Nini faida ya bunge la tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini faida ya bunge la tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kiwi2010, Feb 14, 2011.

 1. kiwi2010

  kiwi2010 Member

  #1
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tumekua tukiona mara nyingi wabunge wetu wakiwa bunguni wakiwakilisha matatizo yetu kwa serekali lakini mambo yaliyo mengi huwa yanaishia hapohapo bungeni bila kupatiwa solution.
  Mfano sasa hivi tunatatizo la umeme lakini hatujaona nguvu ya bunge kuishinikiza
  serikali kutatua tatizo hili la umeme kwa haraka iwezekanavyo,wabunge wanaliongelea tu tatizo halafu hao wanatulia,walikua wanatakiwa waishinikize serikali kwa namna yoyote sio kuishia kusema tu.
  Kiufupi bunge letu linaishia kuongea tu bila kuleta mabadiliko yoyote,mimi naona wabunge watumie nguvu za umma kutatua matatizo yanayo tukwaza.Bila hivyo bunge halitakua na faida yoyote kwani serikali imesha jua mambo yote yataisha bungeni kwa majibu mazuri bila vitendo hasilia.
   
 2. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  SPIKA MAKINDA HANA MAWAZO HURU
  SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi.Anne Makinda ana shida katika mfumo wake wa kufikiri. Ana mawazo funge (mawazo yasiyo huru), mawazo yanayotokana na fikra za wengine. Hii inamaanisha kuwa kuna baadhi ya maamuzi ya Spika hayatokani na fikra zake mwenyewe bali fikra za wengine.
  Kwa watu makini na wanaofuatilia siasa za nchi yetu, watakubaliana na mimi kuwa Makinda wa sasa si yule aliyekuwa naibu Spika kwenye bunge la tisa. Tangu achaguliwe kuwa Spika (kwa mizengwe) Makinda anaonekana kuwa na mtizamo hasi sana kwa vyama vya upinzani bungeni hususani Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA). Sina hakika kama mtizamo huu alikuwa nao tangu kale, lakini nina hakika kuwa mtizamo hasi kuhusu upinzani umezidi maradufu baada ya kuwa Spika. Anawapuuza wabunge wa CHADEMA. Anawakebehi.anawadhalilisha.
  Yawezekana Makinda anakilinda chama chake cha Mapinduzi (CCM), na amekwishajua kuwa chama pekee cha upinzani chenye nguvu kwa sasa ni CHADEMA ndio maana anatumia kila awezalo kuwazima.
  Wabunge wa CHADEMA wanapochangia mijadala au kuuliza maswali utamwona Makinda anakuwa makini zaidi kuliko wabunge wa vyama vingine wakichangia. Yawezekana wengine hawajaiona hali hii, lakini ukifuatilia kwa makini utabaini ukweli wa niyasemayo. Binafsi siioni hali hii kuwa njema wala siamini Spika Makinda anavutiwa sana na hoja za Chadema kiasi cha kuwasikiliza kwa makini sana.
  Bali nionavyo anasikiliza hoja hizo kwa makini ili aweze kuzikosoa kabla hazijawasilishwa, akebehi kabla mtoa hoja hajamaliza, na azipuuze kabla hazijajibiwa. Ili zipoteze nguvu, zionekane hoja dhaifu, na awadhalilishe watoa hoja makini wa Chadema waonekane watu wenye hoja mufilisi.
  Hiyo ndio sababu ya Makinda kuwa makini wanapozungumza Chadema. Hii ndio kazi aliyotumwa na chama chake. Kuua upinzani. Na ni lazima atekeleze kazi hiyo kwa uaminifu ili kulinda kiti chake.
  Hebu tuanze na hili la “mwongozo wa Spika.” Jumanne ya tarehe 08/02/2010 mhe.Tundu Lissu (mbunge wa Singida mashariki-CHADEMA) alikalishwa chini mara kadhaa, na maongezi yake kukatizwa zaidi ya mara kumi kwa kile kinachodaiwa “mwongozo wa spika.” Kuna wakati mwongozo ulikuwa unaombwa mara tu baada ya Spika kutoa mwongozo mwingine. Yaani ilikuwa mwongozo juu ya mwongozo. Jinamizi linaloitwa “mwongozo wa Spika” likatumika kukatiza hoja za msingi za Mhe.Lissu.
  Kwa maana hiyo tukasadikishwa kuwa “jinamizi” mwongozo wa Spika linaweza kukatiza maongezi ya msemaji yeyote bila kujali hadhi yake. Lakina vichekesho vikaanza. Vituko vikatokea. Mipasho ikatawala. Dudu hili “mwongozo wa Spika” linaonekana ni mali ya CCM, na wapinzani hususani CHADEMA hawaruhusiwi kulitumia. Limeundwa mahsusi kuzima upinzani, na CCM wamepewa mafunzo maalumu ya namna ya kulitumia.
  Chadema hawana haki kutumia “mwongozo wa spika.” Ikiwa sivyo ni kwanini mhe.Godbless Lema mbunge wa Arusha mjini, alipoomba mwongozo wa Spika tarehe 10/02 kikao cha asubuhi, kwanza alipuuzwa, baadae akakejeliwa na Makinda kuwa “subiri kwanza niongee mimi.” Akiwa na maana kwamba Mhe.Lema haruhusiwi kuingilia maongezi ya spika.
  Lakini Mhe.Simbachawene mbunge wa Kibakwe (CCM) aliingilia maongezi ya Spika wakati Makinda akikaribisha maswali kwa wizara ya mambo ya ndani. Simbachawene akamkatisha Makinda kwa kigezo cha “mwongozo wa spika.” Lakini tofauti na Lema yeye alisikilizwa, akapewa nafasi na akaitumia fursa hiyo kuonesha upeo wake mdogo wa kufikiri.
  Simbachawene bila aibu akahoji uhalali wa Mhe.Lema kumtuhumu Waziri mkuu kusema uongo, ilihali Waziri mkuu ni mkubwa kwa Lema “kicheo na kiumri.” Katika kuonesha alivyo na mawazo chakavu, akatetea eti kumtuhumu (kuwa ni mwongo) mtu aliyekuzidi cheo na umri ni kinyume na Mila na desturi za Kiafrika. Hivyo eti akataka Lema aadhibiwe. Lahaulah!! Aibu gani hii kwa mtu anayejiita mbunge.
  Yaani Simbachawene anataka kutusadikisha kuwa mtu aliyekuzidi umri na cheo, anaruhusiwa kudanganya, kupotosha na kusema uongo anavyojisikia, bila kuhojiwa popote wala kukosolewa, maana tukimkosoa tutakuwa tumekiuka mila na desturi za kiafrika. Mi naomba Simbachawene asiwasingizie waafrika wote. Aseme tu labda ni mila na desturi za Kibakwe. Lakini hivi bunge letu linaongozwa na Kanuni, au mila na desturi?? Katika hili Simbachawene amepotoka.
  Lakini hapo awali kidogo nilisema jinamizi liitwalo “mwongozo wa Spika” ni mali ya CCM, na upinzani hususani Chadema hawana haki ya kulitumia. Katika kikao cha jioni ya tar.10/02/2011 mbunge wa Kawe mhe.Halima Mdee aliomba mwongozo wa Spika muda mchache kabla Spika hajatangaza wenyeviti wa Kamati za kudumu za Bunge. Tofauti na Simbachawene, Mdee hakuingilia maongezi ya Spika. Lakini Spika akamjibu kwa kejeli “mwongozo sasa hapana, maana ninyi mnadhani kila saa ni wakati wa mwongozo, sasa ni wakati wa kazi”
  Lakini chuki za Makinda kuhusu Chadema hazikuishia hapo. Ijumaa ya tarehe 11/02/2010 kwenye kikao cha asubuhi, akaibuka mbunge wa Nkasi kaskazini. Bila kuheshimu bunge, na bila kujali anatazamwa na Watanzania akaanza kutukana Chadema. Pamoja na matusi mengine, akahitimisha kwa kusema “..ningejiona wa hovyo sana kama ningechaguliwa kwa tiketi ya ChademaAkimaanisha wabunge wote wa Chadema ni wa hovyo.
  Mwanzoni wabunge wa Chadema walimvumilia kwa kuwa ni wastaarabu. Waliamua kukaa kimya maana maandiko yanasema “usimjibu mpumbavu kwa upumbavu wake usije ukafanana nae.” Lakini alipozidisha matusi mbunge wa Kawe Halima Mdee akaamua kuvunja ukimya. Maana maandiko kwa upande mwingine yanasema “mjibu mpumbavu kutokana na upumbavu wake, asije akajipatia kibali machoni pako”
  Kwa hekima Mdee akaomba mwongozo wa Spika, maana chama chake kilidhalilishwa, kiliudhiwa na kauli ya aliyejiita mbunge wa Nkasi Kaskazini. Hivyo akatumia kanuni ya 61 inayomtaka mbunge huyo wa Nkasi kufuta kauli yake ama kuomba radhi maana ni ya kuudhi. Ama sivyo bunge lielezwe kuwa ni ruksa kutumia kauli za hovyohovyo bungeni.
  Lakini cha ajabu badala ya kutoa mwongozo, Makinda akaendekeza hisia. Akatamka kwa hasira “mwenye mamlaka ya kuruhusu kauli za hovyo bungeni ni mimi” kisha akamruhusu yule mbunge wa Nkasi aliyekosa adabu aendelee kutukana. Jamani hata kama ni kukibeba Chama chake hapa sasa imezidi.
  Lakini turejee kidogo katika hoja ya Lema. Je ni kweli Lema alimtuhumu Waziri mkuu kuwa kasema uongo?? Nionavyo mimi Hasha!! Lema hakumtuhumu Waziri mkuu. Wote waliofuatilia kwa makini mjadala ule watakubaliana na mimi. Lema alihoji ikiwa mtu mzito kama waziri mkuu, akidhibitika amesema uongo bungeni, je ni hatua gani mbunge anaweza kuchukua?
  Kwa lugha nyepesi ni sawa na kusema Lema alihoji ikiwa kiogozi mkubwa wa serikali (kwa mfano waziri mkuu) akitoa kauli bungeni, na ikadhibitika kuwa kauli hiyo si ya kweli, je bunge linaweza kuchukua hatua gani?
  Hivyo Spika alipaswa kutoa mwongozo kuwa iwapo itadhibitika kiongozi mkubwa kama Waziri mkuu, ametoa taarifa ambazo si za kweli, ama anaweza kuchukuliwa hatua au vinginevyo. Na kama zipo hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi yake basi Spika aziweke bayana kwa mujibu wa Kanuni za bunge.
  Lakini cha ajabu hoja ikageuzwa. Ikapinduliwa. Ikabadilishwa. Badala ya Spika kutoa mwongozo, akamtaka Lema kudhibitisha. Adhibitishe nini? Lema aliomba mwongozo. Sasa adhibitishe mwongozo au..? Katika hili Spika alionesha fikra kurupushi. Eti adhibitishe tuhuma. Tuhuma zipi? Kumbe CCM wakiomba mwongozo si nongwa, lakini Chadema wakiomba mwongozo wanaambiwa wametoa tuhuma. Wadhibitishe. Ebo!! Ama kweli maskini haokoti,akiokota kaiba.
   
 3. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkubwa uko sahihi kabisa na sijui mwisho wake nini.
  Yani kilicho ongelewa mwaka 1975 ndo hicho hicho kinaongelewa mwaka 2010.

  Na shida kubwa iko kwenye implementation na ndiyo maana kila siku utasikia mambo yale yale yanajadiliwa bungeni (Umeme, afya, elimu, barabara)
   
 4. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #4

 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Mh Makinda kalisababisha bunge kuwa sawa na kijiwe cha ghahawa.
  Uzuri ni kwamba watz siku hizi hakuna haja ya kuelezewa kile kinachoendelea bungeni kwani tunakitizama live.
  Wabunge wote vilaza na wanaosaidiwa ukilaza wao na huyu mama aliyekunywa maji ya bendera ya ccm tutawaazibu majimboni watakaporudi kutoka huko dodoma.
  Watu tuna matatizo chungu mzima yaliyosababishwa na serikali halifu mbunge wetu hayazungumzii zaidi ya kuimba ngonjera ya kuisifu ccm na kuiponda chadema.
  .
   
 6. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kuna mahali nilisema natamani kumtwanga makofi huyu spika. hakika sikukosea! Unapotazama majibu ya huyu mama ni ya kijikonijikoni tu, hayana tija kwa bunge letu. Hatukuwapeleka bungeni kupashana. Tumewatuma kwenda kutekeleza yale ambayo tunataka tufanyiwe. Unapofanya chombo kikubwa kama Bunge letu kuwa ni mali yako then you dont deserve to be there. Sitta alipokuwa spika angalao alifanya kazi nzuri kidogo ingawa alibanwa na wanajiona ndo wenye hii nchi. Mimi naamini ule msemo wa mcimba kaburi huingia mtuwe! Ana Makinda anachimba kaburi ambalo atakitia chama chake humo. Watanzania wanaona, Watanzania wanasikia, Watanzania wanajua na mwisho Watanzania wataamua. Kuimba ngonjera ama mipasho. Subiri utaona matokeo ya kejeli hizi!
   
 7. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mama Maria Ibeshi na Maria mwingine viti maalum CCM wameni boa sana leo.
  Eti wanasema JK anakusudia kufanya maajabu for the next 5 years. Hivi huyu mama mbona anapotosha watu wenye macho na akili zao? . Hivi Maajabu ndio mgao wa umeme au kuilipa Dowans?

  Bibi nakuheshimu sana naomba upumzike kwani spidi ya sasa hivi ni kubwa na umeshaachwa mbali kwani huu udanganyifu na hadithi unazopiga unaweza kufanyia wajukuu zako tu.

  Plse tuwe objective tusiwafanye watanzania wa miaka hii kuwa ndo miaka sitini iliyopita. Watu kama hawa ndo wanaendekeza udikteta kwa kutaka kupitisha hoja za uongo kwa kufikiri watanzania wana vichwa visivyofikiri na kutumia polisi kulazimishia hoja zao feki
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Ni mradi rahisi wa kujipatia mahitaji binafsi kwao!
   
 9. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Historia huwa inaandikwa na watu wema na pia waovu. Ni suala la majira tu, sasa hatuwezi kuelewa Mh spika yeye anampango wa kuandika historia ya namna gani na kwa faida ya nani? Tuachiwe wakati, utatusaidia kuamua natumai macho ya watz na masikio yao yameelekezwa dom, nao pia watashiriki ktk kuandika historia ya nchi hii.
   
 10. z

  zamlock JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  jaman niseme ukweli sijawai kumshuhudia rostam azizi akichangia jambo lolote bungeni hivi anawawakilisha vp wananchi wake bungeni au wenzangu mlishawai kumshuhudia'?
   
 11. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nimegundua wabunge wengi siyo innovative ndio maana wanakuwa watu wa kupiga blabla tu pale bungeni. Wanauliza maswali ambayo ni non-sense na michango wanayotoa ni very cheap.

  Mimi natoka jimbo la Korogwe mjini ambapo mbunge wetu ni bwana Nassir ambae ni mjasiria mali wa pale Korogwe mjini. Bado sijamsikia akichangia na sijui atakuja na lipi jipya. Vilio vya wananchi wa Korogwe mjini vinajulikana ni huduma tu za jamii kama afya, elimu, ajira, maji, umeme etc. Kinacho nishangaza tangu nipate akili wabunge wote wamekuwa wakipiga debe kuhusiana na huduma hizo hizo na hakuna aliyepata ku archieve.

  Wabunge ninaowakumbuka
  1. Mhina
  2. Kihiyo
  3. Kizango
  4. Lupatu
  5. Bendera
  6. Nassir

  Wabunge wote hao waliopita wamekuwa wakipigia kelele vitu hivyo takribani miaka thelathini sasa na hakuna chochote kilichopatikana aidha afya, elimu, maji, umeme etc. Ila ninachotaka kusema lazima wabunge wawe wabunifu katika ku raise funds ili wananchi wajiletee maendeleo wenyewe. Mfano kuboresha hospitali ya wilaya mbunge aikitumia busara zake anaweza kuboresha.

  Kwahiyo ombi langu kwa wabunge jaribuni kuwa wabunif.u kutafuta sources za ku raise funds kwa ajili ya maendeleo ya majimbo yenu na siyo kupiga tu kelele bungeni. Kama wewe ni mbunge ume invest kupata ubunge na huna uwezo wa ku raise funds kwa ajili ya kujenga angalu wodi moja ya wazazi, kuchimba kisima cha maji au kutengezeza hata ajira 100 kwa vijana then YOU ARE USELESS. Binafsi nam count mbunge USELESS pale anaposhindwa kutatua matatizo ya wananchi na kudai kwamba Serikali haina pesa, that is nonsense.
   
 12. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Rais garasha...
  Spika grasha zaidi....
  sijui siku akikaimu madaraka ya uraisi itakuwaje?
  Huyu mama ni kikwazo kwa maendeleo ya TZ kwani ni mbaniaji wa majadiliano huru hasa hoja za msingi ili mradi zimetokea kwa MPs wa opposition...kwa wengine ruksa kubwabwaja
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Wengi sio useless ni opportunist. Politics ndio sehemu ya kutengenezea.
   
 14. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Napendekeza katika maandamano yaliyopangwa kufanyika nchi nzima kuanzia tarehe 24/2 huko Mwanza kitendo cha Makinda kuendesha bunge kama kijiwe kilaaniwe.
   
 15. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ni sawa ila wengi hawajui "the how"
   
 16. M

  MZALAMO JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 60
  Wanafikiri bado wako zama zile za zidumu fikira za mwenyekiti wa CCM hata kama anaboa zidumu. Wanafiki wakubwa!
   
Loading...