Kuna Wanaume wengine Siku inaisha hata “push up “tatu hapigi. Badilika

Kuna Wanaume wengine Siku inaisha hata “push up “tatu hapigi. Badilika

Nshomile wa Muleba

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2015
Posts
2,165
Reaction score
5,643
Jambo jambo?

HUKU TUNA MACHUNGU YA BANDARI YETU EMU TUPITIE HAPA.

Kila mtu yuko bize na mambo yake, iwe kazi biashara au majukumu mengine.

Ila nashangaa kuna wanaume wengine huwa siku inapita hata push up 3 hajapiga ili kuchangamsha mwili na kuweka mwili katika tension. Ukitaka kusema uko bize sana unajidanganya, mimi ni kibarua cha wazungu ambacho kinanilazimu kudamka kila siku saa 10 alfajiri mpka saa 2 usiku( Huwa napiga overtime) ila siwezi kubali siku ipite sijapiga hata push up 10 kabla ya kuoga.

Ndo maana huwa nikikorofishana na mtu huwa nawanyuka kwasababu Ukirusha ngumi moja pumzi inakata halafu unakuta mimi ndo kwaaaanzaaaa naanza, Utakula vitasa mpaka uiite maji mmaaa na ubwabwa utauiita “UWAWA”

SI VZURI MWANAUME KUPITA SIKU BILA HATA KAZOEZI KADOGO AISEE.

Si kwaajili ya kupigana au nini bali hata kuchoma calories na kuweka mapigo ya moyo sawa.

WACHAGA NI WAVIVU WA MAZOEZI NDO MANA WANAUMWA SANA SUKARI(mbali na pombe na nyama)

Mwanaume anafakamia machipsi na makitimoto kitambi kama fuko.

Kwa taarifa yako piga push up hata 20 kwa siku na maji lita 3 uone kama nguvu za kiume zitakusumbua.


BADILIKAAAAA!!!!!!!!!

IMG_7221.jpg



Kwasasa

Chillers ya Kahama,Tanzania.

Gona bwino.
 
Mwili unajengwa zaidi na kile MTU anachokula.
Ukiujua hiyo Kanuni lazima uwe na afya.
Daktari yeyote BINGWA lazima akuambie Jambo hili.
Mazoezi sio lazima
Mazoezi sio lazima ila kama mwili wako haupo active yaani mfano kazi zako wewe ni za kukaa tu kwenye kiti kwa muda mrefu, basi unahitaji utafute namna ya kuustua mwili na namna nzuri ni kufanya mazoezi
 
Mazoezi sio lazima ila kama mwili wako haupo active yaani mfano kazi zako wewe ni za kukaa tu kwenye kiti kwa muda mrefu, basi unahitaji utafute namna ya kuustua mwili na namna nzuri ni kufanya mazoezi

Ni kweli.
Kama kazi zako sio za nguvu, Bali ni za kukaa muda mrefu utashauriwa ule vyakula visivyo na calories nyingi kama Wanga.
Ukila protein, vitamin, maji ya kutosha na wanga kidogo hata usipoushtua Mwili. Fresh
 
Watu wamekazana mazoezi hayasaidia kitu...nani anawadanganya? Wabongo wako na mentality moja kufanya mazoezi ili upungue basi" mazoezi faida zake ni nyingi kuliko hata hizo za kupungua..kama sio mtu wa mazoezi huwezi ELEWA body inavofeel ...kwanza mwili unakuwa calm sana hata wale wenye tatizo la afya ya akili linatatulika, pili unakuwa na mizunguko mzuri wa damu hata wale wenye tatizo la nguvu za kiume unaimprove. tatu ni kama umefanya jioni asubuhi lazima ujihisi mwepesi kama umetua mzigo fulani hivi.. nne ,unacontol kiwango chako cha sukari na blood pressure etc...faida ni nyingi sanaaaa .....KWA KWELI TUNAOFANYA MAZOEZI KUNA RAHA TUNAPATA MWILI SANA...
 
Mwili unajengwa zaidi na kile MTU anachokula.
Ukiujua hiyo Kanuni lazima uwe na afya.
Daktari yeyote BINGWA lazima akuambie Jambo hili.
Mazoezi sio lazima

tangu kini taikon wa fasihi akajua lolote kuhusu body building?

Acha kujidanganya kijana.Mazoezi ni sehemu ya maisha na siyo kula kula tu
 
Watu wamekazana mazoezi hayasaidia kitu...nani anawadanganya? Wabongo wako na mentality moja kufanya mazoezi ili upungue basi" mazoezi faida zake ni nyingi kuliko hata hizo za kupungua....

Naomba ujengeewe sanamu kariakoo.

Nikimaliza mazoezi halafu nikaoga najisikia mwepesi na toka nianze mazoezi najikuta nanyandua bao 4 mpka mademu wanachoka wao.

tatizo watu wanadhani mazoezi mpka ukimbie uwanjani

mimi nafanya hvi.
-Push up 50
-Squat 20
-Kuruka kamba hadi 100

basi
 
Back
Top Bottom