Nini hatima ya Madaktari? Je unawashahuri nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini hatima ya Madaktari? Je unawashahuri nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KakaKiiza, Jan 30, 2012.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Tumeona nakusikia tamko lakiongozi mkuu wa shughuli zote za utawala serikalini akitoa tamko je nini hatima ya madaktari?na mikutano yao imepigwa marufuku!je wewe unaona ninisuruhisho la mgogoro huu?je warudi makazini?au waendelee na msimamo wao?je wakirudi kazini watafanya kazi kwa upendo au nikusaini kitabu nakukaa bila kupiga round wodini?
   
 2. s

  sugi JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  waendelee tu na mgomo,maji ukiyavulia nguo,lazima uyaoge,wakaze buti,mkwara lazima uwepo,lakini haki inadaiwa na wakandamizawaji,kamwe haitolewi na mkandamizaji pasipo kuidai,tena kwa machozi
   
 3. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii imekaa vibaya nadhani watarudi wodini but sidhani kama watafanya kazi kwa moyo. Wasiwasi wangu ni kwa maskini mwagonjwa wetu. maana wanaweza wakagoma kimoyo.
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Madai yao ni mengi na mazito, na serikali WM ametumia ubabe kuwataarifu Sa 12 jioni kuwa kesho yake siku ya ibada wanapaswa kukutana naye sa 4 asubuh, alifanya hivyo akijua wazi kuwa madaktari watakataa ili yeye apate kuuhadaa umma kuwa madaktari ni wajeuri, yawezekana km busara ya kweli ingetumika kungekua na maelewano kati ya madaktari na serikali walipane japo nusu ya madai yao lakini serikali inafanya ubabe kwani inajua wazi kuwa imeishiwa na kike kidogo kilichobaki wanataka wakile wenydwe (posho za wabunge). Ombi langu kwa madaktari WAGOME WOTE ASIBAKI HATA MMOJA HOSP. naimani haki itapatikana ila wakijaribu kurudi kazini wajue serikali itawadharau na ni karne itaisha na hawatapewa haki yao. MSIRUDI NYUMA
   
 5. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,129
  Likes Received: 6,617
  Trophy Points: 280
  waendelee tu na mgomo,maji ukiyavulia nguo,lazima uyaoge,wakaze buti,mkwara lazima uwepo,lakini haki inadaiwa na wakandamizawaji,kamwe haitolewi na mkandamizaji pasipo kuidai,tena kwa machozi

  source: Sugi
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  ni hapo watakaporudi kazini halafu wasiattend wagonjwa, sijui itakuaje!!!!!!!!!!!
   
 7. d

  dmatemu JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 591
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 60
  Nadhan wakirud kazin watakuwa wamefanya jambo la busara sana. Wadai kwa njia ya majadiliano na si kugoma maana wagonjwa wanateseka sana na wengine wanakufa.
   
 8. S

  Shansila Senior Member

  #8
  Jan 30, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waendelee na mgomo,naamini madaktari hawakukurupuka kugoma,walijaribu kudai haki zao kwa njia ya mazungumzo lkn ikashindikana.Serikali hii si sikivu kama inavyojigamba,ni serikali kaidi na serikali inayoelekea kuanguka huwa na sifa ya ukaidi.
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [h=2]Pinda aagiza madaktari wakamatwe[/h]
  Awapiga marufuku kukusanyika
  [​IMG] Awataka warudi kazini au wafukuzwe
  [​IMG] Wenyewe wasema wanaenda mahakamani  [​IMG]
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wa 2 kulia), akitoa tamko la serikali jana kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, linalowataka madaktari walio kwenye mgomo wawe wamerudi kazini ifikapo leo vinginevyo wataachishwa kazi. Kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda. (PICHA: MPIGAPICHA WETU)


  Serikali imewageuzia kibao madaktari walioko kwenye mgomo baada ya kuwataka kuacha mara moja mgomo huo na kuripoti kazini leo na kuonya kuwa yeyote atakayeshindwa kufanya hivyo atakuwa amejifukuzisha kazi mwenyewe.

  Pia imeviagiza vyombo vya dola kuwashughulikia madaktari wote watakaofanya mkutano mahali popote kujadili mgogoro wa maslahi yao kwa vile mikutano hiyo ni kinyume cha sheria.

  Vile vile, imeiagiza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kupeleka madaktari wake katika hospitali za mkoa wa Dar es Salaam ili kusaidia wagonjwa walioko hospitalini, ambako imesema huduma zitaendelea kama kawaida.

  Agizo hilo lilitolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, jana alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, baada ya madaktari hao kukataa kukutana naye ili kupata suluhu ya mgogoro huo.

  Juzi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka, alithibitisha kupokea wito wa Waziri Mkuu wa kukutana na madaktari jana, lakini akasema ulichelewa kuwafikia.

  Alisema kutokana na hali hiyo wasingekuwa tayari kukutana naye jana, badala yake wangekutana leo na baadaye kufanya mikutano ya hadhara katika tarehe na mahali ambako wangepatangaza baadaye.

  "Kuanzia sasa serikali inawahimiza madaktari wote walio katika mgomo kuacha mara moja na kuripoti kazini ifikapo kesho (leo) asubuhi, Jumatatu tarehe 30 Januari, 2012. watakaoshindwa kufanya hivyo, watakuwa wamepoteza ajira zao," alisema Pinda.

  Aliongeza: "Mikutano (ya madaktari walioko kwenye mgomo) inayofanyika ni kinyume cha sheria. Hivyo, naviagiza vyombo vya dola tusiiruhusu. Hakuna (kukutana) Starlight, Don Bosco wala wapi," alisema Pinda.

  Mkutano huo wa jana ulihudhuriwa na mawaziri, Dk. Haji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii), George Mkuchika (Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-Tamisemi), Shamsi Vuai Nahodha (Mambo ya Ndani ya Nchi), Dk. Hussein Mwinyi (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa-JKT), Dk. Lucy Nkya (Naibu Waziri-Afya na Ustawi wa Jamii) na Hawa Ghasia (Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma).

  Wengine waliohudhuria ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime pamoja na maofisa wa wizara hiyo.

  Alisema mgomo unaofanywa na madaktari hao siyo halali kwa vile haukufuata taratibu za kuitisha mgomo.

  Pinda alisema madaktari walipaswa kutangaza mgogoro na kisha kutoa notisi ya siku 60, jambo ambalo alisema hawakulifanya.

  Alisema katika muda huo wa notisi wa siku 60, majadiliano yalitakiwa yawe yanaendelea ili kushughulikia madai yao.

  "Nawaomba sana mgomo ukome, tuache, maana ukiendelea watu wataumia. Tukiwaita kwenye vikao hawaji. Mwisho tutaonekana hatuna heshima. Kwa hiyo, kesho warudi kazini kama kawaida. Atakayeshindwa tutamhesabu si mtumishi," alisema Pinda.

  Alisema kwa uamuzi huo anajua serikali itapata changamoto, lakini akasema ni bora waendelee na changamoto hiyo kuliko iliyopo sasa ya wagonjwa kuendelea kuumia.

  Kutokana na hilo, aliitaka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kuandaa utaratibu wa kuwarudisha kazini madaktari wote walioko kwenye mgomo.

  Pia aliwataka wakuu wa mikoa na hopsitali zote kufuatilia kwa karibu zaidi kuona madaktari walioko kwenye mgomo kama wataendelea kutoa huduma leo.

  Alisema katika hatua iliyofikiwa, serikali imetambua kwamba madaktari wanaoongozwa na Kamati ya Mpito, hawataki suluhu licha ya juhudi zote ambazo zimefanywa za kuwaita ili kushughulikia madai yao.

  Waziri Mkuu alisema serikali imebaini pia kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk. Stephen Ulimboka siyo mtumishi wa serikali na wala hajasajiliwa kama daktari.

  KUHUSU DK. ULIMBOKA

  Pinda alisema Dk. Ulimboka alihitimu Shahada ya Udaktari (MD) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 2004, alipata usajili wa muda wa Baraza la Madaktari mwaka huo huo na kupangiwa internship katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

  Alisema Novemba 2005 aliongoza mgomo wa madaktari nchini na usajili wake ulisitishwa na Baraza hilo.

  Pinda alisema alishtakiwa mbele ya baraza hilo kwa ukiukwaji wa maadili ya taaluma ya udaktari kwa kuitisha na kufanya mgomo ambayo ni makosa ya kimaadili katika taaluma hiyo.

  Alikataa kufika mbele ya baraza kujibu tuhuma zilizokuwa zinamkabili na hivyo, shauri lake halikumalizika.

  Alisema Julai 2006, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alimsamehe na hivyo kurejeshewa usajili na baraza na kuruhusiwa kuendelea na internship.

  Pinda alisema katika kumpa taarifa za msamaha wa Rais, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Baraza la Madaktari kwa nyakati tofauti walimtaka Dk. Ulimboka kutojihusisha na mgomo au suala lolote ambalo ni kinyume cha maadili ya taaluma ya udaktari.

  Alisema Dk. Ulimboka kupitia barua yake kwa baraza ya Februari 2, 2007, alikiri kwamba hatajihusisha wala kutoa ushawishi wowote kwa wengine kufanya vitendo ambavyo ni kinyume cha maadili ya udaktari.

  "Hadi sasa hakuna taarifa kama alimaliza internship kwa kuwa hajawasilisha cheti cha kumaliza mazoezi hayo na hakuna taarifa juu ya mahali anapofanyia kazi. Aidha, Dk. Ulimboka siyo mtumishi wa serikali na wala hajasajiliwa kama daktari," alisema Pinda.

  MADAI YA MADAKTARI

  Waziri Mkuu alisema kulikuwa na mawasiliano kati ya ofisi ya Waziri Mkuu na uongozi wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) na baadaye mwenyekiti wa muda wa kamati ya mpato ya madaktari kuhusu mgomo wa madaktari.

  Alisema katika barua yao ya Januari 27, mwaka huu, walitoa madai manane; ikiwamo posho ya kulala kazini, posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi, posho ya nyumba, posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu, kupatiwa posho ya usafiri, nyongeza ya mshahara, kupatiwa huduma ya bima ya afya na kutaka wenzao warudishwe Muhimbili.

  Pinda alisema madaktari hao wanadai mshahara wa Sh. 700,000 kwa daktari anayeanza kazi ni mdogo sana, hivyo wanapendekeza alipwe Sh. milioni 3.5 kwa mwezi.

  Alisema wakati madaktari hao wakipendekeza kwamba madaktari wanaoajiriwa hivi sasa walipwe kiasi hicho cha mshahara, madaktari wapya wanaoajiriwa wanalipwa Sh. 957,700 wakati watumishi wa kada nyingine kama wahandisi wanaanza na Sh. 600,000, wahasibu kati ya Sh. 300,000 hadi 400,000.

  Pinda alisema posho zote wanazodai madaktari zikijumuishwa zinafikia asilimia 120 ya mshahara wa daktari mmoja.

  Alisema ili kuhakikisha kunakuwa na hali ya utulivu katika mazingira ya kazi, utekelezaji wa pendekezo la madaktari la kulipa mshahara wa Sh. milioni 3.5, kwa mwezi kwa daktari atakayeanza kazi, utailazimu serikali kurekebisha viwango vya mishahara kwa watumishi wote wa kada za afya pamoja na kada nyingine ili kuweka uwiano kufuatana na stahiki za miundo katika utumishi wa umma.

  Pinda alisema kwa mujibu wa mapendezo yao, ina maana kwamba kiwango cha kuanzia mshahara kwa mhudumu wa afya kitakuwa Sh. 670,316 na mshahara wa juu kwa kada za afya utakuwa Sh. 8,145,573 kwa mwezi.

  Alisema utekelezaji wa pendekezo hili utagharimu jumla ya Sh. 83,508,834,430 kwa mwezi ambayo ni sawa na Sh. 417,544,172,150 kwa kipindi kilichobaki cha miezi mitano na kwamba, kiasi hicho ni sawa na nyongeza ya Sh. 301,730,372,400 katika bajeti ya mshahara kwa mwaka 2011/2012.

  Pinda alisema kwa mujibu wa mapendekezo ya madaktari ya mshahara pamoja na posho mbalimbali itamaanisha daktari anayeanza kazi atapata jumla ya Sh. milioni 7.7 kwa mwezi ikijumuisha mshahara na posho nyingine.

  Alisema pia kwa mujibu wa mapendekezo hayo, daktari mshauri mwandamizi atapata Sh. 17,231,020 kwa mwezi na kwamba, kwa kuzingatia ukubwa wa gharama hizo utekelezaji wa mapendekezo ya madaktari utakuwa hauwezekani kwa kuzingatia hali halisi ya bajeti ya serikali.

  Alisema endapo serikali itatekeleza madai yao kwa mwaka mmoja, jumla ya mishahara yao itakuwa ni Sh 799,692,615,592 badala ya Sh. 222,214,936,800 za sasa hadi kufikia Juni, mwaka huu.

  Waziri Mkuu alisema madaktari hao wanadai kwamba watumishi wa kada nyingine za afya wapandishiwe mishahara na posho kama zao na kwamba, endapo watapewa fedha wanazodai, serikali itapaswa kulipa Sh. 202,413,397,568 na kama madai yao yatatimizwa kwa miezi mitano iliyobaki, watapaswa kulipwa Sh. 84,338,915,653.

  Alisema katika makundi hayo mawili tu, nyongeza yao ya mishahara ni sawa na Sh. 1,002,106,013,160 kwa mwaka.

  Pinda alisema ukijumuisha na nyongeza ya posho zao wanazodai za Sh. 1,037,184,854,550 unapata Sh. 2,039,290,867,710, ambayo ni sawa na theluthi mbili ya mishahara ya wafanyakazi wote serikalini ambayo kwa sasa ni Sh. trilioni 3.45.

  "Hii maana yake ni kwamba kiasi kinachobaki cha theluthi moja ndicho kigawanywe kwa watumishi wengine," alisema Pinda.

  MADAI YA KUTAKA WATENDAJI WAKUU WAJIUZULU

  Pinda alisema madai mengine ya madaktari hao, wanataka Dk. Mponda, Naibu wake, Dk. Nkya, Katibu Mkuu, Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mtasiwa wajiuzulu kwa madai ya kuzembea madai yao.

  Hata hivyo, alisema iwapo hoja ni hiyo, hakuna anayeweza kubaki serikalini kwa vile wao ndio wako jikoni wanaona ugumu wa utekelezaji wa madai yao.

  Alisema kumuondoa waziri kuna sababu zake na kuhoji: "Hivi nijiuzulu kwa sababu ya kusema ukweli? Nitakwambia sijiuzulu. Labda kama kuna jambo lingine."

  HALI ILIVYO KATIKA HOSPITALI

  Waziri Mkuu alisema tangu mgomo uanze, serikali imekuwa ikifuatilia na kupokea taarifa za mgomo huo kutoka mikoa yote na kwamba, mpaka Januari 28, mwaka huu, mikoa 21 ilikuwa imewasilisha taarifa za awali juu ya hali ya mgomo huo.

  Aliitaja mikoa ambayo hospitali zake zote za mikoa na wilaya hazina mgomo kabisa kuwa ni Ruvuma, Lindi, Mtwara, Shinyanga, Arusha, Tabora, Kagera, Iringa, Mara, Pwani, Kigoma, Singida, Manyara na Rukwa.

  Aliitaja mikoa ambayo hospitali zake za mikoa (isipokuwa za wilaya) zimekuwa katika mgomo kuwa ni Kilimanjaro, Mbeya, Mwanza, Morogoro, Tanga, Dodoma na Dar es Salaam, mbako ndiko ulikoanzia.  CHANZO: NIPASHE
   
 10. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Hakuna chenye mwanzo kikakosa mwisho ila kwahili madaktari wana haki ila njia wanayoitumia serikali itawabana kwaani kanuni za utumishi wa umma mtumishi wauma hatakiwi kugoma!
   
 11. d

  dkn Senior Member

  #11
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  waache kugoma madai yao yafanyiwe kazi wakiwa kazini na wapeane timeline kati yao na serikali ili wagonjwa watanzania wenzetu wapate huduma.
   
 12. D

  DrT Member

  #12
  Jan 30, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Binafsi,kama ningekuwa Tz,ningeomba kuacha kazi,aidha nikaomba katika private sector au nikajiajiri kuliko kubeba lawama ya kutohudumia wagonjwa ambao kimsingi ni haki yao na ndo mwajiri wangu kupitia serikali kama msimamizi.

  Wito wangu kwa madaktari na serikali ni kuwa wajaribu kutafuta balancing point ili kuokoa madhara yanayotokana na mgomo,hakuna haja ya kutunishiana misuli wakati watu wanakufa/wanaumia.

  Pia tujitahidi tusifanye profession zetu kuwa direct source ya gharama za maisha yetu,bali iwe ni source ya ideas to create businesses ili tusiwe watumwa wa pesa bali pesa itutumikie.

  Kwa mfano,Bill Gates,computer programming ,his profession,sio direct source ya maisha yake,bali ideas from that zime create businesses ambazo zimemfanya kutokuwa mtumwa wa pesa.(just an example from a big man,it doesnt mean it's for some special people only)

  Kama daktari,kila siku una attend wagonjwa,fanya surgeries etc you must come out with something new,sorta innovation from which business could be created.Kwa mfano,some one has come with idea that shark's skin is not harbored by bacteria,thereafter wanaangalia possibility of how to make use of it in preventing nosocomial diseases.

  Kuna idea kama ya kukusanya nguvu na kuanza na modern lab,ambayo itakuwa for both:as the source of money as well as a research center from which creativity inaanza.Things like biochem labs,urinalysis,blood analysis equips dont cost much but are not available in many regions in Tz,u take that advantage for the long term vision.

  Tufanye collaboration with other expertise in our field to create businesses na sio kuishia kula CCD pekee.Even idea on how improve malaria diagnosis would be a great deal.
   
 13. T

  Topical JF-Expert Member

  #13
  Jan 30, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nawashauri waandike mradi wa hospitali kubwa Dar, wachukue pesa bank wajenge hospitali yao (wao wenyewe ndio owners) wanajilipa wapendavyo..
   
Loading...