Nini chanzo cha akinababa kutelekeza famila zao?

Nini chanzo cha akinababa kutelekeza famila zao?

gilbert gratian

New Member
Joined
Mar 6, 2013
Posts
1
Reaction score
1
Katika jamii tumeshuhudia ndoa nyingi kuvunjika na akina mama kubwagiwa majukumu yote ya kuwalea watoto. Idadi ya akina baba wanaotekeleza familia zao inaongezeka siku hadi siku, aidha kwa kuanza familia nyingine ama kuenda kujitegemea na kukaa kama bachelazi wasio kuwa na majukumu ya kifamilia.

Wadau naombeni mawazo yenu, mnadhani tatizo hasa ni nini?
 
ndugu yangu kutelekeza familia wala sio jambo jipya la muda mrefu sana mimi mwenyewe ni muhanga wa jambo hilo kwa uelewa wangu hakuna mtu yeyote anaeweza kumtoa mwanaume ndani kama sio roho na mtazamo wake ameamua kufanya hivyo! hiyo inakua tayari katika moyo wake keshaijenga anasubiri tu chance afanye ivo ebu tua chini kidogo ufikiri mtu kuwekewa mdalasini kwenye maji na kubebwa mgongoni kwenda kuoga anatelekeza familia bila kosa lolote aisee! fuatilia uone mwisho wa mibaba ya dizaini hiyo inakoishiaga chezea radhi ya mke wewe!
 
Mibaba mingi ni mibinafsi sana, Wengi wanawaachia Akina mama majukumu ya familia kwa sababu mama hawezi akamkimbia mwanawe unless akili kapuku.

KUna sababu nyingi zinawafanya wa baba watelekeze family Kama vile kukwepa majukumu ya moja kwa moja, Tamaa inayo amabatana na ubinafsi wa kupindukia na umalaya wa kiume, lifists hawapendi familia, kuna makaka hawataki kukua.

WAnaume pia ni waoga sana anapoyumba kiuchumi anatapatapa na saingine kuamua kukimbia familia.
 
Sababu zipo nyingi lakini napenda kubainisha chache.
1. kutokujitambua na kukwepa majukumu ya kifamiliya.
2. Ujinga wa mwanamke, ukali, uchafu, uvivu, kukosa busara, na kutokujitambua.
3. Kukosa upendo na kutokumjua MUNGU.
Tafakari kwa makini sababu hizi na uzifanyie kazi, kutelekezwa kutabaki historia.
 
Mambo ya uswahilini hayo, unaoa mke halafu unamuacha ukweni na watoto, siku ujkita haja, wamwita kwako.....mmmh utakuta mtu ana wake 4 lakini wote wanakaa kwao(kwa baba na mama) jamaa akihitaji anamuita mmoja wao...... Mambo ya uswahilini bhana ujinga mtupu...............!
 
wavaa suruali wasiojua heshima+wajibu ya uanaume
 
wababa wengi hutelekeza familia kwa sababu mtambuka sana. wengi hutoa sababu kibao na nyingi zikiwa zina onyesha mwanamke ndio chanzo cha matatizo.

but ukweli ni kwamba mwanaume yyte anayetelekeza familia yake husukumwa na ujinga tu na hakuna jambo jingine lolote lile.
 
Wanaume wengi hukimbia familia kwa sababu ya midomo ya wanawake. Kuna wengine huamua kuwapa vipigo vya mara kwa mara na pengine kuwadhuru. Lakini wengine hawapendi vurugu hivyo huamua kumwachia kila kitu na kwenda kuanza maisha upya.
 
Mibaba mingi ni mibinafsi sana, Wengi wanawaachia Akina mama majukumu ya familia kwa sababu mama hawezi akamkimbia mwanawe unless akili kapuku.

KUna sababu nyingi zinawafanya wa baba watelekeze family Kama vile kukwepa majukumu ya moja kwa moja, Tamaa inayo amabatana na ubinafsi wa kupindukia na umalaya wa kiume, lifists hawapendi familia, kuna makaka hawataki kukua.

WAnaume pia ni waoga sana anapoyumba kiuchumi anatapatapa na saingine kuamua kukimbia familia.

$io kweli
 
Mambo ya uswahilini hayo, unaoa mke halafu unamuacha ukweni na watoto, siku ujkita haja, wamwita kwako.....mmmh utakuta mtu ana wake 4 lakini wote wanakaa kwao(kwa baba na mama) jamaa akihitaji anamuita mmoja wao...... Mambo ya uswahilini bhana ujinga mtupu...............!

hizo zilikuwa hadithi za abunu asi...we tangu umezaliwa ulishawihi kuona jambo hilo ulioandika?..au kila kitu unanakili.!?
 
Kuna mtu kaniacha hoi hapa.........anasema sababu ni kina mama ku audit simu za waume zao!
 
Chanzo ni wanawake wanaong´anga'ania waume wa wenzao
 
Mibaba mingi ni mibinafsi sana, Wengi wanawaachia Akina mama majukumu ya familia kwa sababu mama hawezi akamkimbia mwanawe unless akili kapuku.

KUna sababu nyingi zinawafanya wa baba watelekeze family Kama vile kukwepa majukumu ya moja kwa moja, Tamaa inayo amabatana na ubinafsi wa kupindukia na umalaya wa kiume, lifists hawapendi familia, kuna makaka hawataki kukua.

WAnaume pia ni waoga sana anapoyumba kiuchumi anatapatapa na saingine kuamua kukimbia familia.

Asikuambie mtu, hujui nini maana ya kuwa mwanaume halafu you cant provide for your family asisee it is a big mistery nakuambia, na nyie wanawake wengi wenu mnakuwaga sio supportive kipindi baba anapitia financial crisis na ndiyo upate mwanamke mwenye kipato ndiyo utakoma hata remote ya TV ukishika tu ni masimango aisee.

Wakati mwingine ni circumstances zinawafanya waafikie maamuzi ya ajabu sio kosa lao although kuna hayo uliyoyasema kuwa kuna majitu mengine hayataki majukumu ni majitu ya ajabu ila tusifanye generalisation kabisa maana na wenyewe wanawake wengine ni vimeo hatari, wanadhani pesa ni M.a.k.a.l.i.o kwamba kila muda mwanaume anapumua hela tu,.

But for sure nakuambia, hujui ni jinsi gani mwanaume anakuwa na hali ngumu pindi he cant provide for his family, uanaume wote huisha dadangu hata kama mkeo ni muelewa kiasi gani maana unakuwa poyoyo tu huchelewi kuitwa mwanaume suruali jinsi madada zetu wengine walivyo na ligha za chooni.:A S 39:
 
wavaa suruali wasiojua heshima+wajibu ya uanaume

Haya ndiyo majibu mepesi kwenye maswali mazito, najua unajua zaidi ya hayo uliyoyaandika ila umeamua kuishiakwenye hilo tu. Nina jamaa yangu mamake alikuwa hamuambii babake ni nani until alipofika chuo kwa juhudi zake binafsi akamjua babake tayari alikuwa ameoa mama mwingine, kuja kumuuliza story ilivyokuwa, jamaa aliishia kulia na kumlaumu mamake kwa nini hakumkutanisha na babake siku nyingi. kumbe baba wa jamaa alikuwa anataka amsaidie yule mama kusomesha tena ana uwezo wa hali ya juu lakini yule mama kwa kiburi alikuwa hataki.

Ishu ilikuwa babake yule mama alikuwa mkoloni sana na alitaka kukmfunga yule mzee by that time jamaa ikabidi akimbie, lakini yule mwanamke akajifungua na akampa mtoto jina la ukoo wa wajomba, its very sad story maana ni ulimbukeni tu wa yule mwanamke bila kutaka kuelewa kuwa circumstances zilimfanya yule bwana kusepa!

Haya mambo sa nyingine ni zaidi ya unavyoyafahamu ndugu zangu.
 
Back
Top Bottom