Tanganyika1
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 422
- 86
Wakuu leo j3 ya pasaka niko nyumbani nikiwa napitia gazeti la mwananchi nimekutana na habari iliyo nifanya niandike hapa. Katikati ya gazeti kuna jarida la mwananch 2 ambalo ni maalum kwa habari za michezo. Ukururasa wa 3 wa kijarida hiki kuna picha kubwa ikimwonyesha mchezaji wa barcelona na goli kipa wa ac millan wakiwa chini wakiwania mpira katika ligi ya mabingwa ulaya....ajabu ni kwamba mwandishi huyu amjinga mechemka kwa kusema kuwa yule ni ki wa barcelona wakati hata ukiangalia jezi ya goli kipa yule ni ya ac millan....zaidi ni kwamba huyu mwandish amekariri kuwa daniel alves kuwa mara zote ni beki wa barcelona wakati mara nyingine huwa ni right wing wa timu hiyo na siku ya mchezo wao na millan hakua beki bali alicheza namba 7. Rai yangu ni kwamba hizi kazi wapewe watu wenye sifa jamani. Mana huyu mwandish nadhani atakua amevamia fani kwani makosa alio yafanya yana bainisha kuwa ana ufahamu mdogo sana wa mambo ya michezo na bado anaandika habar za michezo.