Nini amekifanya Mbunge wako jimboni kwako toka 2010 hadi sasa?

Pro-CDM JF wengi ni pumba sana hata kazi za mbunge hawajui.
Weka wewe barabara alizojenga mbunge wako

Mzee unatwanga maji kwenye kinu. Hawaelewi hao, wanachojua ni kulalamika na kusingizia.
 
Mbunge wangu Jeremia Sumari(ccm) arumeru toka alipochaguliwa hajawahi fika bungeni. hata kuapishwa bado ni mgonjwa.

Mbunge wetu ni mzima kabisa, I have seen him twice. The only thing i can say he doesnt give a shirt about Arumeru....... busy working in his office in Dar!
 
Nimesoma thread iliyoandikwa kuwa " Filikunjombe afanya makubwa Ludewa " hii imekuja kutokana na Mbuge huyu kijana kutoa gari la kubebea wagonjwa la Tsh mil 90.

Naomba tuangalie kwa kina Wabunge wengine wamefanya nini tangu walipo chaguliwa hadi sasa ili kuwaletea wananchi maendeleo ikiwa ni pamoja na kutimiza baadhi ya ahadi alizo ahidi kipindi cha kampeni.

Mfano SUGU - Mbeya Mjini ( CHADEMA), Barabara nyingi za mitaani zina wekwa changalawe chini ya uongozi wake

Filikunjombe - Ludewa (CCM), Ametoa gari la wagonjwa na kuahidi kutoa zaidi kila kata ikiwa ni pamoja na kufuatilia ahadi ya Mh. Rais

NOTE: Hii itasaidiakujua nani hawajibiki kwa kutimiza ahadi zake kwa hiyo atapoteza nafasi yake 2015
Kumbuka siku njema huonekana tangu asubuhi

Naomba kuwasilisha

mbunge wangu JUMA NKAMIA kilaza kweli najuta kumchagua
 
Mimi nakaa Kijitonyama so Mbunge wangu ni Mnyika,
Angalau sasa kwa kipindi kifupi alichokua madarakani maji yanatoka,
Tofauti na nlivyokaa kinondoni miaka 8 sikuwahi kuona tone la maji likitoka bombani hata siku moja
 
Mbunge wangu GOSBERT BLANDES amefanya mengi sana.Tangu aupate ubunge ameweza kuwanyanganya Ardhi wananchi wa jimbo letu la karagwe na kujimilikisha ng`ombe wengi kutoka kwa wahamiaji / wafugaji haramu kutoka uganda na rwanda wanaoingia tanzania kutafuta malisho ya mifugo wao.
 
Amesimamia kvipi?..... yaani kama nyapara au?
Mbunge haleti barabara, wala haleti umeme .... ungeuliza hizo barabara na huo umeme umefadhiliwa na nani,hizo projects ziliandikwa na nani na fedha zimetoka wapi?
Hapo ndio utajua what it took to get those projects going.
Sio mbunge anayelete miradi ya kiuchumi. Hapa watanzania inabidi tupeane shule.

Uwe unasoma koment ya mwenzako vizuri kabla haujajibu utumbo!? Umeambiwa Zito kafanikiwa kusimamia ujenzi wa barabara, hajasema ka yeye ndo kazijenga
 
Mbunge wangu Vincent Josephat anasomesha watoto wasiojiweza wa sec zaidi ya 90,barabara zimewekwa changarawe na baadhi wameanza kujenga mitaro,kila baada ya miezi 3 anafanya mkutano na kutueleza manispaa wamefanya nini na mipango ijayo,akimaliza kikao cha bunge anarudi jimboni,2015 anaendelea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom