hawa jamaa wasomi wangekuja na simple gadgets za kuifanya itumike majumbani, kwenye magari na kuliokolea taifa mabilioni leo ningewasifu sana. Kwenda kujisifu kuhusu barabara za mawe, khaaa! au open sewer! hatuoni hata haya wala hatujui vibaya. Halafu kaletwa mkewe, anajisifu anatumia hiyo open sewer nyumbani kwake, pale anapoongea unahisi anjilazimisha kwani ingekuwa TV inaleta na harufu na sio picha tu na sauti hakuna ambae angekaa nyumbani kwake siku hiyo.

  Mfano Brazil, wanalima miwa mingi sana, ili kusaidia hilo zao na wananchi, sasa hivi mpaka vituo vya mafuta karibu vyote vya Brazil, unanunuwa "gongo" unatumia kwenye gari, kwetu hapa "gongo" tunalifanya ndio kinywaji cha taifa kwa kubadilisha "cognac" ya wazungu na kuiswahilisha na kuiita "Konyagi", wenzetu wanatumia kwenye magari. Halafu bado tunajisifu.
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Wasomi wa Tanzania hakuna walichofanikiwa zaidi ya kufanya ufisadi tu, hizo elimu wanazojitapa nazo zimelisaidiaje taifa letu kutoka kwenye dimbwi la umasikini.

  Tanzania ni kati ya nchi 20 masikini wa kutupwa duniani baadhi ya nchi nyingine zinakuwa masikini kutoka na vita, kama DRC, Burudi, Somalia, Angola, Rwanda.

  Kiukweli Tanzania hakuna wasomi kuna wasomi makanjanja tu.
   
 13. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa hakika wasomi wetu wengi ni wachumia tumbo. Si wale waliobaki kwenye taaluma zao wala wale waliokimbilia kwenda kupiga domo domo,wote tu wanaongozwa na njaa za matambi tambi yao na ndo maana katika taasisi zetu ambazo zlitakiwa kimsingi zifanye kaz kitaalam,zimegeuka kuwa political wings za wanasiasa. Mifano mingi tunayo kuanzia jeshi la polis,na vyombo vngine vya usalama cvtaji,wataalam waliotakiwa watoe facts wamekuwa na kaz ya kuwafurahisha wanasiasa ili wawape nafasi bas ilimradi tu wote ni wachumia tumbo.
   
 14. b

  bantulile JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,439
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Tatizo la wasomi wa Tz ni mfumo wa elimu. Waalimu wengi hutaka mwanafunzi ajibu swali kwa kukariri neno kwa neno alivyofundisha yeye, sio ajibu kadri alivyoelewa na kwa maneno yake mwenyewe. Ukijibu jinsi ulivyoelewa na kwa mpangilio wako mwenyewe, hakika kwa elimu ya Tz utaambulia 0. Sio kosa la waalimu bali ndivyo na wao pia walivyofundishwa. Neenda vyuoni uone jinsi wanafunzi wanavyohangaika kudesa past paper za watu. Aina hii ya elimu inafanya wanafunzi kukosa kujiamini, kukosa ubunifu na udadisi.

  Ukitumia elimu yako kikamilifu wanasiasa wanakutosa na mwanataaluma mwenzako anakuja kuyatekeleza yaleyale uliyoyakataa wewe kwa misingi ya kuhofia kukiuka matakwa ya kitaaluma. Angalia wanasiasa ambao hupelekwa nje wakati kitaaluma hakukuwa na haja ya rufaa kwenda nje, anagalia majengo yanayopitishwa wakati hayakukidhi viwango vya ubora. Tazama zabuni zinzopitishwa kwa maelekezo ya wanasiasa. Mwanataaluma, usipotii siasa sio tu unakosa mkate, bali pia unaadhibiwa adhabu ambayo hutakaa uisahau. Kama ulikuwa Kamishena wa Bajeti Makao makuu wizara ya Fedha na uchumi utaenda kuwa mkuu wa bajeti Kamachumu.

  Mwanataaluma kama mtu mwingine yeyote naturally anataka ku-maximize happiness na ku avoid pains.

  Hivyo hawezi kung'ang'ania taaluma ili aje ateseke tena pamoja na familia yake. Atakosa amani hata ndani ya familia yake. Wote wataona elimu yake haikumsaidia kitu.

  Katika somo la Historia tunajifunza aina za resistance mfano Adaptive na Active kama vile Maleale wa Moshi aliresisst adaptively na Mkwawa wa Kalenga aliresist Actively . Wanataaluma wa Tz wana resist adaptively. Sio kweli kwamba wanahusuda vitambi bali hawapendi mambo wanayofanyiwa na wanasiasa bali wamechagua njia hiyo kupambana na wanasiasa. Mfano mzuri ni mgomo wa madaktari wa juzi. Kwa kuwa wanasiasa wanajiongezea posho za vikao kwa kazi nyepesi ya kuhudhuria tu kikao pengine bila hata mchango wowote wa maana, Madaktari nao wameamua kudai posho kwa kutumia taaluma yao ya udaktari pasipo kulazimika kuacha taaluma yao kama Dr Kigwangwala na Dr. Ndugulilei walioamua kuresist Adaptively. Madaktari waliogoma wanapinga unyanyasaji wa wanasiasa Actively.

  Waalimu wamejaribu kupinga, lakini wakashindwa, Maprofesa wamejaribu nao pia wameshindwa na sasa ni madaktari. Hawa angalao wamefanikiwa kunyamazisha harakati za wanasiasa kutaka kujilimbikizia malipo isivyohalali. Mapinduzi katika maisha ni jambo la kudumu kwa sababu ni kawaida kila aliyeoneka kuwa mtetezi wa wanyonge jana hubadilka na kuwa mkandamizaji wa walwale alioonekana kuwatetea jana. Na hivi ndivyo ilivyo kwa CCM ya sasa. Ukisema wanataka tu kushibisha matumbo yao, utakuwa umeangalia kwa jicho moja tu na kwa siku ya leo tu. Nakwambia mapambano ya wanasiasa na wanataaluma yatendelea mpaka kitaeleweka. Wanataaluma wanaoacha taaluma zao na kujisalimisha kwa wanasiasa ni wapambanaji waoga kama Maleale, lakini wanapambana.
   
 15. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Well presented
  Lakini kwa kule wanakotumia mawe kutengeneza bara bara huyu msomi ni far better n useful kuliko kandarasi aliye bungeni kujadili kodi ya maji ya chupa na thus msomi huyu kaendeleza alipoachia yule aliyewaachia barabara ya vumbi na mashimo

  Neno context kwenye uwasilishaji wako unalipa nafasi gani mkuu?
   
 16. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wamechoka kudanganywa wameamua na wao wakadanganye wananchi.
   
 17. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160

  Kaka you mean mtoto akionewa shule akirudi nyumabani ni sawa na yeye kuonea wadogo zake?????
   
 18. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mkuu unauliza jamvi msibani wakati walipo ndio walikotufikisha ebo uoni kuwa tumefika huku kwa sababu ya wasomi ambao walitakiwa wawe ndio wenye kutengeneza strategy za kuendesha uchumi na siasa matokeo yake wao ndio wamegeuka waendeshwaji na vidampa wasiojua dalasa ni nini?Toka lundo la wasomi lilipo jongea siasa Nchi imestuck hatuendi mbele tunajiona kama puto tunaelea tu.Ebu acha masihala kama uoni kuwa wasomi wametufikisha huku ilo nalo ni tatizo jingine kukaa chini kukuelimisha kuwa wanatumia elimu zao kumanipulate madhumuni ya wengi kuwa ya wachache kwa kutumia elimu zao,hau uoni wakisaini mikataba na kuongezeana posho,asingpiga kelele CDM kuhusu posho ingekuingia akilini kimya kimya wenzio wanapeta na GX mitaani.
   
 19. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,305
  Trophy Points: 280
  Waafrika hasa Watanzania ni maarufu sana kukosoa bila matendo. Hata Ulaya (kama ulikuwa hujui) bado barabara za mawe zinajengwa na kutumika hata leo. Japokuwa wewe unataka kutuonyesha jamaa wamefanya mambo ya kipuuzi sana lakini nadhani wametoa mchango mzuri. Ni juu wengine kuja na alternative kama wameona hayo hayafai...au?
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyo aliye bungeni ndiye anae mpangia cha kutumia yule aliye danganya watu kuwa yeye ndiye mvumbuzi wa barabara za mawe (zipo miaka zaidi ya 4000 kwa sasa duniani) Mitanzania ilivyo mijinga inashangilia.
  Hao ndio wasomi wa Tanzania, popote atapokuwepo hakuna afadhali.

  Our only solution, tukitaka tusitake ni kuwaacha hawa wazungu warudi, kama ilivyo sasa, ingawa wanarudi sehemu sehemu tu, inabidi tuwarudishe kote, tuanzie serikali za vijijini na wilayani, wawepo tu, uwepo wao tu tosha kabisa. Maana sisi tukiona Mzungu ni kama tumemuona mungu.
   
Loading...