Nini 787 dreamliner na tugemee nini?

What should be done then?
 
What should be done then?
Kwenye hili, rais alazimishwe aeleze.

1. Kwa nini kanunua ndege nje ya bajeti?
2. Kwa nini hajafuata utaratibu wa open tender?
3. Kwa nini haweki wazi gharama za manunuzi na mikataba ya ukarafati ya ndege?

Bila ku address haya masuala, tunaweza kushangikia kama ng'ombe anayeshangilia huku anapelekwa machinjioni.
 
How to do that? Suggestion ya Njia za kufanya haya
 
How to do that? Suggestion ya Njia za kufanya haya
Wabunge kazi yao ni nini? Hususan wa upinzani. Zitto ameshaanza kuizia mikataba.

Hata CCM nako kunatakiwa kuwe na upinzani wa ndani.

Waandishi wa habari waandije ubaya wa kushangikia bila kuchunguza. Wamulike haya mambo. Mara nyingi huwa kinachoonekana juu ni "tip of the iceberg". People are as honest as they are compelled to be. That is, if tge president is not compelled to be transparent by the people, he could pull all kinds of shoddy deals. Thats why we have checks and balance.

Wananchi wako wapi? Wahasibu wako wapi? Wachumi wako wapi?

Hii nchi haina watu wanaofikiri?

Watu hawana confidence? Wana woga?
 
Tuikatekateee waiuzeee scraper mkuuu...
 
Kama huna taarifa kamili ni bora ukakaa kimya.
 
Kinadharia inawezekana upo sawa. Ila ukweli hata wewe unauelewa, namna Jamii ya waTz tunavyoishi, mambo tunayoendekeza na mtindo wetu wa kukosoa serikali, labda kama una suggest tubadilike na hiyo si kazi rahisi au ndogo.
 
Kinadharia inawezekana upo sawa. Ila ukweli hata wewe unauelewa, namna Jamii ya waTz tunavyoishi, mambo tunayoendekeza na mtindo wetu wa kukosoa serikali, labda kama una suggest tubadilike na hiyo si kazi rahisi au ndogo.
Hususan kwa sababu RC kashasema wazi atawashughulikia wasiomuimbia mapambio muheshimiwa.

Hivibwatu wazima na ndevu zao wanakaangalia hako katoto kanawatisha, kwa sababu ya cheo cha serikali?
 
Hususan kwa sababu RC kashasema wazi atawashughulikia wasiomuimbia mapambio muheshimiwa.

Hivibwatu wazima na ndevu zao wanakaangalia hako katoto kanawatisha, kwa sababu ya cheo cha serikali?
Hahaha. Nadhani kwa sentensi yako tupo on the same side kwa sasa. Kusubiri muda utoe tathmini yake.
 
Mkuu,maamuzi ya wafrika wote yamegubikwa na hisia kuliko kuangalia uhalisia wa jambo husika,Tanzania ilikuwa haina haja kununua ndege inayotumia dollar za kimarekani 13,000$ kwa saa,Tanzania inahitaji kuimaimarisha usafiri wa Anga wa ndani,halafu ndio ingekurupuka kununuahiyo Boeing..

Leo nimesima ya "Article" moja ya jamaa aliebobea katika mambo ya Anga anaeitwa Tomas Chlumecky,nafikri huyu jamaani mmarekani..Jamaa amesema hiyo ndege inagharimu dolaa za Kimarekanin 30,000 kwa kupaki kiwanjani,halafu inagharimu dollar za kimarekani 15,0000 kwa saa kama iko angani,hiyo ndege inahitaka iruke masaa +4000 kwa mwaka kwa kwa hesabu za haraka hiyo ndege inatakuwa inagharimu 62,8 mil dolar za kimarekani,hiyo inamaana hiyo ndege lazima itegengeze zaidi ya dolla za kimarekani 62,8mil kwa mwaka.hapo bado hajaongelea matengenezo madogo madogo ya ndege nk..

Watanzania ni watu wapole na wasikivu sana,sema bado hawajapata Kiongozi madhubuti wa kiwaongoza,Nchi inaendele na kupata maendeleo mazuri ya kiuchumi na kijamii kama wananchi wake wananidhamu ya Maisha,watanzani tayari wana nidhamu kinachokosekana ni Kiongozi madhubuti anaewapenda raia wake....

Magufuli kanunua ndege kwa hisia zake binafsi hata ukisikiliza hotuba yake ya kuipokea ile ndege imejaa Hisia kuliko uhalisia au utaalamu wa kwanini ile ndege imenunuliwa..Ndege ubavuni imeandika "Hapa kazi",imeandikwa Kilimanjaro bila ya kufanunua Kilimanjaro Mlima,Mkoa au Bia,Tumeshindwa hata na KLM ubavuni mwa ndege kumeandikwa "Mt Kilimanjaro" inayomaanisha kuwa wamekusudia Mlima wa Kilimanjaro..

Nchi ya Wajinga Raisi wao ndio kubwa la wajinga...😀
 
Nimeisoma hiyo article. Jamaa kachambua vizuri' Ila simfahamu na sijui undani wa aliyosema sababu sifahamu chochote kuhusu ndege. Ningekuwa Nina muda ningefuatilia uhalali wa alichosema Ila kwa sasa nahangaikia kipato zaidi' hayo mengine ngoja niwe mtazamaji na Mtoa maoni pale nilipo na ufahamu. Ila kama jamaa yupo sahihi aisee itakuwa mbaya sana.
 
Tujifunze kusikilize wataalamu sio kila kinamuliwe kisiasa,Mkurugenzi wa Ethiopia Airline alipoulizwa majuzi na DW kwanini shilika la hio la Ndege limefanikiwa sana ijapokuwa kuna changamoto sana za kisiasa Ethiopia,alichojibu ni kuwa Ethiopia Airline inaendeshwa kitaaluma sio kisiasa,Serikai ya Ethiopia haingilii kabisa juu ya maamuzi na uendeshaji wa Shirika hilo..
 
Kama huna taarifa kamili ni bora ukakaa kimya.
Kutokuwa na taarifa haimaanishwi ulishwe matango pori. Kama huna taarifa basi tumia hata reasonableness au logic kuhoji jambo ambalo halina uhalisia vinginevyo utakuwa tofauti na wale wanaosema ndiyo kwa kila jambo yaani wewe ni Zuzu, sasa sijui na wewe nikuweke kwenye kundi hilo.
 
"mfano mgeni huyu anatumia lita 6,811 kwa saa" hili jambo unauhakika nalo, kutoka USA mpaka TZ itatumia lita ngapi? kwa muda wa masaa 13 hadi 16? mnapoongea muwe na uhakika. unajua hiyo ni Sh ngapi mafuta tu. hapa kunauongo kabisaaa.
kaka nakwambia tz tuna watu wajinga kwa kiwango cha lami. yaan wanaongea tu. ndo rais aliwaita mazwazwa. lita 6000 ni tani6 za uzito eti kwa saa, hayo mafuta inayabebea wapi, hebu jaribuni kuwa mnafanya ka utafiti kidogo kabla ya kuleta nyuzi humu, jf ni great thinker, sio whatsap humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…