Ningekuwa mwandishi ningeandaa "documentary" yenye kuonyesha athari za bomoabomoa

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,323
152,136
Raisi aliyeko Ikulu hawezi kujua ni namna gani zoezi hili la bomoabomoa linavyoathiri maisha ya watu kwenye familia hizi za waathirika wa zoezi hili.

Ni bahati mbaya sana mpaka sasa hata waziri wa ardhi ameshindwa kumshauri boss wake wasitishe zoezi hili japo kwa miaka miwili ili kutoa nafasi ya wananchi kuandaa makazi mbadala na sidhani kama kuna msaidizi yeyote wa raisi alietoa ushauri wa aina hii.

Binafsi ningekuwa waziri mwenye dhamana na zoezi hili, ningemshauri mh.Raisi asitishe zoezi hili walau kwa muda huo na kama angekataa basi ningejiuzulu uwaziri kuliko kuwa sehemu ya bomoabomoa hii.

Hivyo basi,kwasababu yote haya yamekwama,vyombo vya habari ni mhimili pekee unaoweza kufikisha ujumbe kwa mh.Raisi kupitia documentary maalumu itakayorushw katika vituo ya Television nchini na pengine picha hizo zinaweza kumuonyesha mh.Raisi uhalisia wa shida na mateso wanachi wake wanayopata na pengine angeguswa na kubadili msimamo wake.

Naamini kuna mengi hatuyajui juu ya athari za zoezi hili, ila kupitia kalamu na kamera zenu, tunaweza kujua mengi kuhusu maisha ya waathirika wa operation hii.

Waandishi timizeni wajibu wenu maamuzi muwaachie wenye mamlaka hata mwenyezi mungu atawabariki.
 
Last edited:
Hakuna haja yakuendelea kuishi kama kunguni, mie naunga mkono bomoa bomoa tuondokane na mabanda yasiopangiliwa. Kwa sasa tutalia ipo siku tutacheka.

Nadhan enzi mwl nyerere anaanzisha vijiji vya ujamaa na kubomolea watu, mlikuepo kama ninyi lkn leo tunafuraia mazao ya zoezi lile.

KAma isingekuwa vijiji vya ujamaa leo ardhi hii ingrkuwa ni damu tu kama saizi tu wafugaji na wakulima hawakai pamoja, vipi kama mwl nyerere angeacha familia moja moja iishi kwa kuhodhi maekari ya ardhi kwa kujitenga?

Tunataka viongozi wanaosimamia sheria, mie naunga mkono bomoabomoa hata kama ni kwangu bomeoeni nitalia nitanyamaza, sheria itakuwa imefanya kazi yake.

Wa tz watu wa ajabu sana, mafuliko, yakitokea mnalilia serikali, wakija kuwaondoa mnalilia serikali, nyumba zinaungua huko kwenye mabanda yasio na mpango kigogo na kwingineko fire wasipofika mnapiga kelele, wakitaka kuweka utaratibu napo tabu.

Bomoeni zote, kuanza upya si ujinga
 
Tumuite MohhammadAli wa Jicho Pevu. Maana tanzania hatuwezi sijui ni sheria au ni nini
 
Raisi aliyeko Ikulu hawezi kujua ni namna gani zoezi hili la bomoabomoa linavyoathiri maisha ya watu kwenye familia hizi za waathirika wa zoezi hili.

Ni bahati mbaya sana mpaka sasa hata waziri wa ardhi ameshindwa kumshauri boss wake wasitishe zoezi hili japo kwa miaka miwili ili kutoa nafasi ya wananchi kuandaa makazi mbadala na sidhani kama kuna msaidizi yeyote wa raisi alietoa ushauri wa aina hii.

Binafsi ningekuwa waziri Lukuvi, ningemshauri mh.Raisi asitishe zoezi hili walau kwa muda huo na kama angekataa basi ningejiuzulu uwaziri kuliko kuwa sehemu ya bomoabomoa hii.

Hivyo basi,kwasababu yote haya yamekwama,vyombo vya habari ni mhimili pekee unaoweza kufikisha ujumbe kwa mh.Raisi kupitia documentary maalumu itakayorushw katika vituo ya Television nchini na pengine picha hizo zinaweza kumuonyesha mh.Raisi uhalisia wa shida na mateso wanachi wake wanayopata na pengine angeguswa na kubadili msimamo wake.

Naamini kuna mengi hatuyajui juu ya athari za zoezi hili, ila kupitia kalamu na kamera zenu, tunaweza kujua mengi kuhusu maisha ya waathirika wa operation hii.

Waandishi timizeni wajibu wenu maamuzi muwaachie wenye mamlaka hata mwenyezi mungu atawabariki.

Mkuu Upo Tayari Nikupe Muongozo Wote Wa Kiuandishi Wa Habari Kisha Uifanye Hiyo Kazi Mwenyewe? Huwa Napenda Mno Watu Brave Na Risk Taker Kama Wewe Hasa Ukizingatia Kuwa Dunia Ya Sasa Ni Ya KIMAFIA Zaidi.
 
Mkuu hivi sasa niko chuoni na shule inabana sana.Asante kwa mchango wako.
 
Namshauri Magufuli atafute Bomu la Heroshima afumue maeneno yote anayofikiri hayajajengwa kwa kufuata sheria.

Kuanza Upya si Ujinga!
 
Raisi aliyeko Ikulu hawezi kujua ni namna gani zoezi hili la bomoabomoa linavyoathiri maisha ya watu kwenye familia hizi za waathirika wa zoezi hili.

Ni bahati mbaya sana mpaka sasa hata waziri wa ardhi ameshindwa kumshauri boss wake wasitishe zoezi hili japo kwa miaka miwili ili kutoa nafasi ya wananchi kuandaa makazi mbadala na sidhani kama kuna msaidizi yeyote wa raisi alietoa ushauri wa aina hii.

Binafsi ningekuwa waziri mwenye dhamana na zoezi hili, ningemshauri mh.Raisi asitishe zoezi hili walau kwa muda huo na kama angekataa basi ningejiuzulu uwaziri kuliko kuwa sehemu ya bomoabomoa hii.

Hivyo basi,kwasababu yote haya yamekwama,vyombo vya habari ni mhimili pekee unaoweza kufikisha ujumbe kwa mh.Raisi kupitia documentary maalumu itakayorushw katika vituo ya Television nchini na pengine picha hizo zinaweza kumuonyesha mh.Raisi uhalisia wa shida na mateso wanachi wake wanayopata na pengine angeguswa na kubadili msimamo wake.

Naamini kuna mengi hatuyajui juu ya athari za zoezi hili, ila kupitia kalamu na kamera zenu, tunaweza kujua mengi kuhusu maisha ya waathirika wa operation hii.

Waandishi timizeni wajibu wenu maamuzi muwaachie wenye mamlaka hata mwenyezi mungu atawabariki.
Labda tumkodi yule Mwandishi wa Kenya wa "jicho pevu" ....!
 
Hiyo documentary itakuwa nzuri zaidi ikiwa itaonyesha jinsi gani maeneo hayo yalivyokuwa kabla hayajavamiwa na watu, halafu itakuwa nzuri zaidi ikiwa mtayarishaji ataonyesha jinsi maafisa ardhi wanavyochukuwa rushwa na kuruhusu ujenzi ufanyike kiholela. Na itakuwa nzuri na yenye kuacha legacy kwa muda mrefu ikiwa itaonyesha jinsi gani wakati wa mvua za masika watu hao hao wanavyohangaika kupanda juu ya dari za nyumba ili kukwepa kuchukuliwa na maji ya mvua yasiyokuwa na msalie mtume. Documentary hiyo itakuwa na thamani kubwa na itauzika kimataifa ikiwa itagusa pande zote zinazohusika na isiwe na lengo la kuwanyooshea kidole watu fulani wachache. Ni wazo zuri likifanyiwa kazi kitaalam na ukweli ni kwamba litahitaji muda mrefu. Kila la kheri katika uandaaji wa hiyo documentary.
 
Ujenzi holela na uvamizi wa maeneo siuungi mkono.. nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria. acha serikali ifanye kazi yake! Haya machungu yataisha tu. Na tutasahau na baadae tutakuja kuimwagia sifa kemkem kama serikali inayofanya maamuzi magumu kwa maslahi mapana ya taifa.
 
hadi sasa karibu ya watu 30 wamepoteza maisha kwa ajili ya kadhia hii. mamia wapatwa uchizi na maelfu presha hazishuki.
 
Hakuna haja yakuendelea kuishi kama kunguni, mie naunga mkono bomoa bomoa tuondokane na mabanda yasiopangiliwa. Kwa sasa tutalia ipo siku tutacheka.

Nadhan enzi mwl nyerere anaanzisha vijiji vya ujamaa na kubomolea watu, mlikuepo kama ninyi lkn leo tunafuraia mazao ya zoezi lile.

KAma isingekuwa vijiji vya ujamaa leo ardhi hii ingrkuwa ni damu tu kama saizi tu wafugaji na wakulima hawakai pamoja, vipi kama mwl nyerere angeacha familia moja moja iishi kwa kuhodhi maekari ya ardhi kwa kujitenga?

Tunataka viongozi wanaosimamia sheria, mie naunga mkono bomoabomoa hata kama ni kwangu bomeoeni nitalia nitanyamaza, sheria itakuwa imefanya kazi yake.

Wa tz watu wa ajabu sana, mafuliko, yakitokea mnalilia serikali, wakija kuwaondoa mnalilia serikali, nyumba zinaungua huko kwenye mabanda yasio na mpango kigogo na kwingineko fire wasipofika mnapiga kelele, wakitaka kuweka utaratibu napo tabu.

Bomoeni zote, kuanza upya si ujinga

wew ndo minus kabsa wakat wanajenga hayo mabanda mbona hawakuwaambia mpaka watu wamekuwa na uhakika wa makazi yao ndo wabomolewe c bure itakua unalala bar wew hata uchungu wa kujenga hujui
 
Unataka wapewe miaka miwili, Kwani kwa miaka 20 sasa wameshaambiwa waondoke mabondeni lakini bado wanang'ang'ania. Badala yake wanazidi kujenga nyumba zaidi.
 
Back
Top Bottom