Nini faida ya Push Up

Baba Kenzo

JF-Expert Member
Sep 16, 2017
224
149
Mamboz wadau !!
Push up zina umuhimu gani katika maisha ya binadamu? Je mwili unaofanya push up na mwili unafanya kunyanyua vyuma utofauti wake ni nini???
 
Kwa kuanzia, pushup ni nzuri, chuma ni mbaya.
Pushup inajenga mwili unakuwa mkakamavu.
Unakuwa na nguvu og.
......
.....
.....
 
Ivi hii thread ni ya hapa MMU au mimi naona kinyume nyume.

MMU and PUSH UP wapi na wapi jamani.....

Watu wengine wakikosa la kuuliza bora ukae pembeni ufanye maombi kwa ajiri ya lissu itakuwa poa saana, kuliko kuleta thread za namna hii...
 
Mi huwa napiga push ups kwa ajili ya mazoezi ya kujenga mwili..Chuma ni siku mojamoja
 
Mkuu umesema pushups ni nzuri kwamba zinajenga mwili unakua mkakamavu mwenye nguvu og, ukasema chuma ni mbaya lkn hukueleza ubaya wa chuma!
Kunyanyua chuma unakuwa unajiboost kwa nguvu yaani unakuwa kama broiler. Ila pushup unajaa kimpangilio.
Kuna uchunguzi ambao hujabainika kwamba chuma inapunguza nguvu za jeshi la north korea.
N.B. kunyanyua chuma sio mazoezi, bali pushup ndio mazoezi.
 
Kunyanyua chuma unakuwa unajiboost kwa nguvu yaani unakuwa kama broiler. Ila pushup unajaa kimpangilio.
Kuna uchunguzi ambao hujabainika kwamba chuma inapunguza nguvu za jeshi la north korea.
N.B. kunyanyua chuma sio mazoezi, bali pushup ndio mazoezi.
Noted mkuu. Kwa mantiki hiyo mwili Wa push up haurudi unapoaacha kupiga push up ila mwili Wa chuma unasinyaa MTU akiacha kunyanyua vyuma. Push zina create muscles wakati vyuma zinaumua mwili.
 
Push ups ni kwa ajili ya kujenga misuli na mazoezi ya maungio/joints.

Kuna aina nyingi za pushups ila nyingi zinahusisha misuli ya kifuani ( pectoralis major ) na ya nyuma ya mkono ( triceps brachii muscles ), hiyo ndio musuli inayojengeka vuzuri kwa kupiga push ups.

kuna push ups watu wa workouts wanaziita V, hizi huwa pia zinahusisha misuli ya kwenye bega (deltoid muscles) .
Hivyo hiyo ni gym tosha.

wanaonyanyua vyuma pia inategemea wananyanyua kwa staili gani, ndio maana mtu kama unaenda gym ni vyema uwe na instructor wa kukuelekeza namna ya kunyanyau chuma ili kufikia lengo lako katika kujenga mwili.

wale wanaolala kwenye bench na kuvyavyua chuma ni sawa tu na wanaopiga push ups tofauti ni uzito na body mechanics.
Wale wanaokaa au kusimama na kunyanyua chuma kwa kukuvya kiwiko(elbow joint) hawa wanafaida ya kujaza misuli ya mbele ya mkono (biceps) .
Hivyo ni vyema kubalance mazoezi ili mtu kuwa na shape nzuri.
I hope umeelewa.
 
Back
Top Bottom