Nini chanzo cha akinababa kutelekeza famila zao?

Nini chanzo cha akinababa kutelekeza famila zao?

Ni bora anayekimbia maana mwanamke anapata shida akijua mme hayupo.

Kuna wengine yuppo nyumbani na hana mchango wowote kwenye familia. Faida yake ya kuwepo kwenye familia iko wapi?
 
Wanaume wengi hukimbia familia kwa sababu ya midomo ya wanawake. Kuna wengine huamua kuwapa vipigo vya mara kwa mara na pengine kuwadhuru. Lakini wengine hawapendi vurugu hivyo huamua kumwachia kila kitu na kwenda kuanza maisha upya.

wanao pia unawatelekeza wamekosa nini
mambo mengi ni ya kurekebisha tu na si kuacha damu
yako kirahisi!ndio maana baba ni kichwa cha familia!
ila wengine huo ni shingo hawafikirii!

 
Katika jamii tumeshuhudia ndoa nyingi kuvunjika na akina mama kubwagiwa majukumu yote ya kuwalea watoto. Idadi ya akina baba wanaotekeleza familia zao inaongezeka siku hadi siku, aidha kwa kuanza familia nyingine ama kuenda kujitegemea na kukaa kama bachelazi wasio kuwa na majukumu ya kifamilia.

Wadau naombeni mawazo yenu, mnadhani tatizo hasa ni nini?

Majibu ya swali lako ni kama ifuatavyo;
UMASIKINI,ROHO MBAYA,AKILI NDOGO,MAUDHI YATOKANAYO NA TABIA KWA MWANAMKE,KUPOEA KWA MVUTO KWA MWANA KE,USHAWISHI WA NYUMBA NDOGO PAMOJA NA KULOGA WANAUME ZA WATU,FAMILIA KUWA KUBWA KULINGANISHA NA KIPATO,KUFUKUZWA KAZI AU KUPOROMOKA KI UCHUMI KWA BABA,BABA KUTAKA KUMKOMOA MAMA KUTOKANA KISABABISHI FULANI KINACHOWEZA KUMDRIVE AFANYE HIVYO.N.K
 
Bora anaebaki nyumban watoto wakila nae chakula ambacho hakina chumvi wataridhika kuliko yule anayeikimbia familia
Ni bora anayekimbia maana mwanamke anapata shida akijua mme hayupo.

Kuna wengine yuppo nyumbani na hana mchango wowote kwenye familia. Faida yake ya kuwepo kwenye familia iko wapi?
 
Wababa wa namna hiyo hukwepa majukumu yao. Na ni kweli familia nyingi zimeteseka kwa hii tabia ya wababa lkn thank God wababa wengi wa leo wanajali sana familia zao ukilinganisha na wababa wa kizamani japo sio wote sitaki kusteriotype. Siku hizi wababa hasa wa mjini naona kuna mabadiliko kidogo kwakweli wanajitahidi kutunza familia.
Hakuna excuse ktk kutelekeza familia ni ubinafsi na roho mbaya tu na wengine ni wavivu wa kufikiri hudhani kukimbia tatizo ni solution, Wengine hutoa visingizio vya maisha magumu nk.
 
Back
Top Bottom