Nini hatima ya jina Airtel iwapo TTCL itaichukua Kampuni hiyo?

Nimekuwa na shauku ya kujua nini kitafanyika kuhusiana na jina la sasa la 'Airtel'..kwamba itakapotokea TTCL imeichukua kampuni hiyo, je, jina litaendelea kuwa lilelile au litabadilishwa? Ifahamike, jina la Airtel linatokea na lina asili ya India.

Je, wafanyakazi wanaotumikia idara ya huduma kwa wateja 'call center' ya Airtel na ambao wapo chini ya kampuni ya uwakala wa ajira (outsourcing company) inayoitwa ISON BPO, nao hatima yao itakuaje?---Keep in mind, wafanyakazi wote wa idara ya huduma kwa wateja wote wanaohudumia wateja wa Airtel hawana mkataba wa ajira na Airtel, bali wana mkataba na kampuni hiyo ya uwakala wa ajira, inayoitwa ISON BPO. Kadhalika ISON BPO asili yake ni India.
Kitakachotokea ni kwa airtel kuachia kiasi kadhaa cha hisa (btn 10% and 30%)ambazo zitaipa serikali share kubwa >50.Kumbuka serikali ina 40% share ktk airtel. So ikishapata hizo share serikali itakuwa na uwezo Wa maamuzi au inaweza kumlipa bhati airtel kiasi cha share kilichobaki na kuimiliki 100% airtel.This is my prediction.
 
Mnajua haya mambo yanachosha akili!

Ni kweli rasimali zetu zimeibwa sana

Kila mtu anatamani kila kilichoibwa kirejeshwe ili kitunafaishe sote

Lakini hao walioiba hawakua zero brain, ni majitu yenye akili yakatumia udhaifu wa watu tuliowapa dhamana kutuibia.

Katika mazingira kama hayo unaanzia wapi kurejesha mali zako? Sio kwa matamko na mbwembwe, lazima ujipange na uone kama utaweza ili usije ukaingia aibu.

Ni kiongozi gani atakaethubutu kufukua madudu yote ya nyuma na kuanza kuchukua hatua?

Tume ya makinia ilikuja kwa mbwembwe na kutangaza majina ya wahusika waliotutia hasara ikapendekeza hatua stahiki zichukuliwe! Hebu tuanzie hapo, NI NANI ALIYECHUKULIWA HATUA kati ya wale waliotajwa pale?

Mara injini za treni
Mara magari
Mara trailers zimekamatwa

Leo unaambiwa Airtel ni mali ya TTCL na watu wamekodoa macho wanasubiri.

Mungu atusaidie.
 
Back
Top Bottom