Nini hasa lilikua lengo lake kuniuliza kama nimeoa au bado?

Nyamalapa

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
206
448
Kuna msichana nikikutana nae maeneo flani katika mizunguko ya hapa na pale nikatokea kumpenda, ingawa sikumuweka wazi palepale ila nilifanikiwa kupata mawasiliano yake na yeye mwenyewe ndie alienipa.

Mwanzoni tulikua tu kama marafiki wa kawaida ila baada ya kupita kama wiki moja nikaona nimuweke wazi kwamba nahitaji kuwa nae kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Baada ya kuwasilisha ombi langu kwake akaniuliza hujaoa? Nikamueleza ukweli kwamba sijaoa ndio maana nahitaji kuwa na wewe.

Baada ya kumuuliza anaonaje juu ya hili ombi langu akanambia yeye kwasasa anae mpenzi ila tunaweza tu kuwa marafiki wa kujuliana hali basi kutokana na jibu lake hilo nikaona sina sababu tena ya kumshawishi aachane na jamaa yake kwasababu yangu.

Sasa nikawa najiuliza wakati namtongoza kulikua na haja gani ya kuniuliza kama nimeoa au la ilhali anae mpenzi na angeweza tu kunijibu mojakwamoja kwamba haiwezekani sababu nina mpenzi.

Naomba mwenye uzoefu aniambie nini hasa lilikua lengo la yeye kuniuliza kama nimeoa au la wakati tayari ana mpenzi ingawa amenambia kwamba mpenzi wake haeleweki kama atamuoa au la.
 
Mwambie nataka kukuoa na sikukuchezea wanawake wengi wakisikia kuolewa akili zinawaruka Note; inategemea na mwanaume unavyojiweka.
 
Alitaka mme wa mtu, sio wewe bachelor...
Ilitakiwa jibu lako liwe fifty fifty ili upime upepo, akisema anataka mme wa mtu unajifanya umeoa, akisema anataka single unajifanya single.

Siku nyingine usikosee
Daaah 😆😆😆
 
Huyo alitaka nyote muwe wachepukaji mkuu, maana anamkubali Jamaa ake lakini Kuna vitu anavikosa kwa Jamaa

Nia ya kukuuliza vile ni alitaka uwe na mtu wako na yeye awe na wake ila muwe mnaruka pamoja ili kwamba usimnyime uhuru kwa Jamaa ake anapomhitaji maana ukiwa huna mtu Utakua unamzodoa sababu ya Yeye kua na uhusiano mbili kwa pamoja hivyo ungem'bana mno
 
Kuna msichana nikikutana nae maeneo flani katika mizunguko ya hapa na pale nikatokea kumpenda, ingawa sikumuweka wazi palepale ila nilifanikiwa kupata mawasiliano yake na yeye mwenyewe ndie alienipa.

Mwanzoni tulikua tu kama marafiki wa kawaida ila baada ya kupita kama wiki moja nikaona nimuweke wazi kwamba nahitaji kuwa nae kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Baada ya kuwasilisha ombi langu kwake akaniuliza hujaoa? Nikamueleza ukweli kwamba sijaoa ndio maana nahitaji kuwa na wewe.

Baada ya kumuuliza anaonaje juu ya hili ombi langu akanambia yeye kwasasa anae mpenzi ila tunaweza tu kuwa marafiki wa kujuliana hali basi kutokana na jibu lake hilo nikaona sina sababu tena ya kumshawishi aachane na jamaa yake kwasababu yangu.

Sasa nikawa najiuliza wakati namtongoza kulikua na haja gani ya kuniuliza kama nimeoa au la ilhali anae mpenzi na angeweza tu kunijibu mojakwamoja kwamba haiwezekani sababu nina mpenzi.

Naomba mwenye uzoefu aniambie nini hasa lilikua lengo la yeye kuniuliza kama nimeoa au la wakati tayari ana mpenzi ingawa amenambia kwamba mpenzi wake haeleweki kama atamuoa au la.
Hilo nalo unataka tukufafanulie?.Hivi vijana wa JF mtakua lini?.Hapa ni sehemu ya great thinkers tu,lete hoja zinazogonga vichwa.
 
Back
Top Bottom