Nini Cha kufanya ukiwa unapitia kipindi kigumu?

Mama 1

Member
Joined
Oct 15, 2026
Posts
8
Reaction score
28
Habari wanajukwaa, tupeane moyo na uzoefu Kwa wale wote waliopitiaga kipindi kigumu waliweza vip kufanikiwa na kuvuka hapo.

Nimekata sana tamaa ya Maisha.

Ni muda mrefu Sasa sina shughuli maalum ya kufanya,nimefanya biashara ndogo ndogo lakini zimekuwa zikifa kutokana na ugumu wa biashara na pia kutegemea biashara hiyo hiyo kwenye mahitaji ya familia.

Kwa Sasa Nina muda mrefu bila shughuli yoyote rasmi tofauti na kufua fua nguo Kwa watu .nikipata elf tano inaisha Kwa matumizi ya familia .na sio mara zote napata kibarua..

Hakuna kitu kinaumiza kichwa kama unaamka asubuhi huna kazi yoyote na ndani hakuna chumvi Wala unga. Usiombe jamani

Kama Kuna mwenye kibarua ambacho naweza pata kipato Kwa wiki au Kwa mwezi naomba anisaidie niweze kujikimu na familia.

Asanteni sana
 
Andika details zako kwa kina tuangalie namna ya kukusaidia.

Andika umri wako, unapoishi, elimu yako, uzoefu wako wa kazi ulizowahi kuzifanya kabla.

Marital status yako ikoje, una watoto nk.
 
Habari wanajukwaa, tupeane moyo na uzoefu Kwa wale wote waliopitiaga kipindi kigumu waliweza vip kufanikiwa na kuvuka hapo.

Nimekata sana tamaa ya Maisha.

Ni muda mrefu Sasa sina shughuli maalum ya kufanya,nimefanya biashara ndogo ndogo lakini zimekuwa zikifa kutokana na ugumu wa biashara na pia kutegemea biashara hiyo hiyo kwenye mahitaji ya familia.

Kwa Sasa Nina muda mrefu bila shughuli yoyote rasmi tofauti na kufua fua nguo Kwa watu .nikipata elf tano inaisha Kwa matumizi ya familia .na sio mara zote napata kibarua..

Hakuna kitu kinaumiza kichwa kama unaamka asubuhi huna kazi yoyote na ndani hakuna chumvi Wala unga. Usiombe jamani

Kama Kuna mwenye kibarua ambacho naweza pata kipato Kwa wiki au Kwa mwezi naomba anisaidie niweze kujikimu na familia.

Asanteni sana
Unapatikana wapi Mama 1? Umeifikisha shida yako mahali sahihi. Na imetugusa sana ☺️
 
Pole sana kwa mapito, kitu cha kwanza ukiwa kwenye nyakati ngumu ni IMANI, Amini kwamba huu ni wakati umekuja ili upate kujifunza,
Amini nyakati ngumu hazidumu...kisha kubali kujinyima hata mahitaji ya msingi ili utengeneze chanzo imara cha mapato ya kila siku...
Usichague kazi yoyote halali hata kama inakuletea fedheha kiasi gani, ifanye kwa malengo na kwa moyo wako wote...
Usiache kumuomba na kumshukuru Mungu kila unapoenda kulala na unapoamka asubuhi kwenda kwenye mihangaiko, sala huwa zinaleta nguvu na kukupa IMANI.......
Mwisho usikubali kupoteza FOCUS na kuingia kwenye utafutaji kwa njia haramu zisizofaa kwenye jamii..
 
Usikate tamaa,hiyo ndio sumu kuu kwenye maisha,endelea kupambana,

Matatizo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu,sometimes matatizo hua ni njia tu ya kukupeleka sehemu iliyo bora zaidi,wengi wa waliofanikiwa,walipitia ugumu kama wako,

Wakati wewe unalalamikia ugumu wa maisha,kumbuka kua,kuna watu sasa hivi wanapigania uhai wao kwa magonjwa yasiyo tibika,

Narudia tena,usikate tamaa,
If you are still alive,you can be a King.

All the Best.
 
Marital status yako ikoje
Screenshot_20261017-063758.jpg
 
Back
Top Bottom