Asante hivyo kutokana na aliyo yafanya NYERERE ataendelea kukumbukwa?βI learned that everyone dies alone. But if you meant something to someone, if you helped someone, or loved someone. If even a single person remembers you, then maybe you never really die. And maybe, this isnβt the end at all.β
Person of Interest - Quote by the Machine....
Nawaza ipo siku itajadiliwa na kusema inatia hasara Taifa hivyo ifutwe.Hii siku ni muhimu sana, lakini inakuwa ya kuliingiza taifa hasara ya matumizi ya fedha kutokana na ukweli kuwa siku hii imekuwa ya kutoa matamko tu ya kumenzi hayati Mwl Nyerere lakini ikipita tu, kila mtu anaendelea na mambo yake, hakuna vitendo!
Kwani kuuliza ni kosa lengo ni kujuaNyerere angekuwa anatoka kwenye ukoo wenu sidhani kama ungekuja na uzi kama
Mkuu hakuna kitu Cha faraja familia ya Nyerere inajivunia kama kuona anakumbukwa kama hivi, sasa unataka kuipoka faraja ya watu kwanini.
Alikataa mawazo mbadala ya kina kambona na mtei singerpore na Malaysia ilikuwa sawa na Tanzania kiuchumi 1960s lakini kutokana na Nyerere kujiona mungu mtu alikataa sera za nzuri za maendeleoTujuze mkuu kivipi?
Shukurani mkuu kwa maelezo yako nimepata kituAlikataa mawazo mbadala ya kina kambona na mtei singerpore na Malaysia ilikuwa sawa na Tanzania kiuchumi 1960s lakini kutokana na Nyerere kujiona mungu mtu alikataa sera za nzuri za maendeleo
Kwa kutuletea ujamaaTujuze mkuu kivi
Ni ukilaza/utahahira/upuuzi/wendawazimu/ufyatu wa hali ya juu kumchukia Nyerere eti ndie alileta umaskini.Alikataa mawazo mbadala ya kina kambona na mtei singerpore na Malaysia ilikuwa sawa na Tanzania kiuchumi 1960s lakini kutokana na Nyerere kujiona mungu mtu alikataa sera za nzuri za maendeleo
Shukurani mkuu kwa zege hiyoNi ukilaza/utahahira/upuuzi/wendawazimu/ufyatu wa hali ya juu kumchukia Nyerere eti ndie alileta umaskini.
Tangu ameondoka kiti cha urais kodi anakusanya yeye? Uchaguzi anachaguliwa yeye? Vyuo, bodi, wizara, majimbo, kamati anachagua na kuongoza yeye?
Bajeti ngapi zimepita tangu Nyerere ang'atuke. Nyerere kaongoza Tanzania kwa miaka pungufu ya miaka ambayo marais wengine waliofuata waliongoza. Wao walificha akili zao wapi kuifanya Tanzania tajiri na wakati ndio wamekuta resources nyingi zaidi yake? Kwahiyo tule kashata na kunywa kahawa tukimlaumu Nyerere, yeye mmoja kashindwa hao wengine wanne wamefanyaje?
Umaskini wetu unaletwa na Watanzania wengi kuwa wajinga. Mtu tangu 1985 sio Rais ila analaumiwa kwa umaskini, huwezi enda Ujerumani ukakuta wanajiliza wakimlaumu Adolf Hitler kwa kuwaingiza vitani na hasara kubwa waliyopata.
Mwalimu Nyerere ni underrated hasa na watu wake mwenyewe. Alikuwa na uwezo mkubwa kuliko waliofuata ndio maana vikojozi hadi leo wanalilia kwanini hakuwafanyia nchi tajiri. Kumbe ambacho Nyerere hakufanya hakuna mtu yeyote anaweza, hata katiba aliyoacha bado tunayo. Asingeacha multipartism tusingekuwa nayo