Nini hatma ya CHADEMA endapo watashindwa uchaguzi?

Mbowe kabet kwa Lowassa this time,isipowork inabidi awajibike kwa uamuzi huo ambao umeibadili Chadema kuwa chama tofauti,badala ya kuwa kinara wa mapambano ya ufisadi Chadema imewakumbatia sasa mafisadi.

Ni ngumu kwa Mbowe kama mwenyekiti kuongoza tena Chama kitakachokemea ufisadi, ndio maana ni vyema kuja na timu mpya,Tindu Lissu na Mnyika wangefaa kuongoza timu hiyo.

Wazo zuri mkuu,kamari aliocheza mbowe ni ya hatari kubwa sana ingawa moja ya theory of distribution in economics inasema the higher the risk,the higher the returns.
 
nini hatma ya ccm na hizi tafiti zao zinapingwa kila kona na makundi hayo hayo waliotajwa kwenye tafiti zao kuwa wako pamoja ,uchaguzi utakapofanyika ibainike kura zao hazitoshi na wameshindwa itakuwaje ,wamejipanga kukabidhi kijiti bila purukushani

Kafungulie uzi wako mkuu.
 
Mnyika apewe uongozi, sio Tundu Lissu, Tundu Lissu ameonesha udhaifu wa hali ya juu kwa msomi kama yeye. Anakurupuka na anatoa majibu ya saluni za wanawake kwa maswali mazito. Amekula matapishi yake, ameonesha hana msimamo hata kwa body language. Mnyika ameonesha ukomavu fulani, body language ya Mnyika na Mdee speaks volumes. Mnyika wenye akili tumeona na tunajua kabisa kuwa hakubaliani na kinachoendelea na kilichotokea cha kuwapokea makapi na kuiweka kapuni chadema asili, ila kafanya yake kama mgombea ubunge, kanadiwa na Lowassa na kasema chagua Lowassa. HATUJAMUONA yule Mnyika machachari wa bungeni akiwa anamnadi Lowasa, (akili za kuambiwa changanya na zako hapa).

Uchambuzi wako ni very objective nimeukubali mkuu.:thumbup::thumbup::D
 
Yani kama ungekua umeongea kwanzia mwanzo kama ulivoandika hiyo para ya kwanza kusingetokea malumbano yoyote sababu ndio thread yangu inaongelea hvo.Na usifikiri mimi sitaki mabadiliko ni ngali sio mwanachama wa chama chochote yani kama wewe tu mkuu Kaptula la Marx

Ila kitu kingine,usitegemee siasa kwa 100% ikuletee madadiliko katika maisha yako.baadhi ya watu wanaona mabadiliko ni kwa wanasiasa na wanachadema tu sababu washawaona hao wenye political platform (ccm) wanafanya nini kwahyo wakiwapa wengine platform watafanya hivyo hivyo tu.

Ni kweli ulichosema mkuu. Lakini bado tunahitaji kuwaunga wanasiasa mkono. Hii ni kwa sbb uchaguzi mkuu ni njia mojawapo ya wananchi kufanya mabadiliko kwa kuchagua viongozi wanaowataka. Sasa kwa katiba yetu ya sasa hakuna wagombea huru, bali wagombea wa nafasi za kisiasa lazima wapatikane kupitia vyama vya siasa. Sasa kwa upande wa nchi yetu tuna CCM km chama tawala na kambi ya upinzani. Kwa hiyo, hatuna budi kuunga mkono kambi ya upinzani kwa ujumla wake; hata vilivyopo nje ya UKAWA.

Chadema mwaka huu imeshika usukani tu km ilivyowahi kufanya NCCR mwaka 1995; CUF mwaka 2000 na 2005; na CHADEMA ikaibuka 2010 na mwaka huu. Kwa hiyo, binafsi hata km CHADEMA itakufa nitaendelea kuunga mkono mabadiliko na nimeanza kufanya hivyo tangu mwaka 2010. Kabla ya hapo, uchaguzi mkuu wa 1995 hadi 2005 niliwaunga mkono CCM na nilichagua wagombea wake mara zote hizo. Lkn baada ya kuona hakuna mabadiliko yale niliyotarajia ikabidi nianze kuunga mkono kambi ya upinzani.

CHADEMA ikifa vyama vingine vitaibuka na vitachukua nafasi. Hiyo ndio kanuni ya historia. Hata CCM mwisho wake utafika tu itakufa km vyama vingine vilivyowahi kufa. Kitu kisichobadilika dunia hii ni mabadiliko tu, lkn vingine vyote vinabadilika. Binafsi sina tatizo na kufa kwa chama chochote cha siasa, iwe CUF, CHADEMA au CCM; vyama vitapita lakini nchi yetu Tanzania itabaki. Labda Tanzania ikifa ndio nitapata shida maana sitakuwa na kwa kwenda. Japo tukifika huko itakuwa ndio mwisho wa dunia labda
 
Last edited by a moderator:
Yaan wwe bukoba boy, ungepata wafuasi wakukusaidia kujibu maana . unauliza swali wakat unamajibu yako kichwan tukusaidiaje sasa.
 
Yaan wwe bukoba boy, ungepata wafuasi wakukusaidia kujibu maana . unauliza swali wakat unamajibu yako kichwan tukusaidiaje sasa.

Kwahyo wewe huna majibu yako na hoja zako kwenyewe ukazilinganisha na zangu.
 
Kumbe ningesema CUF itakufa

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom