Nini chanzo cha nchi za Magharibi kuitwa "Mabeberu"?

carcinoma

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
5,059
13,720
Kwenye vitabu vya shule ya msingi ubepari uliokomaa unaitwa ubeberu... hapa nadhani wataalamu wa kiswahili waje watuambie ilikuaje kiswahiki cha imperialism kikawa ubeberu.
 
... kwanza beberu ni mbuzi dume lililokomaa na lenye maguvu mengi; kutokana na maguvu hayo, lina uwezo wa kuwaonea mbuzi wengine hususan wadogo kwa kuwapiga na hata kuwanyang'anya chakula chao. Sometimes likiamua linajitwalia majike lipendavyo bila kubughudhiwa na "vidume" vingine na kitakachothubutu kukaribia ni kipigo kikali sana pengine hadi mauti.

... hivyo inawezekana (sina uhakika) dhana ya ubeberu ilitokana na mtazamo wa nchi za kijamaa (East) kuziona nchi za magharibi kwa mtazamo huo (hata kama sio sahihi) kwamba kutokana na maguvu mengi ye kiuchumi, kiteknolojia, kijeshi, n.k. zilizokuwa nazo, zilitumia maguvu hayo kuzionea nchi masikini (vimbuzi vidogo) na hata kuwanyang'anya kile kidogo (rasilimali) walizokuwa nazo kwa faida zao.

... nahisi hiyo ndio dhana japo ya kipumbavu kwa sababu dhana hii iliacha sababu nyingine za msingi za umasikini wa nchi maskini kama viongozi kutoheshimu katiba na sheria, kujilimbikizia na kufuja mali za nchi zao; upendeleo katika nafasi mbalimbali; uongozi wa kiimla a.k.a miungu watu; chama kushika hatamu; uongozi wa hovyo usio na dira ya maana, n.k. Ni dhana ya viongozi kutafuta pa kujificha pale wanaposhindwa kutatua matatizo ya nchi zao badala yake kutupa lawama kwa "mabeberu" ili kuwahadaa wananchi.

Nyerere aliwahi kusema, ili tuendelee tunahitaji vitu vinne - watu, ardhi, siasa safi, na uongozi bora. Sasa pima mwenyewe Afrika imekwama wapi? Ni kwa sababu ya "mabeberu"? Beberu linaingiaje kwenye hizo issues 4 a.k.a nguzo muhimu za maendeleo kwa mujibu wa Mwalimu?
 
Back
Top Bottom