Najua ulimanisha hivyo, lakini ninachokisema hiyo nguvu au mwamko upo kila uchaguzi. Kama ni tofauti imetokana na kutofautiana kwa nyakati na majira, na sio sababu ya Lowassa. Sasa hivi wananchi wengi wamechoka hicho chama chenu cha CCM ambacho kinaonekana sasa kimechoka. Watu wengi wanataka mabadiliko, basi. Kwa hiyo, kuhusisha nguvu au mwamko uliopo mwaka huu na Lowassa pekee ni upotoshaji mkuu. Kuna watu wengi tu ukiongea nao mitaani wanasema kabisa kuwa mwaka huu hata wakiweka jiwe wako tayari kulipigia kura lakini sio CCM. Hata ungegombea wewe kupitia CHADEMA / UKAWA, watu wangekupa kura
Pili, hiyo dhana ya wakishindwa ndio wanakufa haina ukweli wowote, ni dua la kuku halimpati mwewe. Pamoja na kwamba UKAWA sio chama cha siasa, lakini ni mmoja unaoundwa na vyama vya siasa. Sasa km wabunge wataongezeka na kuwa wengi bungeni, wewe unadhani hawatakuwa ni wabunge wa vyama hivyo vya siasa kwa sababu tu UKAWA sio chama? Mimi naamini CHADEMA, CUF watakuwa na wabunge wengi tu wa kutosha. Kadhalika, hata NCCR itapata Wabunge. Wote hao wataunda kambi ikiwa watashindwa uchaguzi kama unavyotaka wewe