Ningependa kumjua msemaji rasmi wa wakazi wa Dar es Salaam

Msemaji mkuu kwa sasa ni
KUBENEA na Meya JACOB

(Hata I. MWITA hatuna haja naye.. Anaonekana msaliti)
 
kwa mtazamo wangu kiongozi au msemaji wa jiji la dar alipaswa kuwa kiongozi wa kuchaguliwa na si kiongozi wa kuteuliwa na rais kamwe. huku ni kuwadharau wananchi.
 
Bavicha acheni kujitoa fahamu
Rc ana nguvu zote kuhusu mkoa wake,vyombo vyote vya dola vipo chini yake
Meya labda uniambie kuhusu kuzoa taka na yafananayo kama leseni za vileo lakini sauti ya mwisho ni mkuu wa mkoa
Halafu mbona hamuhoji sehemu zenu zingine zenye halamashauri mameya hawana nafasi yoyote zaidi ya Rc kama Arusha
 
"ISSUES" ZINATOFAUTIANA NA UGENI HUSIKA, " TEAM WORK" NI MUHIMU SANA KATIKA ITIFAKI ZOTE...
MKUU WA MKOA NA "HIS LORDSHIP THE MAYOR OF DSM."....KITAIFA NI MKUU WA MKOA NA KUNA ISSUES ZA JIJI AMBAZO MAYOR HUHUSIKA.....
2.Ulinzi na usalama Mkuu wa Mkoa
3.Itifaki za kitaifa na wageni Mkuu wa Mkoa Mayor huenda pia kwa MWALIKO MAALUM
 
Kuna hapa watu wamepewa vyeo halafu wakatamkiwa kuwa nyinyi ndio maraisi wa hiyo mikoa/wilaya sasa walivokuwa vichwa zege bila kutafsiri vizuri wakachukua job description zao wakazifungia kwenye makabati. Wakachukua kibao juu yake wakaandika, MIMI NI RAISI WA DAR... MANYARA... ARUSHA....

Hawa ndio vinara wa miaka 7/kumpa ufalme BWANA MALAWAMA
 
Huyo Huyo unaemjua...
Anaetoa matamko kila kukicha...
Nadhani utamjua siku akikuweka mikononi.
Kuongoza kwa kutumia intimidation and fear ni kitu kilichopitwa na wakati. Hii ilishika chart enzi za kina Mobutu, banda na Mzee Kenyatta. Kiongozi anayefanya hivyo sasa hivi ni kama anafukuza kivuli chake. Anaweza kufanikiwa kwa kipindi kifupi lakini in a long run nchi inaweza kuingia kwenye fujo mbaya sana. Magufuli angeweza kuwa mmoja wa marais wazuri sana kama asingekuwa anasikiliza ujinga kama huu wa kwako!
 
Jiji la Dar es Salaam lina viongozi wa Serikali Kuu na viongozi wa Halmashauri (serikali ya mtaa). Viongozi wa serikali kuu huteuliwa na Rais na viongozi wa Halmashauri huchaguliwa na wananchi. Kwa kweli nimekuna kichwa lakini bado nimeshindwa kupata majibu sahihi kwa maswali yangu haya matatu kisheria, kiutaratibu, kikanuni, kiutamaduni na kiitifaki;
  1. Nani ni msemaji rasmi wa Jiji la Dar es Salaam.
  2. Nani ni mwakilishi rasmi wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam
  3. Kama kuna mgeni ama wa ndani au nje anataka kufanya ziara rasmi kulitembelea Jiji la Dar es Salaam nani anastahili kuwa mwenyeji wake?
MAKONDA
 
Acha upuuzi wewe, tumia ubongo Wa nyuma, Rc anachaguliwa na Rais.Baada ya sisi kumchagua yeye, na ndiye mwakilishi wake mkoani.
Wewe ni empty brain. Kauli yangu ile ilikuwa ya kupima hilo. Una bahati umepata mtu wa kukuelezea kidogo.
 
Kwa nchi karibu zote ninazozifahamu zenye meya wa kuchaguliwa, viongozi wote ndani ya mji/jiji wako chini ya Meya na wanawajibika kwake.

Kwa kuongezea wakati Jiji la Dar es Salaam liko mikononi mwa Meya marehemu Kitwana Kondo, yeye ndiye alikuwa kila kitu kwa mambo yanayohusu jiji na wakazi wake.

Tz Meya hachaguliwi na wananchi , anachaguliwa na madiwani na wabunge, ukisema Meya anachaguliwa na wananchi basi hata Spika pia utasema anachaguliwa na wananchi, wakati si kitu sahihi. Tofauti kabisa na nchi nyingine ambako Meya anachaguliwa moja kwa moja na wananchi so usichanganye mambo mkuu.
 
kwa mtazamo wangu kiongozi au msemaji wa jiji la dar alipaswa kuwa kiongozi wa kuchaguliwa na si kiongozi wa kuteuliwa na rais kamwe. huku ni kuwadharau wananchi.
Meya si kiongozi wa kuchaguliwa na wananchi, au lini umewahi kupiga kura ya kumchagua Meya ? Meya anachaguliwa na madiwani na wabunge wa jimbo husika na sio wananchi. Kama ilivyo kwa Spika anachaguliwa na wabunge na sio wananchi vivyo hivyo Meya anachaguliwa na madiwani na sio wananchi.
 
Mstahiki Meya ni mtu mkubwa sana Marekani. Kwenye himaya yake kiongozi yeyote ambaye hana ridhaa ya wananchi (hakupigiwa kura) anawajibika kwake hata kama kateuliwa na shetani.
 
Back
Top Bottom