Nini hasa tatizo la Spika Ndugai wa Bunge letu?

Tatizo la Ndugai anafanya kazi kama Mwigizaji aliye live jukwaani ambae lengo lake ni moja tu: Kuifurahisha hadhira!

Ndugai nae yupo jukwaani huku akili yake ikimweleza hadhira yake ni Magufuli, na kwahiyo lengo lake ni moja tu: Kumfurahisha Magufuli.

Na amini amini nawaambia! Usikute ka Ndugai na kenyewe kana tamaa ya Urais! Na hili kufanikisha lazima awe anajikomba komba kwa Rais!

Na amini amini nawaambia... Usikute Magu nae keshamjaza ujinga Ndugai kwamba hakuna yeyote anayemuamini kudumisha ndoto yake ya Dodoma kuendelea kuwa HQ ya nchi hata baada ya yeye kuondoka madarakani zaidi ya wewe (Ndugai).
Hivi Dodoma kutokuwa HQ ya nchi inamuumiza sana Magufuli?
 
Ameanza kuwatuhumu wapinzani kuwa wameiba pesa za umma. Mbona hakusema mwanzo? Anaanza kuwaamuru warudi bungeni au warudishe posho zao.
Haka ka mchezo nilikuwana nako Primary, demu akinikataa tu namwambia anirudishie kila kitu nilichomhonga, afu namwandikia barua kali ya kumtukana saana !! kuna siku niliwahi kurudishiwa hadi .... ya ndani. (teh teh teh)

Sasa kwetu sisi haya yaliishia shule ya msingi, ukubwani sisi ni waugwana yakhe!! masuala ya kuitana Mwizi, Kibaka, kubebana kwa tanganyika jeki, kukamatwa kama chagudoa nk haya ni madhaifu!!
 
Wameanza kuivunja tangu 2015 na wameahaona hatuchukui hatua ndiyo maana sasa wamekomaza kiburi na kushupaza shingo zao.Fikiria mbunge Mwambe alijivua nyadhifa zake zote CHADEMA ikiwa ni pamoja na ubunge,akajiunga na CCM,leo kaitwa kurudi Bungeni na Watanzania wapi kimya,Wabunge wa CCM wanamshangilia na anapokelewa kishujaa bungeni.
CCM na viongozi wake ni janga LA Taifa letu.
 
Ndugai alikuwa na Audit Query ya matumizi mabaya ya fedha kwenye Audit report ya 2016/17. Kama unakumbuka allazwa Hospitali ya India na kutumia Bilions kwa kuwa alikwenda na familia, nurse na mpambe tofauti na sera inataka aende na msindikizaji mmoja.

Aliporudi utakumbuka alitaka kumtunishia kidogo Jiwe kwa kumtetea Zitto Kabwe alipotaka kushikwa ndani ya Bunge. Na kwa kweli alikuwa na nia ya kutaka kusimama kama Spika Huru na Mhimili wake. Jiwe akamtishia kupitia watu wa Usalama kwa kunmuambia akiendelea kupishana naye basi atazianika kashfa zake zilizoibuliwa na CAG. Nakwamba ifikapo 2020 hawatampitisha kuwa Sipka wa Bunge instead watampitisha Tulia Ackson.

Basi baada ya hapo ikabidi asalimu amri na kuanza kumunga mkono.
Na huyo kwenye avatar yako aliishia wapi? Au alibadirisha sare siku ile ile
 
Wameanza kuivunja tangu 2015 na wameahaona hatuchukui hatua ndiyo maana sasa wamekomaza kiburi na kushupaza shingo zao.Fikiria mbunge Mwambe alijivua nyadhifa zake zote CDM ikiwa ni pamoja na ubunge,akajiunga na CCM,leo kaitwa kurudi Bungeni na Watanzania wapi kimya,Wabunge wa CCM wanamshangilia na anapokelewa kishujaa bungeni.
CCM na viongozi wake ni janga LA Taifa letu.
M hata cjui hii nchi inapelekwa wapi...ver sad!
 
YANI SPIKA ANAFIKIRIA KUWAKATA MISHAHARA WATU WALIOJIKINGA NA KORONA KWA SIKU 14, HALAFU HAPO HAPO ANAMWITA MBUNGE MWAMBE NA KUSEMA ANASTAHILI KULIPWA KILA KITU.
JE MWAMBE AMEKOSA VIKAO VINGAPI VYA BUNGE? MBONA YEYE HAKATWI POSHO?
 
Spika anasema katibu WA chadema alimpelekea tu barua ya kumwelezea kua MWAMBE sio Mbunge Tena wa chadema bila kuambatanisha barua ya MWAMBE, Hivyo hawezi kumchukukulia hatua MWAMBE.

Sasa cha kujiuliza, mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na IBRAHIM LIPUMBA Spika alitambua barua ya LIPUMBA? Na japo wabunge wale wa cuf walikimbilia mahakamani lakini haraka haraka mbona spika aliwaondoa bungeni?
 
(Copied from somewhere)

TATIZO LA NDUGAI NI LIPI?

Kama ukimuuliza Mtanzania yeyote wa kawaida sana juu ya tatizo la spika wa bunge letu tukufu ni vigumu kupata majibu sahihi. Job Ndugai amekuwa mtu wa kubadilika badilika sana kulingana na nyakati. Wapinzani naona sasa walishamjua na wakipiga ngoma lazima akate mauno. Wanamchezesha kwa tune wanayotaka wao. Wanaujua udhaifu wake vilivyo. Ni vigumu kujua kama spika huyu amekuwa naibu spika wa bunge letu chini ya maspika mahiri kama Samwel Sitta (marehemu) na mama Anne Makinda. Alipikwaje? Aliokwa, alikaangwa au alipikwa mchemsho? Hivi anaamini Watanzania wanamwelewa?

Anafikiri Tanzania ya leo ni ile ya akina Pius Msekwa? Hajui kuna matoleo ya miaka minne mtaani ya wahitimu mtaani wenye weledi sana na hawana ajira? Ni wasomi pamoja na wadogo zao na wazazi wao na wanamchora tu? Kwa sasa Watanzania hata hawahitaji runinga ili kujua yanayoendelea. Kabla hajasema maneno yake, tayari wameelewa kuwa anatumika. Tatizo kubwa la Ndugai ni udhaifu! Niliwahi kuandika makala na ikachapishwa kupitia gazeti la Tanzania Daima toleo na. 5147 la aprili 17/2019.

Hivi wapinzani ndio tatizo la nchi hii? Wamekwamisha nini ambacho ni chema? Kwa nn tusiwaapuuze na kufanya mema kufuatana na ilani ya chama cha mapinduzi? Mbona huku mtandaoni MATAGA wanatangaza kuwa CHADEMA na upinzani umekufa Tanzania? Kwa nini kuhangaika na vilivyokufa? Unawezaje kuhangaika na marehemu au ndio kujitoa ufahamu? Mimi naona upinzani una nguvu sana kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote ule. Badala ya serikali kupambana na maadui wa taifa letu sasa kila kukicha ni kuwasakama wapinzani. Tumezalisha kundi la wajinga ambao kucha kutwa ni kusifia tu bila kufikiri.

Wapinzani wameamua kuaondoka bungeni kwa amani kabisa na sababu wamezitoa. Kubwa ni kujitenga ili kujiepusha na corona. Hii imekuja baada wenzao kuambukizwa ugonjwa huo. Wamejipa siku 14. Ndugai kama spika mwanzo alijifaragua kuwa hatishwi na misimamo ya CHADEMA! Akadai anaendeleà na vikao vya bajeti. Hakuna mbunge wa upinzani alijibu. Walinyamaza kwa sababu wanamjua. Baada ya muda mfupi tu Ndugai amegeuka tena. Na huu ndio udhaifu!

Ameanza kuwatuhumu wapinzani kuwa wameiba pesa za umma. Mbona hakusema mwanzo? Anaanza kuwaamuru warudi bungeni au warudishe posho zao. Naamini kuna taratibu za malipo ya Wabunge ambazo Ndugai hajatwambia. Atwambie yote ili tuwazomee hawa wabunge. Amesema ni wazururaji. Tayari kila mtu ndani ya serikali kuanzia juu mpaka chini wamepoteana. Kila mtu anasema lake. I am sure wapinzani wanawajua ccm vizuri sana kuliko hata wao wanavyojijua.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, ndugu Paul Makonda naye ameingizwa ngomani. Anawataka watoke nyumbani kwake. Hapa hata hajasoma katiba inasemaje kuhusu maisha ya Watanzania na wanapaswa kuishi wapi. Hapo kwa kuwa wapinzani wanajua katiba sawasawa, wamemunanga vilivyo! Yote haya ni udhaifu wa bunge.

Acheni wapinzani wakae karantini popote ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Na ninyi endeleeni na vikao huko, naona Ndugai ameanza kuokoteza hata wabunge waliohama vyama vyao kwa hiari yao wenyewe. Kama hujui, Mwambe aliyehama CHADEMA bila kufukuzwa ameambiwa arudi bungeni. Sasa swali ni anarudi kwa tiketi ya chama gani?

Wonders will never end in this country.
Uingiaji wa tundu la sindano Madam nae yupo speed kutaka kiti atafanyaje sasa kujilinda kwenye silaha ya maangamizi wakiamua wameamua! Confuser
 
Ana hasira ambayo haina maelezo,ni vigumu kulijua tatizo lake.
 
Back
Top Bottom