mwangalingimungu
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 1,301
- 733
Kwenye Toleo la leo la Mwananchi chini ya Kichwa cha Habari 'Phiri Atoa ya Moyoni', mwalimu huyo ameelezea jinsi anavyoiona Simba, vilabu vya Tanzania na mustakbali wa soka la nchi hii. Miongoni mwa maoni yake ni kuwa Simba haitafika popote iwapo itaendekeza mtindo wa kufukuza makocha kila baada ya muda mfupi. Kuhusu soka la Tanzania, alisema halitaweza kupiga hatua iwapo ubovu uliopo sasa kuanzia vilabuni wa kuendesha soka kisiasa zaidi hautashughulikiwa.
Sina sababu ya kuhoji maoni yake hayo; anayo haki kama mdau, ameona mengi kuliko ninayoyaona mimi nikiwa jukwaani na ana uzoefu na soka la nchi hii akiwa ameshafundisha kwa vipindi vitatu tofauti. Ninayemhoji ni mwandishi wa habari hiyo kwa kumwacha Kocha huyo na sisi wasomaji katikati ya safari.
Ningekuwa mimi ndiye niliyeongea naye, ningetaka kujua kwa nini basi akakubali kujiunga na Simba wakati akiyajua yote hayo, hasa ikitiliwa maanani kwamba (kwa ilivyoripotiwa) alikuwa tayari ana ofa ya Timu ya Taifa ya Namibia? Kuna yeyote anaweza kutusaidia kupata jibu humu JF?