Nini hasa tatizo la Spika Ndugai wa Bunge letu?

Kwa kuchapi chapi hayo maneno yako yamenikumbusha show moja ya luninga ambapo mkuu wa kitengo aliugua, akapewa kipaumbele kwenye madawa ambayo yalikuwa yanalipiwa na kundi la watu wenye kuhodhi nguvu za dola na uchumi, basi kila wakati akigoma au kuwachelesha kwenye mitikasi yao, nao wanachelewesha matibabu au dawa...sidhani kama hii ndicho kinachoendelea, lakini mkumbuke baada ya kupigwa marufuku kwa matibabu ya wakulu nje ya nchi, au sijui ilikuwa kabla maana sikumbuki vizuri, huyu spika alikuwa magazetini kila kukicha wakati anafarijiwa baada ya kurudi kutoka kwenye matibabu. Sasa sijui kama kuna ukweli na ninayoyasoma au ndio kama tu watu waonavyo kama
huyu ndugu yetu anaburuzwa...
Kaazi kweli kweli
 
(Copied from somewhere)

TATIZO LA NDUGAI NI LIPI?

Kama ukimuuliza Mtanzania yeyote wa kawaida sana juu ya tatizo la spika wa bunge letu tukufu ni vigumu kupata majibu sahihi. Job Ndugai amekuwa mtu wa kubadilika badilika sana kulingana na nyakati. Wapinzani naona sasa walishamjua na wakipiga ngoma lazima akate mauno. Wanamchezesha kwa tune wanayotaka wao. Wanaujua udhaifu wake vilivyo. Ni vigumu kujua kama spika huyu amekuwa naibu spika wa bunge letu chini ya maspika mahiri kama Samwel Sitta (marehemu) na mama Anne Makinda. Alipikwaje? Aliokwa, alikaangwa au alipikwa mchemsho? Hivi anaamini Watanzania wanamwelewa?

Anafikiri Tanzania ya leo ni ile ya akina Pius Msekwa? Hajui kuna matoleo ya miaka minne mtaani ya wahitimu mtaani wenye weledi sana na hawana ajira? Ni wasomi pamoja na wadogo zao na wazazi wao na wanamchora tu? Kwa sasa Watanzania hata hawahitaji runinga ili kujua yanayoendelea. Kabla hajasema maneno yake, tayari wameelewa kuwa anatumika. Tatizo kubwa la Ndugai ni udhaifu! Niliwahi kuandika makala na ikachapishwa kupitia gazeti la Tanzania Daima toleo na. 5147 la aprili 17/2019.

Hivi wapinzani ndio tatizo la nchi hii? Wamekwamisha nini ambacho ni chema? Kwa nn tusiwaapuuze na kufanya mema kufuatana na ilani ya chama cha mapinduzi? Mbona huku mtandaoni MATAGA wanatangaza kuwa CHADEMA na upinzani umekufa Tanzania? Kwa nini kuhangaika na vilivyokufa? Unawezaje kuhangaika na marehemu au ndio kujitoa ufahamu? Mimi naona upinzani una nguvu sana kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote ule. Badala ya serikali kupambana na maadui wa taifa letu sasa kila kukicha ni kuwasakama wapinzani. Tumezalisha kundi la wajinga ambao kucha kutwa ni kusifia tu bila kufikiri.

Wapinzani wameamua kuaondoka bungeni kwa amani kabisa na sababu wamezitoa. Kubwa ni kujitenga ili kujiepusha na corona. Hii imekuja baada wenzao kuambukizwa ugonjwa huo. Wamejipa siku 14. Ndugai kama spika mwanzo alijifaragua kuwa hatishwi na misimamo ya CHADEMA! Akadai anaendeleà na vikao vya bajeti. Hakuna mbunge wa upinzani alijibu. Walinyamaza kwa sababu wanamjua. Baada ya muda mfupi tu Ndugai amegeuka tena. Na huu ndio udhaifu!

Ameanza kuwatuhumu wapinzani kuwa wameiba pesa za umma. Mbona hakusema mwanzo? Anaanza kuwaamuru warudi bungeni au warudishe posho zao. Naamini kuna taratibu za malipo ya Wabunge ambazo Ndugai hajatwambia. Atwambie yote ili tuwazomee hawa wabunge. Amesema ni wazururaji. Tayari kila mtu ndani ya serikali kuanzia juu mpaka chini wamepoteana. Kila mtu anasema lake. I am sure wapinzani wanawajua ccm vizuri sana kuliko hata wao wanavyojijua.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, ndugu Paul Makonda naye ameingizwa ngomani. Anawataka watoke nyumbani kwake. Hapa hata hajasoma katiba inasemaje kuhusu maisha ya Watanzania na wanapaswa kuishi wapi. Hapo kwa kuwa wapinzani wanajua katiba sawasawa, wamemunanga vilivyo! Yote haya ni udhaifu wa bunge.

Acheni wapinzani wakae karantini popote ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Na ninyi endeleeni na vikao huko, naona Ndugai ameanza kuokoteza hata wabunge waliohama vyama vyao kwa hiari yao wenyewe. Kama hujui, Mwambe aliyehama CHADEMA bila kufukuzwa ameambiwa arudi bungeni. Sasa swali ni anarudi kwa tiketi ya chama gani?

Wonders will never end in this country.
Spika inaonekana wadudu wamepamba moto kichwani. Kila akikaa akilala akiamka anawawaza Chadema tu
 
Wameanza kuivunja tangu 2015 na wameahaona hatuchukui hatua ndiyo maana sasa wamekomaza kiburi na kushupaza shingo zao.Fikiria mbunge Mwambe alijivua nyadhifa zake zote CDM ikiwa ni pamoja na ubunge,akajiunga na CCM,leo kaitwa kurudi Bungeni na Watanzania wapi kimya,Wabunge wa CCM wanamshangilia na anapokelewa kishujaa bungeni.
CCM na viongozi wake ni janga LA Taifa letu.
Dharau kubwa sn kwa wananchi
 
"I fear the Government more than i fear terrorism" ...By Richard Jewell
 
(Copied from somewhere)

TATIZO LA NDUGAI NI LIPI?

Kama ukimuuliza Mtanzania yeyote wa kawaida sana juu ya tatizo la spika wa bunge letu tukufu ni vigumu kupata majibu sahihi. Job Ndugai amekuwa mtu wa kubadilika badilika sana kulingana na nyakati. Wapinzani naona sasa walishamjua na wakipiga ngoma lazima akate mauno. Wanamchezesha kwa tune wanayotaka wao. Wanaujua udhaifu wake vilivyo. Ni vigumu kujua kama spika huyu amekuwa naibu spika wa bunge letu chini ya maspika mahiri kama Samwel Sitta (marehemu) na mama Anne Makinda. Alipikwaje? Aliokwa, alikaangwa au alipikwa mchemsho? Hivi anaamini Watanzania wanamwelewa?

Anafikiri Tanzania ya leo ni ile ya akina Pius Msekwa? Hajui kuna matoleo ya miaka minne mtaani ya wahitimu mtaani wenye weledi sana na hawana ajira? Ni wasomi pamoja na wadogo zao na wazazi wao na wanamchora tu? Kwa sasa Watanzania hata hawahitaji runinga ili kujua yanayoendelea. Kabla hajasema maneno yake, tayari wameelewa kuwa anatumika. Tatizo kubwa la Ndugai ni udhaifu! Niliwahi kuandika makala na ikachapishwa kupitia gazeti la Tanzania Daima toleo na. 5147 la aprili 17/2019.

Hivi wapinzani ndio tatizo la nchi hii? Wamekwamisha nini ambacho ni chema? Kwa nn tusiwaapuuze na kufanya mema kufuatana na ilani ya chama cha mapinduzi? Mbona huku mtandaoni MATAGA wanatangaza kuwa CHADEMA na upinzani umekufa Tanzania? Kwa nini kuhangaika na vilivyokufa? Unawezaje kuhangaika na marehemu au ndio kujitoa ufahamu? Mimi naona upinzani una nguvu sana kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote ule. Badala ya serikali kupambana na maadui wa taifa letu sasa kila kukicha ni kuwasakama wapinzani. Tumezalisha kundi la wajinga ambao kucha kutwa ni kusifia tu bila kufikiri.

Wapinzani wameamua kuaondoka bungeni kwa amani kabisa na sababu wamezitoa. Kubwa ni kujitenga ili kujiepusha na corona. Hii imekuja baada wenzao kuambukizwa ugonjwa huo. Wamejipa siku 14. Ndugai kama spika mwanzo alijifaragua kuwa hatishwi na misimamo ya CHADEMA! Akadai anaendeleà na vikao vya bajeti. Hakuna mbunge wa upinzani alijibu. Walinyamaza kwa sababu wanamjua. Baada ya muda mfupi tu Ndugai amegeuka tena. Na huu ndio udhaifu!

Ameanza kuwatuhumu wapinzani kuwa wameiba pesa za umma. Mbona hakusema mwanzo? Anaanza kuwaamuru warudi bungeni au warudishe posho zao. Naamini kuna taratibu za malipo ya Wabunge ambazo Ndugai hajatwambia. Atwambie yote ili tuwazomee hawa wabunge. Amesema ni wazururaji. Tayari kila mtu ndani ya serikali kuanzia juu mpaka chini wamepoteana. Kila mtu anasema lake. I am sure wapinzani wanawajua ccm vizuri sana kuliko hata wao wanavyojijua.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, ndugu Paul Makonda naye ameingizwa ngomani. Anawataka watoke nyumbani kwake. Hapa hata hajasoma katiba inasemaje kuhusu maisha ya Watanzania na wanapaswa kuishi wapi. Hapo kwa kuwa wapinzani wanajua katiba sawasawa, wamemunanga vilivyo! Yote haya ni udhaifu wa bunge.

Acheni wapinzani wakae karantini popote ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Na ninyi endeleeni na vikao huko, naona Ndugai ameanza kuokoteza hata wabunge waliohama vyama vyao kwa hiari yao wenyewe. Kama hujui, Mwambe aliyehama CHADEMA bila kufukuzwa ameambiwa arudi bungeni. Sasa swali ni anarudi kwa tiketi ya chama gani?

Wonders will never end in this country.
Mpumbavu na lofa unaachana naye.

Mjinga anaisidiwa kuondokana na ujinga kwa mafunzo ya maneno na vitendo.

Jeuri anashikishwa adabu kwa kutumia sheria, kanuni na taratibu.

Wapinzani wako katika makundi hayo. Kwa kuwa Spika ameshika mpini, han budi kutumia vyema madaraka yake kama silaha.
 
Huyu mbunge aliehama chadema na kuhamia CCM.. jee aliandika barua rasmi na kukitaarifu chama chake kwamba anajiuzulu nafasi zote na kukihama chama? Au alimwandikia barua rasmi spika juu ya huo uamuzi wake? Naomba kujuwa kuiyambia Tz kuwa nahama chama na kuhamia chama chengine kwa kutumia mass media inatosha bila kuandika barua rasmi?
 
Spika atayauliza hayo mahakamani. Kupelekwa mahakamani kwa kiongozi aliyeapa kulinda katiba na kuivunja hakuna tofauti na mwanamke mwenye kiapo cha ndoa akazini. Niaibu kubwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu haya mambo.hayafanywi kwa bahati mbaya ,Hawa viumbe wapo tayari kufanya lolote wanalojickia kinga ipo
Spika anasema katibu WA chadema alimpelekea tu barua ya kumwelezea kua MWAMBE sio Mbunge Tena wa chadema bila kuambatanisha barua ya MWAMBE, Hivyo hawezi kumchukukulia hatua MWAMBE.
Sasa cha kujiuliza, mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na IBRAHIM LIPUMBA Spika alitambua barua ya LIPUMBA? Na japo wabunge wale wa cuf walikimbilia mahakamani lakini haraka haraka mbona spika aliwaondoa bungeni?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom